Kiswahili: Methali, Vitendawili, nahau, Misemo n.k

Kiswahili: Methali, Vitendawili, nahau, Misemo n.k

ukiona zinduna ambari iko nyuma,kata pua uunge wajihi,joka la mdimu hulinda watundao,
 
ukiona zinduna ambari iko nyuma

ni sawa na kusema ukimuona mke anapita mumewe yupo nyuma anakuja

vitu vinavyofuatana
viwe vizuri au vibaya lakini huenda pamoja kwa kufuatana kimoja mbele kingine nyuma
 
ukiona zinduna ambari iko nyuma

ni sawa na kusema ukimuona mke anapita mumewe yupo nyuma anakuja

vitu vinavyofuatana
viwe vizuri au vibaya lakini huenda pamoja kwa kufuatana kimoja mbele kingine nyuma

joka la mdimu hulinda watundao, Tafsiri yake ni kuwa "kuna nyoka ambaye yeye hukaa kwenye mti wa mdimu (ndimu) hali ndimu lakini huwadonoa wale wanaokuja kuchuma hizo ndimu"

Maana yake ni sawa na mtu anayezuia wenzake kupata wanachokitaka ilhali yeye mwenyewe hakihitaji hicho wakitakacho..........(roho ya kwa nini)
 
Hii pia kwa lahaja ya kimrima na Mtang'ta husemwa Mkyama ago kanyele hwenda akauya papo
Mchama ama Mkyama = ni muhamaji
Ago au huitwa Rago = ni sehemu watu huhamia kufuwata kazi kama vile zamani watu hufuwata kazi wakati wa msimu wa karafuu kule Pemba , sasa wanapohamia pale kukaa kwa ajili ya kazi paitwa AGO ama RAGO ,
kwa hiyo mtu hupanyei huwenda ukaja tena kufata kazi halafu utakaa wapi ? na wewe umeshapachafuwa ?
 
habari wanajamvi,

naombeni msaada wa vitendawili hivi:

"mbuzi wangu hula udongo tu."

"watoto wa tajiri wa nguo hulala na kutembea uchi."

Kuna mdogo wangu hapa amepewa HW tafadhali nisaidien.

Natanguliza shukrani zangu kwenu!
 
Kweli kiswahili kigumu sana au hakuna mabingwa wa kiswahili humu jamvini!
inamaana kweli maana ya vitendawili hivyo imeshindikana kuipata hapa jamvini??
 
mkuu iyo ya pili ni maboga lakini kwa sentensi ya kwanza mi mwenyewe imenipiga mtama
 
Back
Top Bottom