Kitabu katika kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar sehemu ya kwanza. Pitio la kitabu: Mimi, Umma Party na Mapinduzi ya Zanzibar

Kitabu katika kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar sehemu ya kwanza. Pitio la kitabu: Mimi, Umma Party na Mapinduzi ya Zanzibar

JK,
Nguruvi anataabishwa na safari zangu na "kaimati."

Haya ndiyo anayoyajua kuhusu mimi kuwa ni mtu wa kula maraha ndani ya madege na ma 5 Star Hotel.

Ule ujuzi wangu katika historia ya Tanzania na niliyoandika hayataki.

Mimi nakua baba yangu mwana TANU na rafiki zake wakubwa wawili Abdulaziz Twala na Jaha Ubwa ni wana ASP kindakindaki.

Huu ndiyo ulikuwa msimamo wa wazee wetu wote wakitaka ASP itawale Zanzibar na waliyaunga mkono mapinduzi.

Lakini...

Walipokuja kujua ukweli na walipodhihirikiwa na unyama uliopitika katika mapinduzi na jela za mateso na mauaji zilipoanzishwa waliyachukia mapinduzi na wakayapa mgongo.

Baba yangu hakuacha kuugulia kifo cha Twala na Jaha Ubwa akiwakumbuka mara nyingi tu.

Haya ndiyo maisha yangu nimeishi ndani ya historia hizi.

Ama kuhusu Uislam naam sisi ni Waislam na hawa Wazanzibari ni Waislam na Twala, Karume na Jaha Ubwa ni Waislam.

Kwangu ni shida kuishi nje ya ukweli huu.

Ndiyo maana leo unaona CCM Zanzibar haiwezi kushinda uchaguzi huru na wa haki visiwani lazima msaada wa ushindi utoke Tanganyika.

Hii ndiyo historia ya mapinduzi na ukijua historia hii itakufungulia kuyaelewa yote yaliyopo Zanzibar hii leo.

Hao akina Twaha na Jaha Ubwa hata hajawahi kuwasikia kwenye historia na hawajui walikuwa na role gani kwenye Mapinduzi ya Zanzibar
 
KITABU KATIKA KUMBUKUMBU YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR SEHEMU YA KWANZA
PITIO LA KITABU MIMI, UMMA PARTY NA MAPINDUZI YA ZANZIBAR MWANDISHI: HASHIL SEIF HASHIL

Kuandika historia ya ukombozi katika nchi za Kiafrika kunahitaji ujasiri mkubwa sana na sababu yake ni kuwa Afrika ina historia rasmi.

Historia hii rasmi ni ile ambayo imepitishwa na kukubalika na watawala.

Historia hii ikishaandikwa ndiyo mwisho kwani haitoi nafasi ya kuwapo kwa historia nyingine itakayokwenda kinyume na hiyo.

Hii ni moja ya sifa ya siasa katika Afrika.

Historia rasmi ndiyo hiyo itakayokuwa katika mitaala kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu.

Hatari yake ni kuwa inasababisha na pengine kwa miaka mingi sana kusomeshwa historia yenye upungufu hadi pale atakapotokea mtu jasiri akaandika ukweli.

Wako watu bado wa hai na pengine wapo hapa ukumbini wanaijua historia ya mapinduzi ya Zanzibar kwa kuyaona mapinduzi yenyewe na kwa kushiriki lakini hawajanyanyua kalamu kuandika wala kufungua mdomo kuihadithia na watakwenda kaburini na watazikwa na historia zao ambazo laiti wangeliziandika nchi ingenufaika pakubwa.

Hashil Seif Hashil anastahili pongezi kwa ujasiri huu wa kutuandikia kitabu na kutueleza historia ya Zanzibar ambayo si wengi wanaijua khasa vijana waliozaliwa baada ya mapinduzi mwaka wa 1964 ambao kwa sasa ni watu wazima.

Kuiandika historia ya mapinduzi ya Zanzibar ni kazi inayohitaji, ushujaa kwani si rahisi kuieleza na ukakosa kuwaudhi baadhi ya watu na wengine watu wako wa karibu sana.

Afrika tuna utamaduni wa kuzifanya historia zetu kuwa kitu nyeti kwa hiyo iogopwe na isiguswe kwa kuigeuzageuza kutaka kujua undani wake. Hashil Seif ni mwandishi jasiri na mtu huwezi kustaajabu kwa huu ujasiri wake utakapoijua historia yake binafsi.

Hashir Seif mwaka wa 1962 akiwa kijna mdogo kabisa wa umri wa miaka 26 alitoroka Zanzibar pamoja na wenzake wapatao 20 kwenda Cuba kupata mafunzo ya vita kwa nia ya kurejea Zanzibar na kupindua serikali na kuweka utawala wa Ki-Marxist.

Hili la kwanza na kaeleza katika kumbukumbu hizi.

Pili, Hashir Seif hajasita hata mara moja katika kitabu hiki kueleza kuwa yeye alikuwa mwanachama wa ZNP, maarufu kwa jina la ‘’Hizbu.’’

Katika historia ya Zanzibar baada ya mapinduzi neno, ‘’Hizbu,’’ lilikuwa linatisha na kuna watu na si wadogo hadi leo bado wana hofu kubwa ya kunasibishwa na historia yao katika Hizbu.

Katika kumbukumbu hizi Hashil Seif anaeleza historia yake ndani ya chama hiki na mchango wake kama kijana katika Youth Own Union (YOU) bila hofu wala wasiwasi wowote na hadi leo katika umri mkubwa wa miaka 80 bado ni komredi na hajabadili fikra zake za siasa za mrengo wa kushoto.

Katika kitabu hiki Hashil Seif anaeleza fikra zake kama bado yuko katika Zanzibar ya miaka ya 1960 bila ya kuongeza wala kupunguza nukta.

Hii ni moja ya mambo yanayokifanya kitabu hiki kiwe kiongozi katika kuijua historia ya mapinduzi na wanasiasa wake wa nyakati zile.

Ili kitabu kiwe kitabu ni lazima kiwe kina elimu mpya ambayo kabla haikuwa inajulikana.

Wazanzibari wengi, ukimtoa Dr. Harith Ghassany: ‘’Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru,’’ (2010), walioandika historia ya mapinduzi wote wamepita mle mle katika historia rasmi.

Msomaji hapati jipya isipokuwa tofauti ya jalada, jina la kitabu na la mwandishi.

Unapoanza kumsoma Hashil Seif mwanzoni tu unakuwa mfano wa mtu aliyekuwa kalala usingizi fofofo na ghafla anatokea mtu akammwagia maji baridi usoni na kwa maji yale akashtuka kutoka usingizini na pengine kwenye ndoto akawa karejea katika dunia ya kweli.
Hashil Seif anakifungua kitabu kwa majina ambayo hutayakuta katika historia tuliyoizoea ya mapinduzi ya Zanzibar.

Hashil Seif katika kitabu hiki kataja majina ambayo yalifutika katika historia ya Zanzibar na kama utayakuta basi yatakuwa yemetajwa, ‘’in passing,’’ kama Waingereza wasemavyo, yaani majina hayo yatakuwa yametajwa kijuujuu.

Nitatoa mfano kwa uchache.

Hashil anawataja mara kadhaa katika kitabu Abdulrahman Babu, Khamisi Abdallah Ameir, Ali Sultan Issa na Badawi Qullatein katika siasa za kupigania uhuru wa Zanzibar.

Ahmed Rajab mmoja wa makomredi, ambae kaupitia mswada wa kitabu hiki ameniandikia na kunifahamisha kuwa Khamis Abdallah Ameir kama ‘’Theoretician,’’ sifa hii hutaisoma katika kitabu lakini katika mawasiliano yangu na Ahmed Rajab hili kanieleza na akasema kuwa Khamis Abdallah Ameir hakuwa mwanachama wa kawaida katika harakati zile.

Hili lilidhihirika baada ya mapinduzi kwa Khamis Abdallah Ameir kuwa memba wa Baraza la Kwanza la Mapinduzi.

