Kitabu katika kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar sehemu ya kwanza. Pitio la kitabu: Mimi, Umma Party na Mapinduzi ya Zanzibar


Hao akina Twaha na Jaha Ubwa hata hajawahi kuwasikia kwenye historia na hawajui walikuwa na role gani kwenye Mapinduzi ya Zanzibar
 
Nisaidie kupata hiki " kwaheri ukoloni,kwaheri uhuru,^ kinauzwa wapi nikanunua
Inshallah
 
Nisaidie kupata hiki " kwaheri ukoloni,kwaheri uhuru,^ kinauzwa wapi nikanunua
Inshallah
Kinoa...
Kuna nakala ya bure soft copy mtandaoni na hard copy knapatika maduka yote ya Ibn Hazm Msikiti wa Mtoro, Manyema na Mtambani.
 
..Tatizo wanaonekana wamepatana sasa hivi lakini ikifika wakati wa uchaguzi wanarudi kwenye uhasama.

..Zanzibar inahitaji Tume ya Maridhiano na Ukweli, vinginevyo CCM wataendelea kurithishana mzigo wa kuficha ukatili uliofanywa na wanamapinduzi.

Lakini generation ya wana mapinduzi inazidi kupotea. na vizazi vya waliofuata kwenye madaraka pia. Lazima waridhiane. lazima wapeleke maendeleo Pemba ili visiwa vyote viwe na neema sawa.
Umaskini ndio unaleta shida. Mtu akila na kushiba, maneno mengi ya ajabu ajabu huwa yanapungua
 

Nani ni adui wa Zanzibar sasa kama wenyewe kwa wenyewe ndio walianza hayo? Watanganyika wanasingiziwa tu
 
Nani ni adui wa Zanzibar sasa kama wenyewe kwa wenyewe ndio walianza hayo? Watanganyika wanasingiziwa tu
Tangawizi,
Kulikuwa na kambi Tanganyika kijiji cha Kipumbwi iliyotumika kwa mafunzo ya wale Wamakonde wakata mkonge wa shamba la Sakura waliovushwa kuingia Zanzibar kusaidia mapinduzi.

Kushiriki kwa Tanganyika si kwa kusingiziwa.
 

..tatizo ni kwamba kizazi kipya nacho kinafanya unyama ili kuficha unyama wa wanamapinduzi.

..kila uchaguzi mkuu kuna unyama unafanyika na lengo ni kuzuia yeyote wale wanaopinga unyama wa wanamapinduzi kuingia madarakani.

..sidhani kama kuna Mtz alitegemea utawala wa Dr.Shein utavuruga uchaguzi, au utamwaga damu, lakini hayo yote yalitokea.
 
Kwa kuwa kitabu hicho hakipatikani., basi makala haya tunaweza kuyaunganisha na kupata historia inayosemwa
 
Nawasalimu katika jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kuwatumia salaam zangu za kuadhimisha kumbukumbu ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, tutayalinda kwa gharama yoyote.

Nawatakia maadhimisho mema ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Kazi Iendelee!.

Paskali
 
Umeishapata jibu juu ya Utukufu wa mapinduzi haya Matukufu? Kama bado basi this is the right place,Mohamed Said yupo kukusaidia Pascal Mayalla
 
Unasemaje wakidokeza ilikuwa uvamizi na uasi wa watu kuoka bara? Si ya wenyeji?
 
huo ni urongo!
P
Unajuaje? Wewe kijana sivyo? Ulikuwepo?

Karume hakuandaa mapinduzi; Petterson (balozi wa Marekani wakati ule) anaandika katika kitabu chake Karume mwenyewe aliwahi kusikia kwa mbali tu akamwambia afisa Mwingereza kabla ya 12 Januari 1963 kutakuwa na vurugu akaona vema kuondoka kwenda bara. Aliyeendesha uasi alikuwa Okello aliyeongoza pia mauaji ya hovyo
("He recruited volunteers for a revolutionary force. Of the 330 men he said he had enlisted in the cause, most were mainlanders. .......... He told his men that when the fighting began, they were to kill all Arabs between the ages of eighteen and fifty-five. Young, old, and pregnant women were to be spared. Europeans, he ordered, were not to be attacked. Virgins and women whose husbands had been killed or detained should not be raped (all others, presumably, were fair game)" - Don Petterson, Revolution in Zanzibar, uk. 27)

Hii ni kweli "mapinduzi tukufu"?
 
Hilo ni jina la Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
P
 
Mzee Mallya, umekimbia na kuepukana na jibu. Unaleta jibu lako kwa Mohamed Said. Sina kazi na dhana za utukufu katika Uislamu. Si shauri yangu.
Nilikuletea taarifa ya mtu aiyeshuhudia mapinduzi (Petterson) anayemnukuu Okello aliyesema mwenyewe kundi lake lilikuwa hasa na watu kutoka bara - na wewe ulisema "uwongo" nilipouliza eti si wenyeji, ni watu wa bara waliendesha mapinduzi haya?

Halafu nilitaja maagizo ya kuchinja wanaume waliotazamiwa kuwa "Waarabu" lakini kutochinja wale wadogo na wazee juu ya miaka 55. Na kutobaka makundi fulani kati ya wanawake yao.
Nikauliza kuhusu utukufu wa maagizo hayo.
Hapa umekimbia kwa Mohammed Said, lakini mimi si huyu.
 
Ninachokisema mimi, ni jina la Mapinduzi ya Zanzibar yanaitwa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na jina hilo sikulitunga mimi, hivyo kuniuliza mimi kuhusu Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yana utukufu gani, ni kunionea bure!. Hili swali waulizwe wanao yaita Mapinduzi Matukufu na sio akina sisi tuliokuta yanaitwa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, badala ya kuwauliza waliyoyaita, mnatuuliza sisi!. Huku ni kutuonea bure!.
P
P
 
Asante. Ila nisipokosei, ni watu fulani tu wanaotumia lugha "mapinduzi matukufu". Kwa hiyo ni azimio kuchagua lugha yao?

Basi lakini hatujaanza na utukufu. Niliuliza kuhusu hoja kwamba haikuwa mapinduzi ya watu wa Zanzibar, lakini zaidi maasi ya watu kutoka bara. Hapa ulijibu "huo ni urongo!"
Nimeleta ushahidi wa balozi aliyekuwepo kiswani wakati ule na jinsi anayvomnukuu Okello.
Petterson anaandika: "He recruited volunteers for a revolutionary force. Of the 330 men he said he had enlisted in the cause, most were mainlanders. .......... He told his men that when the fighting began, they were to kill all Arabs between the ages of eighteen and fifty-five. Young, old, and pregnant women were to be spared. Europeans, he ordered, were not to be attacked. Virgins and women whose husbands had been killed or detained should not be raped (all others, presumably, were fair game)" - Don Petterson, Revolution in Zanzibar, uk. 27)

Kwa nini ulisema "uwongo!" ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…