Mr Kiroboto
JF-Expert Member
- May 3, 2008
- 350
- 90
Haya muungwana mpaka buje na hii buje nayo ni kiswahili ama kifaransa ?
Hii Pedejee inanikumbusha yule mzaa Makaranga kule ilala miaka ile wanaomjua bado yupo ? ila yeye alikuwa mcha mungu.
SAHIBA.
maneno mengi ya kigeni ambayo yametoholewa huwa si sahihi kutumika katika kiswahili sanifu.Hilo neno pedejee bado halijasanifiwa.
mfano neno either ambalo baada ya kutoholewa likawa aidha,lakini si sahihi kutumia neno hilo katika kiswahili sanifu.
Yeah...I guess kuwa Pedejee is in now....(kwa bongo, of course)
Samahani hapa kidogo nataka kuhitilafiana: neno aidha ni neno la kiarabu na kiingereza wamelipatia huko na kulifanya either. Na mengi kama vile Ardhi = Earth, Bila-ain = Blind kwa kiingereza. Kwa mfano huo yapo pia maneno ya kiingereza au kifaransa yaliyojiingiza katika kiarabu au kwa lugha nyingine yeyote ile.
YOYOTE ndilo neno sahihi hapo. YEYOTE inamaana ya MTU ama MNYAMA lakini kwenye vitu visivyo uhai haifai kutumia yeyote.
Kiswahili kitamu sana kukizungumza kwa ufasaha.
Samahani hapa kidogo nataka kuhitilafiana: neno aidha ni neno la kiarabu na kiingereza wamelipatia huko na kulifanya either. Na mengi kama vile Ardhi = Earth, Bila-ain = Blind kwa kiingereza. Kwa mfano huo yapo pia maneno ya kiingereza au kifaransa yaliyojiingiza katika kiarabu au kwa lugha nyingine yeyote ile.
Mkuu ndio maana nikasema sio kiswahili sanifu.katika kiingereza kuna "either......or",sisi katika kiswahili fasaha tuna "ama.............au" na sio aidha.
QM, naomba kujaribu.
Maneno sahihi kwa maoni yangu kama vile ulivyo orodhesha ni:
1. hujasikia
2. istahili
3. yahitajiyo
4. unaipa
Tafsiri:
Inspirational - Yakutia mori/morali. Au kutia moyo, kuriwaza mtima.
Show - onyesha, jidai, funua, fichua, hadhara
Widow - mjane (mwanamke)
Widower - ....sijui