Khamis Abdallah Ameir sikupatapo kumsikia kabla mpaka nilipomuona hapa katika ukumbi huu katika muhadhara wa Abdallah Kassim Hanga na sasa kaletwa tena na Hashil Seif.

Babu, Ali Sultan na Badawi Qullatein hawahitaji maelezo.

Bahati mbaya sana kuwa kitabu hakikuwekwa faharasha yaani ‘’index,’’ lakini laiti ingekuwapo faharasha msomaji angeweza kuona umihumu wa wazalendo hawa waliotajwa katika kitabu hiki kwa kuangalia ni mara ngapi majina yao yametajwa katika historia hii.

Huu ni mfano mmoja tu katika majina mengi ambayo hayajatajwa katika historia ya Zanzibar lakini Hashil Seif ameyarejesha na kueleza historia za watu hao katika kupigania uhuru wa Zanzibar.

Msomaji atamsoma Ali Sultan Issa aliyekuwa Mkomunisti ndani ya ZNP, Badawi Qulattein, Salim Rashid aliyekuwa katibu wa kwanza wa Baraza la Mapinduzi.

Wazalendo hawa historia zao zina mvuto wa pekee kabla na baada ya mapinduzi.

Ali Sultan ndiye aliyetengezeza mpango mzima wa kuwapeleka vijana wa ZNP, Cuba kwa mafunzo ya kijeshi kujitayarisha kwa mapinduzi.

Haya ndiyo msomaji atakutananayo katika kitabu hiki na ikiwa ni hivi ndivyo hali ilivyokuwa wakati wa kupigani uhuru wa Zanzibar haiwi tabu kuelewa sifa za makomredi katika uongozi na mchango wao katika mapinduzi.

Picha: Khamis Abdallah Ameir na Mwandishi. Picha ya pili Mwalimu Nyerere katika mkutano wa Hanga Mbele ya Kibarua Bar, Mnazi Mmoja.

Nisaidie kupata hiki " kwaheri ukoloni,kwaheri uhuru,^ kinauzwa wapi nikanunua
Inshallah
 
Nisaidie kupata hiki " kwaheri ukoloni,kwaheri uhuru,^ kinauzwa wapi nikanunua
Inshallah
Kinoa...
Kuna nakala ya bure soft copy mtandaoni na hard copy knapatika maduka yote ya Ibn Hazm Msikiti wa Mtoro, Manyema na Mtambani.
 
..Tatizo wanaonekana wamepatana sasa hivi lakini ikifika wakati wa uchaguzi wanarudi kwenye uhasama.

..Zanzibar inahitaji Tume ya Maridhiano na Ukweli, vinginevyo CCM wataendelea kurithishana mzigo wa kuficha ukatili uliofanywa na wanamapinduzi.

Lakini generation ya wana mapinduzi inazidi kupotea. na vizazi vya waliofuata kwenye madaraka pia. Lazima waridhiane. lazima wapeleke maendeleo Pemba ili visiwa vyote viwe na neema sawa.
Umaskini ndio unaleta shida. Mtu akila na kushiba, maneno mengi ya ajabu ajabu huwa yanapungua
 
JK,
Nguruvi anataabishwa na safari zangu na "kaimati."

Haya ndiyo anayoyajua kuhusu mimi kuwa ni mtu wa kula maraha ndani ya madege na ma 5 Star Hotel.

Ule ujuzi wangu katika historia ya Tanzania na niliyoandika hayataki.

Mimi nakua baba yangu mwana TANU na rafiki zake wakubwa wawili Abdulaziz Twala na Jaha Ubwa ni wana ASP kindakindaki.

Huu ndiyo ulikuwa msimamo wa wazee wetu wote wakitaka ASP itawale Zanzibar na waliyaunga mkono mapinduzi.

Lakini...

Walipokuja kujua ukweli na walipodhihirikiwa na unyama uliopitika katika mapinduzi na jela za mateso na mauaji zilipoanzishwa waliyachukia mapinduzi na wakayapa mgongo.

