Kiswahili: Matumizi ya Herufi “L” na “R”

Kiswahili: Matumizi ya Herufi “L” na “R”

bora mtu aongee tu lakini hadi kwenye uandishi jamani khaaa.. ninachukia from the heart kukutana na hayo mambo .... ukitaka kunichefua niletee tu hizo habari za mara umekura tayali... umerara, razima huje.... mwingine bila haya kabisa anaandika sorution badala ya solution... aaah kero kwa kweli.
 
Asante SaaMbovu.

Bwa Allen Kilewella mimi ni mzaliwa wa pwani ambaye nimekulia pwani, kiswahili ni lugha yangu na sina nyengine kabisa, na nimesoma kiswahili na kupasi vizuri mpaka form six.

Sijawahi hata siku moja kusikia mswahili akiita dharula.
Una hakika kuwa hakuna matumizi rasmi ya neno Dharula? Mimi siyo tu nilizaliwa Pwani lakini pia nimekiishi kile kiswahili kisichobebwa na maneno lukuki ya kutoholewa au ya kukopa. Kwa mfano wewe badala ya kusema kuwa "ulipasi vizuri" ulipaswa useme "ulifaulu vizuri" au sivyo mswahili mwenzangu?
 
Una hakika kuwa hakuna matumizi rasmi ya neno Dharula? Mimi siyo tu nilizaliwa Pwani lakini pia nimekiishi kile kiswahili kisichobebwa na maneno lukuki ya kutoholewa au ya kukopa. Kwa mfano wewe badala ya kusema kuwa "ulipasi vizuri" ulipaswa useme "ulifaulu vizuri" au sivyo mswahili mwenzangu?

ukichambua kiswahili utakuta ni mchanganyiko wa lugha nyingi, nyengine za kienyeji na nyengine (siyo nyingine) za kigeni. Kiswahili cha kwenu bara kina asili ya mchanganyiko wa maneno mengine ya kidachi, lakini cha visiwani kina asili ya baadhi ya maneno ya kiingereza (skuli, kupasi...), kiarabu (mengi sana soko, karibu na hata hilo dharura likiwemo), kihindi (chai, chapati..) na kireno (meza, pesa..) nadhani mifano ni mingi sana.
 
bitimkongwe asili ya maneno kwenye lugha yoyote ile hayatokani na asili moja. Nakubaliana na uasili wa maneno hayo lakini kumbuka kuwa utamkaji wa maneno nao pia huathiri uandishi wake. Kwa Mfano wahehe wengi hawawezi kuandika neno "hamna" badala yake huandika "hamuna". Neno "kupasi" na mengineyo ya Kiingereza kwa bahati mbaya wewe unadhani yanatumiwa na watu wa visiwani (Bila shaka ulitaka kumaanisha Zanzibar) pekee lakini sivyo.

Kupasi na mengineyo ya Kiingereza yanatumiwa sana Zanzibar kwa kuwa Kiswahili chao kilikosa misamiati inayowiana na tendo husika. Utaona neno "Marikiti" ni la kawaida sana Zanzibar kama lilivyo neno "Bomba" likimaanisha Kipaza sauti au "mfereji" likimaanisha Bomba la maji!

Hoja yangu ni kwamba nyie mnaodai neno "Dharura" ndiyo sahihi dhidi ya "Dharula" ni budi kwenu kufanya utafiti na kujua kama neno dharula halijawahi kutumika au ni lini neno dharura limeanza kutumika kwenye kiswahili Rasmi. Halafu mimi si wa bara ingawa ni M-bara ninayeishi bara!!
 
Last edited by a moderator:
Mimi mtu alinitumia message kuwa yupo "teali" Nilihairisha na hiyo safari kabisa.
 
Hivi ni........Nilihairisha au Niliahirisha..........nimeshachanganyikiwa tayari.......

Usichanganyikiwe, nafikiri "Niliahirisha" ni sahihi.
Vipi kuhusu
zambi na dhambi
ng'ombe zangu na ng'ombe wangu.
 
Back
Top Bottom