Kiswahili: Matumizi ya Herufi “L” na “R”

Tatizo hili naona limekuwa kubwa sana kwenye matumizi ya kawaida na wakati mwingine hadi kwenye matumizi Rasmi ya Lugha yetu ya Kiswahili. Inanonesha kwamba watu wengi labda kutokana na Lugha zao za asili wanashindwa kabisa kutofautisha matumizi ya her " L " na " R " wakati wanafanya uandishi wa maandiko yao.

Mtu badala ya kuandika "Jaribu" yeye ataandika "Jalibu", au wengi wetu hatuwezi kuandika "Dharula" badala yake tunaandika "Dharura" na mengine mengi yanayohusisha matumizi ya herufi hizo mbili.
 
Allen hata na wewe kiswahili kinakupiga chenga kwani neno sahihi ni dharura na siyo DHARULA
 
Kwa hiyo ni kiswahili tu, vp lugha nyingine wanatamka itakikanavyo?
 
Mleta mada na wewe pia Kiswahili kinakupiga chenga.... kwa ujumla mada yako ni nzuri nami pia hukerwa sana na matumizi mabaya ya hizo herufi na nyinginezo pia mfano badala ya kusema 'ipo' mtu ana sema 'hipo'
 
Hilo ni tatizo la wengi aisee..Afadhali mtoa mada umedhihirisha ilo pia
 
Kweli kabisa aiss...mara kadhaa nimekuwa nikiandika erection badala election....in tanzania we have general "erection" once in every five years...
 
tatizo hili si dogo,
...kuna mwalimu wangu mmoja alileta swali fulani na majibu mawili yakiwa ni 1) river 2) liver. na ni ya multiple chice, ikawa balaa, pale mto unapotajwa kuwa ni ini!
 
Wanakera sana kwa kweli. Bora kutamka sio kesi ila katika kuandika hapana kwa kweli ni u Bhanunu.
 
okonkwo jr miye siyo kilaza wa Lugha hii adhimu. Dharula ndiyo neno sahihi na wala siyo "dharura". Nikwambie tu wengine tulishiriki kwenye vita kati ya siye tuliokuwa tunadhani matumizi sahihi ya neno linalotakiwa kuashiria uelekeo ni "onyesha" na siyo "onesha" na wale waliokuwa wanaamini kinyume chake, bahati mbaya sana tulishindwa vita ile baada ya mapambano mengi sana. Kama una ushahidi kuwa neno sahihi ni DHARURA na siyo DHARULA basi uuweke hapa Jamvini.

Preta, bitimkongwe 42_007 nziriye Manyunchwi Zamaulid SaaMbovu Kaboom hii lugha ya Kiswahili tunaitumia kwa mazoea lakini wakati mwingine huwa tunaipotoa!! Nimeona brawn shao kaathiriwa labda na lugha yake ya asili badala ya kuandika "thamani" akaandika "dhamani" Tujifunze wote kwa pamoja!!
 
Last edited by a moderator:

Mie nafahamu ni Dharura na sio kama unavyo sema.
Hii hapa ni kamusi ya TUKI.
 
Attachments

  • 1448962283295.jpg
    1448962283295.jpg
    128.1 KB · Views: 263
Last edited by a moderator:
SaaMbovu Nakubaliana na wewe kabisa, hapa ni kama yale mabishano ya "Onesha" na "onyesha" yalivyokuwa. Hapo mwanzo tulitumia neno "dharula" na kama TUKI (nawaheshimu sana) wametoa toleo jipya kuonesha kwamba "dharura" ndiyo neno sahihi hapo nina cha kujifunza!! Lakini amini kuwa kuna Kamusi mbali mbali wanalitambua neno "dharula" na wala siyo "Dharura". Je hao watu wa TUKI waliathiriwa na mmoja wao ambaye matumizi ya "L" yameathiriwa na matumizi ya "R" badala ya "L" toka kwenye lugha yake ya asili!?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom