James Comey
JF-Expert Member
- May 14, 2017
- 8,759
- 14,831
Daktari daktari daktari...nilitamani kuwa utakuja na kitu kilichokuwa na nguvu sana katika kusapoti hoja zako. Lakini kwa hii hapana na lengo langu lilikuwa kujifunza. Ameshasemanhapo mambo yaliotimizwa katikati yetu. Yeye hakuwa among the disciples ila wapo wanafunzi na mitume wameandika ija yeye akaandika kama mtafiti yaani aliyepata commission ya kuandika ripoti ya kupeleka kwa Theofilo kiongozi wa kiserikali.Even a Fabricated Story can Form Coherence Mkuu...
NA ndo maana kuna kipimo maalumu cha Kupima Story kabla ya kuiamini..
Kipindi Nilipokuwa nasoma Bible Textual Analysis sanaa sana kwenye OT [Old testaments] (Textual Critiq)
Kuna maandishi mengi yana Ideas Sawa na yana maana Sawa na Ni hadithi za zamani zimeandikwa na watu tofauti ila zinakosa ubora wa Kuwa Za ukweli na Walishindwa kuyaweka kwenye Biblia Kwa sababu kwanza ni uongo pili vinakosa Analytical Truth..
ntakuandikia kimoja kama sio viwili tu..
Uthibitishwaji wa Nyakati (Nyakati inapimwa kwa Vitu Vingi kama Lugha iliyotumika Muda huo, Aina ya Uandishi, Miji ya Mda huo Na hata majina ya Miji)..
Kwa mfano..
Baba Yako alikuandikia Barua ya maelezo kabla ya yeye Kufariki mwaka 2001 akakuambia..
"Mwanangu Nimekuachia Mali nyingi sana ila mali hizo niliamua Kuzigawa katika sehemu mbali mbali Zingine zipo Mkoa wa Manyara na zingine zipo Mkoa wa Geita Mwanangu tumia Hizo mali vizuri, Kwani ni mali pekee Zenye utajiri wa Nafsi kuliko Utawala wote wa Rais Obama"
ukiisoma Kwa haraka haraka Habari hii kwa mwaka 2012 mpaka mwaka 2024 Unaweza ukaona Ni sawa na haina Shida ila kama ukituma critical Thinking and analysis utaona shida nyingi sna..
Kwanza mwaka 2001 hakukuwa na Mkoa unaitwa Manyara wala Mkoa wa Geita na wala Mwaka 2001 hakukuwa na rais anaiyeitwa Obama..
So obvious its fabticated story iliyotungwa Kwenye miaka Ya 2010 mpaka mwaka 2018 hivi..
Kwahyo ulifanya Textual analysis ya Maandiko ndani ya Biblia Yanafail kuendana na authentification na Autharitative Regulation..
Umesema Luka Ilikuwa na Uvuvio wa Roho mtakatifu, samahani kwa kusema hivi "I doubt that"..
Luka(Alikuwa ni Daktari wa Binadamu) mwenyewe anasema Ukisoma Luka 1:1-4..
Kuwa ametafuta Kwa kufanya Research na kuuliza wazee walioishi miaka hiyo na baada ya kuwauliza akaandika.. kwahyo unamaanisha Research pia Zina uvuvio??
na Elewa neno alilotumia Luka Kutunga
Kutunga Ni kubuni Jambo ambalo hapo kabla halikuwepo.. (Kama BAKITA wanavyitafsiri)
View attachment 3042830
Nilidhani utakuja na flaws za maana ktk vitabu vya biblia ili nifatilie lakini hii hapana.
Nakumbuka kuna kipindi Kiranga aliwahi kutoa biblical contradictions na zikajadiliwa lakini hii yako hapana.
Pia, tukumbuke Kiswahili kilichotumika kutafsiri ni kile cha zamani kidogo hivyo kuna maneno mengine yanakosa kuleta picha halisi ya maneno hayo kutoka maandishi ya zamani yaliyotumika ktk uandishi wa biblia.
Mathalani, watu wa bukoba wanajua aina nyingi za ndizi. Lakini mzungu zote anaziita banana. Lugha ni utamaduni. Wakati mwingine tunaweza kukosa neno kwakuwa halikuwepo ktk utamaduni.
Kwahapo kwa Luka neno kutunga liangalie ktk tafsiri ya kingereza litakupa maana zaidi ya nini kilimaanishwa. Asante.