Kitabu cha Enoch kinawataja malaika 200 walioasi ambao ndio waliiba Siri na teknolojia za mbinguni kisha wakamfundisha Binadamu

Kitabu cha Enoch kinawataja malaika 200 walioasi ambao ndio waliiba Siri na teknolojia za mbinguni kisha wakamfundisha Binadamu

Book of Enoch ni sehemu ndogo tu ya Saga,
Hayo mambo yote Yamo katika Sumerian tablet
Kwa ujumla wake tunaiita
THE CHRONICLES OF ANNUNAK

Hapa utapata kwanini Dunia ina race kibao na ndipo utajua saga la kina Semyaza (Enlil) na Sayansi za juu za ku clone viumbe wa Dunia,Ujenzi wa Mapyramids kama Wireless Power plant na kuweka magnetic field za hali ya juu,
Masuala ya time travel yaani Haya majamaa yalikua hayatumii magari wala Ndege yalikua yana disappear na kutokea sehemu yanayotaka na ndio Maana hapa Duniani kuna maeneo yana mageti yanayodhaniwa yalikua ni spaceport kama huko Baalbek, Puma punku,China,India,Sri Lanka ,Peru inca mpaka Aztec na Mayan kote kuna sites zinazofanana
Kiufupi tukiwaletea Haya maswala hua mnaona chai na story za kahawa ila kwa mtafiti ukianza fuatilia sites za wanaodaiwa ni Miungu utabaki kushangaa tech yaliyotumia Haya majamaa
Imagine mawe yanachongwa na raser tool hiyo tech hatuna ila majamaa yalifanya!
Mkuu binafsi nimefuatilia sana, na nimegundua kuwa Biblia kwa sehemu kubwa imetokana na Summerian tablets, kiufupi ni kwamba Mungu anayeongelewa kwenye Biblia ni Anu, Enki na Enlil.
 
Wahusika ni wale wale mkuu
Mfano god of science and technology wa Kemet aliitwa Thot huyo huyo kwa Wahindi ni Krishna na kwa Aztec na Mayan ni Quetzalcoatl
Na ukiangalia sites zao zinafanana na sifa za hao Miungu ni the same na wagiriki,Roman na Jamii nyingi hapo lazima ujiulize who are they?
Na ndio Enki(Summerian Mythology).
 
Alafu hizi Stori za kale ukisoma utagundua Dini NI uongo
Mpaka sasa mimi naamini hivyo.
Zimejiundia visheria sheria ili kuepuka kua criticised, viongozi wake hawagusiki, imani yao haitetereshwi na haikosolewi ukaachwa bila kushutumiwa na wafuasi.

Hizi dini zina contradiction nyingi sana. Huko tuendako ukweli utadhihirika.
 
Mkuu binafsi nimefuatilia sana, na nimegundua kuwa Biblia kwa sehemu kubwa imetokana na Summerian tablets, kiufupi ni kwamba Mungu anayeongelea kwenye Biblia ni Anu, Enki na Enlil.
Yeah ndio hao hao hakuna wengine,
Watu hawaelewi hili Ila kama ukisoma Summerian tablet vizuri ukaja kusoma kitabu cha Mwanzo kwa jicho la tatu utagundua ndio wale wale,
Mfano ni kile kitendo cha Mungu kumtembelea Abraham pale mialoni mwa Mamre akiwa katika umbo la binadamu utagundua kabisa kitu hakipo sawa!
 
KITABU CHA ENOCH KINAWATAJA MALAIKA 200 WALIOASI AMBAO NDÎO WALIIBA WALIIBA SIRI NA TEKNOLOJIA ZA MBINGUNI KISHA WAKAMFUNDISHA BINADAMU

Anaandika Robert Heriel
Mtibeli

Kwa Wakristo na waumini wa Dini ya kiyahudi jina Enock siô geni Kwao. NI Moja ya binadamu ambao hawakuwahi kupatwa na umauti.

Kwa wale wasiomjua Enoch. Kw kifupi Enoch ni Moja ya Watu WA mwanzoni katika simulizi za Zamani za kiebrania ambao NI uzao wa Nuhu.

