Kiswahili fasaha kinatoweka

du
kazi ipo
 
daah pole sana kiongozi.

tatizo kuna walimu hawajitambui namna wanavyoweza kuathiri maisha ya wanafunzi kwa matendo yao tu.
 
maneno kama vile mhanga ,mwathirika ,rindima na zizima huwa mara nyingi yanatumika ndivyo sivyo.
 
Shukran Wakili Msomi Ngabu, hebu tunaomba utuwekee hapa hizo picha tujifunze zaidi.

Lakini pia nikutonye sikio kwamba, hata watu wenye elimu za juu sana wanaweza kufanya makosa ya kijinga sana mpaka ukashangaa.

Ninaheshimu elimu zao na kwa kweli ninakiri ni watu manguli mno wa Lugha, lakini makosa ya kimaskhara kwenye kazi zao ni jambo la kutarajia kwa wakati mwingi.

Hao oxford nadhani wananakili taarifa kutoka TUKI na taasisi zingine za elimu ya Kiswahili na kuzifanyia uhariri kidogo, kwahiyo kuna uwezekano mkubwa wa kubeba na makosa yaliyomo.
 
Naomba niwe tofauti kidogo nanyi.
Lugha yoyote huwa inabadilika over time. Old English haifanani na kiingereza tunachoongea leo. Sawa na Kiswahili cha zamani. Ukimfufua mtu aliyekufa mwaka 1970 leo mzungumze Kiswahili hamtaelewana.

Kufanikiwa.....kujipata, yote ni maneno ya Kiswahili, na lugha ni sauti za nasibu, kama tunaelewana na ikakubalika ndio basi unakuwa msamiati mpya. Shida iko wapi? Ndio maana kuna maneno mapya yanazuka kama vile UNYAMA SANA, MUKIDE........

Unataka tuongee lugha za uandishi? Kama vile mzungu akiongea Kiswahili, yeye anaongea cha kujifunza kwenye vitabu.
 
Bongo fleva pia inachangia sana kuua lugha ya taifa
 
Kwakweri habali hii inakela sana sipendi kiswahiri kikichezewa hivyo ndo mahana najitorea kufundisha kiswahiri
 
Dah! Kutoka mbeba maboksi mpaka wakili msomi! Umenipendelea sana. Usomi huo mi mbeba maboksi niutoe wapi? 😀

Hata hivyo, ahadi ni deni. Nimechoka kama mbwa, lakini naamini katika kutimiza ahadi.

Haya, twende kazi;

Kama nilivyosema hapo awali, maneno yote mawili, ‘onesha’ na ‘onyesha’, ni sahihi.

Neno sahihi katika kuelezea utumikaji wa hayo maneno ni ‘kibadala’ au ‘vibadala’. Kwa kimombo nadhani ni ‘alternate’.

Kama picha ya sehemu ya ukurasa inavyoonyesha hapo chini, kibadala ni moja kati ya maneno mawili au zaidi yanayotofautiana kidogo kwenye maandishi au matamashi, lakini yanakuwa na maana sawa; onyesha/ onesha. Na unakumbuka niliongelea mambo ya lahaja? Hata wao watu wa TATAKI wamelizungumzia hilo [2009 walibadili jina kutoka TUKI]. TATAKI ni Taasisi ya Taaluma za Kiswahili.



Uzuri wa hizi kamusi za siku hizi, huwa zina maelezo mazuri sana kuhusu masuala ya lugha.

Kwa mfano, moja ya hizi kamusi nilizonazo ina orodha kabisa ya vibadala vya maneno na mojawapo ya hayo maneno ni ‘onyesha’ na ‘onesha’.



Huu hapa ukurasa yaliyopo hayo maneno.



Hapa chini ni kipande cha ukurasa wa kamusi ya Kiswahili sanifu tu. Yaani Kiswahili peke yake.

Angalia hayo maneno ‘onesho’ na ‘onesha’ utaona yakifuatiwa na neno ‘pia’ “onyesho “ na “onyesha”.



Hiyo’pia’ maana yake ni kwamba hicho kibadala cha hilo neno, nacho ni sahihi pia!

Tukienda kwenye kamusi ya Kiingereza.- Kiswahili, neno ‘show’ wao wamelitafsiri kama ‘onyesho’.



Hii hapa orodha ya watu waliohusika kuzitengeneza hizi kamusi. Wachache kati yao nafahamiana nao. Ni watu wanaoaminika kwa uwezo wao kwenye fani yao.



Haya bana, baadaye. Nimechoka kama mbwa koko leo.

✌️
 
Wakili Msomi Ngabu umeupiga mwingi mno hapa, ndio maana nimekutunuku uwakili bila kupitia mafunzo ya Law School.

Unastahili tunu ya uwakili japokuwa hii si tiketi au garantii ya wewe kuacha kubeba maboksi. Endelea. Chakula ni muhimu zaidi kuliko uwakili.

Nikirejea kwenye ujumbe wako hapa, niseme tu kwamba, hichi kibadala cha ONESHA vis-a-vis ONYESHA ni kibadala TATANISHI mno kwenye akili yangu na kiukweli kinanitusi ujuzi wangu wa Lugha.

Hawa manguli wa lugha siwapingi kwenye hili na ninawaheshimu mno, lakini wameninyong'onyeza na kunisikitisha mpaka najiuliza inawezekanaje kosa la kimaskhara kama hili likachukuliwa na kudhaniwa ni Kiswahili sanifu ati kwa msingi kuwa ni KIBADALA!

Kwa kutumia msingi wa maelezo yao ya utangulizi wa maana ya KIBADALA, nimegundua kuwa wameridhia usanifu wa neno ONYESHA kwa sababu linatumika sana miongoni mwa watu kama LAHAJA MBADALA.

Hii ni hoja fikirishi na yenye utata, kwa sababu watu wengi wanaotumia Lugha hawana weledi au upeo, na wanaweza kutengeneza maneno yao mabovu yasiyo na usahihi wa kisarufi au usanifu.

Kuyachukua maneno ya hawa watu wasio na upeo wa Lugha na kuyaingiza rasmi katika Kiswahili sanifu ni kututusi sisi wenye ujuzi na umahiri wa Lugha.

Lakini nitasema nini? Manguli wameshaamua.

Nimeridhika kinyonge sana. Kama kungekuwa kuna Baraza la Kukata rufaa kwa mambo yanayohusu usanifu wa Lugha, ningekata rufaa na kuomba hili neno LITENGULIWE au lihakikiwe upya usahihi wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…