NN kwa hiyo hapo inaonyesha kuna sababu za msingi na zisizo za msingi.
Wengi ya watu wanaoandika/ongea hivyo huwa Kiswahili wameanza kujifunza walipoanza shule na si lugha yao ya mwanzo.
Wanatibua sana, hususani wale wanao changanya kwenye R na L, lakini tutaendelea kuwapa darsa, humu JF wangi waliokuwa wakifanya makosa hayo wamejirekebisha.
Yeah...unaweza kabisa kusema kuwa zipo sababu za msingi na zisizo za msingi. Kwa mfano, mtu ambaye anaandika "alafu" au "afu" badala ya "halafu" huku akijua "alafu" au "afu" si sahihi utaiweka hiyo kwenye kundi gani?
Naweza Sema karibu kila post haswa ikiwa ni yenye maneno mengi huwa haikosi kasoro,na utakuta mtu anapost baadae akiipitia anakuta makosa kadhaa tizma utaona last edit was date dash dash.
Mimi ni mhanga mmojawapo wa R na L ila huwa siogopi kutumia popote nikiwa nahitaji kufikisha Ujumbe Na Ukinikosoa huwa napata Faraja zaidi hata miaka ya Nyuma tunachat kwenye hizi chat zetu marehemu za Bongo5 chat DHW Jambo Darchat nilikuwa natupa mawe ya R na L bila wasi wasi na walikuwa wananiweka sawa.
Kiswahili nimezaliwa nacho na ninacho bado japo sikipendi nadhani Tuliingizwa mkenge na JKN kukiendekeza mashuleni hakijatusaidia sana kwenye maendeleo ya kimataifa kuna wanaopinga ila ukweli hujitenga Uganda na kenya wamewahi
Wachaga hawana ''Z'' Huweka ''S'' Mfano Sa Saa hisi = Za Saa Hizi
Wakurya Mwendo ni ''R'' Kwenda mbele Rirete hiro ri mwizi turiarest Rione rimenyoa V
Wavisiwani wengi wapo sawia
<br />Wengi ya watu wanaoandika/ongea hivyo huwa Kiswahili wameanza kujifunza walipoanza shule na si lugha yao ya mwanzo.<br />
<br />
Wanatibua sana, hususan wale wanao changanya kwenye R na L, lakini tutaendelea kuwapa darsa, humu JF wangi waliokuwa wakifanya makosa hayo wamejirekebisha.
Kama mtu akiandika hivyo wakati anajua wazi sivyo, hapo hakuna sababu ya msingi. Lakini mbona hii imejikita zaidi kwenye Kiswahili? Unafikiri mtu anayechanganya "R" na "L" kwenye Kiswahili kwa sababu za msingi au zisizo za msingi anaweza kuchanganya kwenye Kingereza? Mfano "rike" badala ya "like", Engrish" badala ya "English".
Yawezekana japo huwezi kuwa na asilimia nyingi. mie hunichangaya haswa neno lenye R na L ndani yake Kama waluguru Sielewi ni Waluguru , Warugulu au Waruguru Walugulu Sijui lipi ni Sawa ila nikiwa nataka kufikisha ujumbe naweka lolote hapo msg Sent Hapo Vipi!Mkuu hapo kwenye red hata mimi nakosea sana spellings. Lakini kwa hili la kutumia "R" badala ya "L" sidhani kama lina uhusiano mkubwa sana na spelling. Wapo watu unakuta wamefanya editing lakini hawa edit walipotumia "R" badala ya "L" labda kwa sababu za msingi.
Nadhani wengine ni kutokana na matatizo ya utamkaji tu, kama vile wale wenye kithethe...! Wamezaliwa hivyo na hawawezi rekebishwa.
Ndio maana mimi wakati mwingie humpa maiwaifu wangu kuhakiki kile ninacho wasirisha/kiwasilisha hapa! Japokuwa mimi ni mwana kindakindaki pale Gerezani Kariakoo, mitaa ya Livingstone, Somali na Kidongo Chekundu.
Ah! Kiswahili kitamu bana ukikijuwa (ukikijua).
Ukizowea/ukizoea kusema kwa kuchanganya R na L, basi kuna hatari ya kuandika vile unavyo tamka.Hiyo sawa kabisa mkuu, lakini tatizo linakuja pale matamshi yanapoanza kufanana na maandishi!