Kitabu cha Enoch kinawataja malaika 200 walioasi ambao ndio waliiba Siri na teknolojia za mbinguni kisha wakamfundisha Binadamu


Ukisoma kitabu cha Jasher kinaeleza kuwa Tera alikuwa moja ya watumishi wa Ikulu ya Nimrodi(mjukuu wa Hamu) ambaye alikuwa mfalme wakati huo.

Tera alikuwa mchonga vinyago vya miungu hapo Uru. Naye alikuwa anatumikia miungu aliyoichonga.
Ibrahim alienda kwa Nuhu Babu wa Babu zake sio kwa kupenda bali ni baada ya tukio la usiku wa kuzaliwa Ibrahim ambapo tukio la kuogofya lilitokea na wanajimu wakamshauri Nimrodi amuue mtoto wa Tera kwani mtoto huyo nyota yake ilionyesha kuwa atakuwa mwiba kwenye utawala wa Nimrodi hapo baadaye.

Tera akampeleka mtoto wa mwingine wa mfanyakazi wake badala ya Ibrahim na Ibrahim akaenda kumficha mapangoni kwa zaidi ya miaka 10.
Alipofikisha miaka hiyo 10 ndio wakampeleka kwa Nuhu kumficha.
Nuhu alikuwa akiishi na Shem mtoto wake na babu wa kina Ibrahim.
 
Binafsi naona umezunguka sana. Nilitaka kwanza uweke kitabu ambacho kwa maoni yako kingetakiwa kutoka halafu ndo ungenipa hili darasa. Kama ingekuwa ni sehemu inayohitajika jibu la swali sidhani kama hayo maelezo yangejitosheleza.
 
Kaka katika hadithi ya ya Enoch ina maana Mungu anajua mwanzo wa Dunia kama Biblia inavyosema sasa mbona kuna sehemu Mungu alikuwa hajui kinachoendelea mpaka anaelezewa

Anajua lakini anafuata kanuni na sheria alizojiwekea.
Kwa mfano Mungu aligawa mamlaka kwa viumbe wengine IKIWEMO wewe kuongoza katika level yako. Sio kama yeye alishindwa kufanya hivyo.
Mfano, Mungu alikupa uzao alafu utakapozaa akakupa wajibu na mamlaka ya kumlea mtoto. Sio kwamba yeye hawezi kufanya hivyo.

So unapoenda mbele zake lazima akuulize maswali ili wewe uliyepewa kazi utoe ripoti ya nini umefanya na nini kimekushinda.

Mungu sio Much Knows ingawaje anajua Kila kitu.
Hiyo inatufundisha kuwa hata kama jambo unajua lakini kama halipondani ya mamlaka yako waachie wenye mamlaka nalo walisemee
 

Umejadili kisayansi zaidi Mkuu. Shukrani sana
 

Kitabu hicho na vingine Bado vinanipa picha kuwa mambo mengi ni marudio. Lakini pia vinatoa picha kuwa binadamu sio kiumbe pekee mwenye akili ingawaje tunajipa faraja
 
Leo shetani katetewa hakuhusika na udanganyifu wa Adam kula tunda ...mkuu umetisha izo reference zitunze bwana Lucifer anaeza kuja kakutumia kama shaidi
 
Kiranga
Uzi unahitaji maoni yako huu!
Unakizungumziaje kitabu cha Enoch? Vipi kuhusu sayari ya Nibiru kubeba hatma ya maisha yetu hapa duniani!?
 
Miaka 2000 linaweza kutokea janga ambalo hakuna historia yoyote itakayobakizwa.

NI hekima kusema, ngoja tuone. Kwa maana Sisi tumejikuta katikati. Hatukuwepo mwanzoni na bila Shaka mwishi hatutakuwepo.
Hivyo hatujui yaliyotukia na hatutajua yajayo
nimeielewa post yako,kuna imani unaiamini kabisa kabisa ila unauacha mjadala uendelee
 
Can you tell us more about ''Nibiru -Earth" relation?
Ni maelezo maerefu sana maana inabidi nianze kuelezea kuhusu Races na mihula yake..

Na najua umeamwahi kusikia kuhusu Planet X au Earth X ni kama Warmhole au Kama au black hole wengi wana irelate na Nibiru na Ndiyo hasa itaimeza Dunia Through the Induced Singularity..
Ni mengi sana ya kuongea kuhusu Hii kitu sema Muda wangu ndo hautoshi maana naingia kwa Machale
 
Binafsi naona umezunguka sana. Nilitaka kwanza uweke kitabu ambacho kwa maoni yako kingetakiwa kutoka halafu ndo ungenipa hili darasa. Kama ingekuwa ni sehemu inayohitajika jibu la swali sidhani kama hayo maelezo yangejitosheleza.
Nimezunguka kwa sababu ya kujua kama unazo basic Knowledge ya Discusion ambayo tunataka kuingia....