Enoch alizaliwa na Yaredi. Enock ni Babu yake Nuhu(Nuhu NI kitukuu cha Enock)

Kwa Mujibu wa simulizi za kiebrania, enock ndiye Mtu pekee aliyeweza kukutana na MALAIKA tofauti tofauti yàani zaidi ya mmoja. Binadamu Wengine waliowahi kukutana na MALAIKA walikutana aidha na Gabriel au Mikael au Rafael

Enock ndiye Mhusika pekee aliyeweza kuwataja MALAIKA wengi zaidi Kwa majina na Sifa zào za kimaumbile.

Enoch ndiye Mhusika pekee kwèñye Biblia aliyeweza kuelezea Mianga kama Jua na Mwezi na mizunguko yake.
Enock alikuwa MTU wa kusafirishwa na MALAIKA kutoka anga Moja kuelekea ñyiñgine. Ilikuwa kawaidà Kwa Enock kupotea hata miaka 50 bila kujulikana alipo.

Enock ndiye Mhusika pekee aliyeelezea Kwa majina MALAIKA 200 Walioasi na kuzaliana na WANADAMU.

Kwa jinsi nilivyoielewa simulizi ya Enock ni Kwamba, binadamu ni kama mnyama, tofauti yake ni utashi tuu.
Binadamu Hana uwezo wowote WA kubuni kitu hata Moto, sîjui, urembo, sîjui ndege, sîjui computer, sijui bastola, miongoni mwa TEKNOLOJIA zingine.

Stori ya KITABU cha ENOCH Kwa kifupi Ipo hivi;

1. Kûna mbingu 12 na kîla mbingu kuna MALAIKA wake Mkûu anayoiongoza.

2. Malaika 200 waliasi wakiongozwa na Kiongozi wao aitwaye Samzaiya. Viongozi Wengine ni Azazel

3. Katika hao MALAIKA kîla MALAIKA alikuwa na sîfa, uwezo na Ñguvu zake. Wàpo waliokuwa na mbawa Mbili, wàpo mbawa nne(serafi) wàpo WA mbawa sita (Makerubi) na yupo Malaika mmoja aitwaye Samael mwenye mbawa Kumi na Mbili(huyu role yake ipo kitofauti)

4. Malaika hawa walikuja kuzaa na Wanawake wa WANADAMU. Wakazaa majitu, nephili au miunguwatu (demigods)

5. Azazel Moja ya Malaika alioasi aliwafundisha Wanadamu Teknolojia za silaha, uchawi, unajimu, urembo kama kupaka makeup. Kitabu kinaeleza kuwa MALAIKA walioasi wakawafundisha mambo meñgi sana àmbayo Kwa Sasa ndîo tunaita Teknolojia na utandawazi.

Jambo lililonishangaza NI kuona mpaka masuala ya Teknolojia ya kutumia Dawa Fulani ili Wanawake wasibebe mimba ili kutoharibu urembo wao. Hii ilifanya Baadhi ya Wanawake waliotumia Teknolojia ya Kuzuia mimba baadaye kushindwa kupata Watoto. Enock anaeleza hayo.

6. Demigods yàani wale machotara wa Malaika na binadamu ambao Kwa uelewa wàngu ndîo nahisi wanaitwa Majini. Wakawa wanakula kupita kiasi Jambo ambalo mama zào(Wanawake wa kibinadamu) walishindwa kuwalisha, wale Demigods wakaanza Kunywa damu za watu, kisha nyama zào, kisha wakawa wanakula ndege, wanyama na samaki wa baharini. Kipindi hicho nafikiri wanyama kama Godzilla waliishia kuliwa na hawa demigods.

Urefu wao(hao Demigods) ulikuwa Mita thelasini kwenda juu na walikuwa na uwezo mchangayiko yàani uwezo WA kibinadamu na kimalaika.

7. Wanadamu wakawa wanalia kutokana na kuuawa na hawa Watoto chotara(demigods au wanefili).
Kilio Chao kilitokana na dhulma ya uhai, kuchukuliwa Wake zào, kuteswa n.k.

8. Kilio Kikafika Mbingu ya Tano Huko alikuwepo MALAIKA Mikael, Gabriel, Rafael na Uriel. Malaika hao nao cheo chao NI kikuu. Wakaweka kikao huku wakilalamika wao Kwa wao Kwa matendo yanayofanywa na kina Samzaiya na Azazel na wenzao.

