KISWAHILI: Naomba maana ya maneno haya...

KISWAHILI: Naomba maana ya maneno haya...

Haya muungwana mpaka buje na hii buje nayo ni kiswahili ama kifaransa ?

Hii Pedejee inanikumbusha yule mzaa Makaranga kule ilala miaka ile wanaomjua bado yupo ? ila yeye alikuwa mcha mungu.

SAHIBA.

teh teh
unanikumbusha mzee wa totoz(sakisi).Hilo neno buje ni kifaransa maana yake " move"
 
maneno mengi ya kigeni ambayo yametoholewa huwa si sahihi kutumika katika kiswahili sanifu.Hilo neno pedejee bado halijasanifiwa.

mfano neno either ambalo baada ya kutoholewa likawa aidha,lakini si sahihi kutumia neno hilo katika kiswahili sanifu.

Samahani hapa kidogo nataka kuhitilafiana: neno aidha ni neno la kiarabu na kiingereza wamelipatia huko na kulifanya either. Na mengi kama vile Ardhi = Earth, Bila-ain = Blind kwa kiingereza. Kwa mfano huo yapo pia maneno ya kiingereza au kifaransa yaliyojiingiza katika kiarabu au kwa lugha nyingine yeyote ile.
 
maana yake ni PDG yaani presidaa director generale kwa kifaransa! asili ya hili imetoka kongo ambao wanazungumza kifaransa na wanapewa watu fulani ambao mambo yao yako safi kwenye nyanja fulani....sasa wao wanachukua kifupi cha maneno hayo matatu na badala ya kutamka piidigii wanatamka pedeg^ee
 
Samahani hapa kidogo nataka kuhitilafiana: neno aidha ni neno la kiarabu na kiingereza wamelipatia huko na kulifanya either. Na mengi kama vile Ardhi = Earth, Bila-ain = Blind kwa kiingereza. Kwa mfano huo yapo pia maneno ya kiingereza au kifaransa yaliyojiingiza katika kiarabu au kwa lugha nyingine yeyote ile.

YOYOTE ndilo neno sahihi hapo. YEYOTE inamaana ya MTU ama MNYAMA lakini kwenye vitu visivyo uhai haifai kutumia yeyote.
Kiswahili kitamu sana kukizungumza kwa ufasaha.
 
Samahani hapa kidogo nataka kuhitilafiana: neno aidha ni neno la kiarabu na kiingereza wamelipatia huko na kulifanya either. Na mengi kama vile Ardhi = Earth, Bila-ain = Blind kwa kiingereza. Kwa mfano huo yapo pia maneno ya kiingereza au kifaransa yaliyojiingiza katika kiarabu au kwa lugha nyingine yeyote ile.

Mkuu ndio maana nikasema sio kiswahili sanifu.katika kiingereza kuna "either......or",sisi katika kiswahili fasaha tuna "ama.............au" na sio aidha.
 
Mkuu ndio maana nikasema sio kiswahili sanifu.katika kiingereza kuna "either......or",sisi katika kiswahili fasaha tuna "ama.............au" na sio aidha.

aidha ya kiswahili ina maana ya vilevile/na, sio kama either ya kiingereza ambayo humaanisha ama/au/kama sio.
 
Hawa mapedeshe ndio wanaotuharibia watoto wetu wakike wenye miaka 18-25 lakini kama walivyosema wengine ni mitaa ya uswahilini sio upanga,seaview,oysterbay,masaki, mikocheni etc.
 
Nimatumani yangu kuwa wote wana JF ni wazima, nilikuwa naomba nipatiwe jibu kuhusu hawa watu wanaojiita MAPEDEJE AU PAPA nimefanya uchunguzi wangu binafsi nikagundua wengi wao ni matapeli wanawatapeli wazungu madini feki na wengine wanafanyabiashara za magari ya wizi,wengine kuiba benk kwa njia ya mtandao, je ili uwe pedejee hizi ndizo sifa zinazotalikiwa na upedejee maana yake nini?
 
Kuhusu mtambo ni tarakishi au afadhali tarakilishi. Sawa vilevile ni kompyuta (angalia Tarakilishi - Wikipedia). "Ngamizi" ilikuwa tu pendekezo la kampuni ya Microsoft ("kadogokalaini") lakini halitumiwi hali halisi.

"Mtandao" hutumiwa sawa na "intaneti"; kwa "lugha ya mtaani" (lakini mtandaoni) unasikia pia "kwenye nyavu". Ni ile mawasiliano ya tarakilishi pamoja na habari zinazotunzwa kwenye mashine hizi zinaziweza kuwasiliana kati zao kote duniani. (angalia: Intaneti-Wikipedia ).
 
Sijui kama umeshapata maana yake "unyanyapaa". Ikiwa hapana, neno hili lina maana ya kutokubali kumtambua mtu, kutoshirika naye, kumwacha kando n.k. Kamusi Sanifu ya Kiswahlili inasema ifuatayo: -nyanyapaa = kuepuka mtu kwa dharau na kumwona kama kinyaa au mchafu

Kwa Kiingereza ni "to ostracise", "to send to Coventry", "to have no dealings with" etc. Siku hizi husikika neno hilo kwenye muktadha ya wale wenye ulemavu hasa maalbino.
 
Tafadhali rafiki zangu tutumie Kiswahili! Mbona kutotumia "mstari wa kwanza", "mstari wa pili" (kama A.E. Musiba afanyavyo kwenye riwaya yake "Hofu").
 
Kichuguu, Mkuu wangu una hakika neno AJUA limetokana na maelezo yako maanake navyofahamu mimi limetokana na neno la kiingereza - As You are!
Jaribu kuulizia tena..
 
QM, naomba kujaribu.

Maneno sahihi kwa maoni yangu kama vile ulivyo orodhesha ni:

1. hujasikia
2. istahili
3. yahitajiyo
4. unaipa

Tafsiri:

Inspirational - Yakutia mori/morali. Au kutia moyo, kuriwaza mtima.

Show - onyesha, jidai, funua, fichua, hadhara

Widow - mjane (mwanamke)

Widower - ....sijui

---
widower Mgane
 
Back
Top Bottom