Kwanini nimefanya hivyo??
Wengi sana hapa Jf nimekuwa Nikijenga nao hoja nilikuja kugundua mwishoni kuwa Wengi wao hawana hata ile Basic knowledge ya kitu wanachokijadili zaidi ya Knowledge ya juu...

sasa Niliamua kuwa ili niweze kuIngia kwenye Mjadala wa kisomi lazma nijue na nihakikishe mjadili mwenza anayo angalau elimu ya Msingi ya Kitu kinachojadiliwa..
 
Connection ni kupokea Yesu Kristo kuwa BWANA na Mwokozi wa MAISHA YAko.

Utampokea Roho wa Yesu Kristo ambaye ndiye Roho mtakatifu, hapo habari ya kumtafuta Mungu itaishia Hapo maana Mungu ataingia na kukaa ndani Yako.

Unakwama wapi ndugu?
 
Asante kwa maelezo yako, vipi kitabu cha Jasher Play store kipo?
 
Mwafrica mjinga sana, kusoma hadithi za vizazi na vizazi kama tu vina link na biblia au dini inakua sawa. Lakini ukimleta kwenye mazungumzo babu yako wa pili au wa tatu... ghafla inageuka kua ni mizimu. Nidokeze tu; Kuna nguvu kubwa sana kwenye muunganiko wa vizazi. Hao jamaa wanajua ndio mana wakamleta jesus kwenye nafasi ya ndugu zako(Mizimu). Yote ni kukata link ya nguvu. Jina Yesu halina madhara sababu ni mchanga wa macho. Jiulize kwa nini watu wanvyolitumia hilo jina wachungaji hata komedi. Jesus is LORD!! msemo maarufu kabisa!! Angalau MUNGU linaheshimika!

Binafsi tukiongea kidini hasa katika ukristu; Adam alikua na mke wa kwanza, then Eva alikuja baadaye baada ya mambo kwenda ndivyo sivyo na mwanamke wa mwazo wa Adam.

Tukiongea kiafrica; Mungu ni mimi, wewe na yule na yule na wale. Sisi na vyote vinavyotuzunguka ndivyo vinamkamilisha mungu Mungu. Inaleta maana kabisa jiulize fact hii: Mchawi hawezi kukuloga kama hajui chimbuko la ukoo wako(Walau majina) au kumpa access ya kitu chako mfano nguo, kioo, kivuli etc. Tumekosa nguvu hasa waafrica sababu badala ya kubeba jina la ukoo unabatizwa jina la kupewa na Paroko. Enegy/Divine broken.
 
Mkuu share nasi basi baadhi ya vitabu vinavyoelezea the mentioned issue
Vingi Sio documented mkuu,
Na vilivyo andikwa vimeandika taarifa chache kuwahusu hasa hasa mwandishi kama
Zacharia Sitchin alianza kutafsiri book of ENKI angalau yeye ndio msingi kwa wale wachache wanaoanza kufuatilia
Ila vitu deep vipo mikononi mwa Wachache sana ambao hawapo verified na ni watu wa kawaida hasa Wazee fulani wa hapa Africa,Wahindu wekundu na Jamii fulani za huko Peru inca,wale maguru wa huko India wanaokaa karibu na Matemple ya kale ya Miungu wao,makabila machache kama Dogon ya kule Mali na Jamii za siri yaani kiufupi hakuna Maandiko yaliyonyooka ila wachunguzi hua wanaenda huku na huku kufanya mahojiano na locals na kuunganisha dot na matukio ili kupata uhusiano na kugundua mambo yanaingiliana,
Kule You tube ukiingia kuna documentaries kibao kuhusu haya maswala ni wewe tu kujifunza tena nyingine ni chunguzi za kisayansi kabisa
Utaona maajabu ya kufa mtu!
 
Ten commandments haikuanza kwa Moses pale Sinai,
Kabla yake kulikuepo na Hamurabi code hizi ni Amri tata kutoka kwa Mfalme Hamurabi alizozipokea kutoka kwa mungu Shamash na ni kongwe kabla ya Musa na ni zile zile za Musa sasa akili kichwani!
😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…