Mikael akiwa Kiongozi wa Malaika AMBAO hawakuasi akamuita Baba yao(Mungu). Mungu akawauliza kûna nini mbona kuniita. Wanasema(akina Mikael), tazama Samzaiya na Azazel wanachokifanya Huko Duniani. Wameiba Siri za MBINGUNI Ambazo Mwanadamu hakupaswa kuzijua lakini waô wamewapa. Wamewafunisha siri zetu, Kisha wakazaa nao Watoto. Ndio maana unasikia kilio Huko Duniani. Umwagaji WA damu umekuwa Mkubwa.

9. Mungu akatoa Amri akina Samzaiya na wenzake wakamatwe Kisha wafungwe katika maeneo mbalimbali mpaka Siku ya hukumu.

10. Kuhusu Demigods Mungu akawaambia atafutilia mbali Watoto na kizazi cha demigods na Wanadamu walioasi (walioungana na demigods) Kwa kutumia Gharika.

11. Basi kulikuwa na vita Kali Baina ya Malaika walioasi na MALAIKA waaminifu. Upande WA waliasi ukiongozwa na Samzaiya na Azazel huku upande WA MALAIKA waaminifu ukiongozwa na Mikael, Gabriel, Rafael na Uriel.
Mungu akamteua Malaika WA Mbingu ya Tano Aitwaye Samael kuhakikisha Haki inatendeka katika vita hiyo. Samael maana yake sumu y Mûngu, Malaika wa Kifo àmbayo majukumu yake yalikuwa mosi, kuhakikisha Haki inatendeka, pili, kushawishi na kujaribu viumbe Wengine Mpaka Malaika wènyewe,

12. Samael ndiye aliyeuweka MTU WA ujuzi WA Wema na ubaya pale Bustani ya Edeni na kumtumia nyoka kumdanganya Eva.

13. Samael ndiye aliyemtuma Ammado yàani Malaika wa ukahaba kumlaghai Adamu Kisha adamu akalala na Ammado na kuzaa naye Mtoto

14. Samael alikuja kuanguka baàda ya kumchukua Lilith kuwa Mkewe na kwenda naye kwèñye Mbingu ya Tano

15. Samael ndiye aliyepigana na Yakobo usiku ule ambao Yakobo alikuwa anaenda Kwa Labani Mjomba wake.
Samael ndiye prosecutor na ndiye aliyemletea majanga Ayoub katika kupima Haki na ukamilifu wa Ayoub

16. Ingawaje Watu wengi wanamhusisha Lucifer kuwa ndiye aliyemdanganya Eva lakini Samael ndiye aliyefanya Jambo hilo.

17. Nuhu hakuwa Mtoto WA kawaida. Jambo lililopelekea babaake Aitwaye Lameki kutaka kumkana Kwa kuona amebambikiwa, Methuselah babaye Lameki akapeleka habari hizô Kwa Enoch(Babu yake Lameki)
Nuhu tofauti na Watoto Wengine wanapozaliwa kwa Wakati huo. Alikuwa amezaliwa akiwa mweupe kupitiliza mwenye nywele kama za dhahabu. Kwa Sasa ungemuita albino. Lakini kama hiyo haitoshi, macho yake yalikuwa yakiwaka kama taa na kujuza mwanga chumbani
Jambo hilo lilimfanya Baba yake, Lameki kuona huenda Mkewe alilala na demigod au Moja ya wale Malaika walioasi.

18. Enoch ndiye aliyemwambia Methuselah Mwanaye kuwa asihofu kuhusu Mtoto wa Lameck kwani NI wake, na ndiye atakuwa mkombozi wa Wanadamu na amepewa jukumu la kujenga Safina àmbayo Watu nane tuu ndîo watakaookoka Wakati huo ûkifika. Enoch akamuita kitukuu chake hicho jina Nuhu.

19. Samael ndiye aliyemlaghai Eva na kuzaliwa Kaini.

20. Gharika ikaja kufuta na kuangamiza Watu wôte waovu na wale Demigods ingawaje wàpo ambao waliescape

21. Nuhu alipata nafasi ya kuingia na nguo ya Adamu Ile aliyovikwa na Mungu kipindi kile walichoasi.
Baàda ya gharika Hamu Mwanaye Nuhu aliiba Ile Nguo àmbayo ilikuwa na maajabu. Kisha Nimrodi Mjukuu wa Hamu naye akaiiba. Yeye akaweza kûitumia katika shughuli zake za Kúpiga upinde. Baadaye akawa Mfalme.

22. Ibrahim alizaliwa Nuhu bado akiwa hai. Nuhu alikufa Ibrahim akiwa na Miaka 55
Hivyo hadithi zote za tangu Adamu Ibrahim alizipata Kwa Babu yake, Nuhu.

Kwa Leo tuishie Hapa.

Ijumaa Kareem

Robert Heriel
Taikon WA Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam
Duuh! Enoch ana balaa..
 
Kinachonisumbua mpaka sasa ni Yesu anaingiaje hapa?
Yaani Yesu ana uhusiano gani na Annunaki?
Hahaha Wana uhusiano mkubwa tu maana Annunak Nephilim walikua divine being na Yesu ndio master wa Spiritual Realm,
Moja ya sifa kubwa ya Annunak ni kua wao ni super race waliowahi exist wakiwa ni Immortal na ndio viumbe wa kwanza kumfungua Binadamu kuhusu maswala ya kiroho ila baadae watu kwa kutokuelewa wakaanza kuwaabudu kama gods!

Ila uhalisia sisi wao na viumbe wengine ni demi gods katika Ulimwengu wa Roho tena Binadamu anaweza kuadvance mpaka anaenda mbali zaidi hivyo walihakikisha wanaficha hio elimu ila Teacher Master Yashua Amashiach Mnazarene akaja toa siri hiyo!
Haya mambo deep yana balaa lake!
 
Kama hawakuandika unàtaka Watoto waô wajulie Wapi?

Waafrika NI wakati wetu kuandika historia za Maisha yetu ili Miaka 1000 ijayo kizazi chetu kisije uliza na kuongea Jambo la aibu na fedheha kama ulilolileta Hapa

Wewe hata ukifa Sasa hivi sina hakika kama umeandika popote hata Robo ya mambo muhimu ya uliyoyapitia katika Maisha yako
😂
 
1720798125758.png
 
Kitabu cha Henoko kina uongo hatari usipoteze muda mfano Biblia inasema Malaika walioasi mbinguni walikuwa wengi mno theluthi ya malaika wote Biblia inatamka wazi kuwa idadi ya malaika huwezi hata kuwahesabu ni innumerable sasa one third ya malaika wasiohesabika haiwezi kuwa 200

Pili kitabu cha henoko kinasema katika hao malaika 200 wawili walirudi tena kibabe mbinguni kwenda kuiba siri kuwa walibadili majina wakapita getini huko mbinguni wakaenda kuiba siri wakaja nazo duniani

Lingine Yesu mwenyewe alisema malaika hawaoi ,hawaolewi wala kuzaliana na kiumbe chochote kitabu cha Henoko kinasema malaika wana uwezo wa kumwingilia mwanamke akabeba mimba na akazaa mtoto binadamu wa kawaida kabisa unayekutana naye barabarani. Huyo binadamu uzao wa malaika na binadamu anaitwa mnefili

Yesu ni mkuu kuliko huyo Henoko alichosema Yesu ndio sahihi .Henoko matapeli walitumia jina lake tu


Hicho kitabu cha Henoko ni hadithi za vijiweni za wahuni hakitambuliwi kwenye Biblia ya wayahudi ni hadithi za vijiwe vya kahawa

Hivyo biblia ni uongo
 
Hiki ni kitabu cha kizushi na ushahidi wote wa kihistoria na kiteolojia unaonesha kuwa Enoch au Henoko hakuwahi kuandika kitabu. Ushahidi wa kimazingira pia unaonesha kitabu hicho kilitungwa miaka mingi baadaye baada Henoko kutwaliwa mbinguni. Hicho ni kitabu cha kipepo tuu chenye lengo la kupotosha imani na historia ya ukombozi wa mwanadamu. Ni sawa tuu na wanaongalia fiction movie.

Nani aliandika kitabu cha mwanzo
 
Usichojua ni kwamba Enock alikutana na ''Mungu mwenyewe"
Enock ni descendant wa Uzao wa EL inasemekana ni mtoto wa Enki anayetokana na uzao wa EL, wakati Elohim walipokubaliana mwanadamu aangamie na Gharika, Enki alimtuma mmoja wa watoto wake aende akamlinde Nuhu, baadaye Enki aliagiza kuwa Nuhu ajenge Safina.
SOURCE: 1.The lost book of Enki
2.The Epic of Gilgamesh

Henoko ni malaika metatron ni mkubwa sana kwenye rank za angels
 
Back
Top Bottom