Baba yangu hakuacha kuugulia kifo cha Twala na Jaha Ubwa akiwakumbuka mara nyingi tu.

Haya ndiyo maisha yangu nimeishi ndani ya historia hizi.

Ama kuhusu Uislam naam sisi ni Waislam na hawa Wazanzibari ni Waislam na Twala, Karume na Jaha Ubwa ni Waislam.

Kwangu ni shida kuishi nje ya ukweli huu.

Ndiyo maana leo unaona CCM Zanzibar haiwezi kushinda uchaguzi huru na wa haki visiwani lazima msaada wa ushindi utoke Tanganyika.

Hii ndiyo historia ya mapinduzi na ukijua historia hii itakufungulia kuyaelewa yote yaliyopo Zanzibar hii leo.

Nani ni adui wa Zanzibar sasa kama wenyewe kwa wenyewe ndio walianza hayo? Watanganyika wanasingiziwa tu
 
Nani ni adui wa Zanzibar sasa kama wenyewe kwa wenyewe ndio walianza hayo? Watanganyika wanasingiziwa tu
Tangawizi,
Kulikuwa na kambi Tanganyika kijiji cha Kipumbwi iliyotumika kwa mafunzo ya wale Wamakonde wakata mkonge wa shamba la Sakura waliovushwa kuingia Zanzibar kusaidia mapinduzi.

Kushiriki kwa Tanganyika si kwa kusingiziwa.
 
Lakini generation ya wana mapinduzi inazidi kupotea. na vizazi vya waliofuata kwenye madaraka pia. Lazima waridhiane. lazima wapeleke maendeleo Pemba ili visiwa vyote viwe na neema sawa.
Umaskini ndio unaleta shida. Mtu akila na kushiba, maneno mengi ya ajabu ajabu huwa yanapungua

..tatizo ni kwamba kizazi kipya nacho kinafanya unyama ili kuficha unyama wa wanamapinduzi.

..kila uchaguzi mkuu kuna unyama unafanyika na lengo ni kuzuia yeyote wale wanaopinga unyama wa wanamapinduzi kuingia madarakani.

..sidhani kama kuna Mtz alitegemea utawala wa Dr.Shein utavuruga uchaguzi, au utamwaga damu, lakini hayo yote yalitokea.
 
Kwa kuwa kitabu hicho hakipatikani., basi makala haya tunaweza kuyaunganisha na kupata historia inayosemwa
 
KITABU KATIKA KUMBUKUMBU YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR SEHEMU YA KWANZA
PITIO LA KITABU MIMI, UMMA PARTY NA MAPINDUZI YA ZANZIBAR MWANDISHI: HASHIL SEIF HASHIL

Wako watu bado wa hai na pengine wapo hapa ukumbini wanaijua historia ya mapinduzi ya Zanzibar kwa kuyaona mapinduzi yenyewe na kwa kushiriki lakini hawajanyanyua kalamu kuandika wala kufungua mdomo kuihadithia na watakwenda kaburini na watazikwa na historia zao ambazo laiti wangeliziandika nchi ingenufaika pakubwa.

Hashil Seif Hashil anastahili pongezi kwa ujasiri huu wa kutuandikia kitabu na kutueleza historia ya Zanzibar ambayo si wengi wanaijua khasa vijana waliozaliwa baada ya mapinduzi mwaka wa 1964 ambao kwa sasa ni watu wazima.

Kuiandika historia ya mapinduzi ya Zanzibar ni kazi inayohitaji, ushujaa kwani si rahisi kuieleza na ukakosa kuwaudhi baadhi ya watu na wengine watu wako wa karibu sana.
Nawasalimu katika jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kuwatumia salaam zangu za kuadhimisha kumbukumbu ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, tutayalinda kwa gharama yoyote.

Nawatakia maadhimisho mema ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Kazi Iendelee!.

Paskali
 
Umeishapata jibu juu ya Utukufu wa mapinduzi haya Matukufu? Kama bado basi this is the right place,Mohamed Said yupo kukusaidia Pascal Mayalla
 
Nawasalimu katika jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kuwatumia salaam zangu za kuadhimisha kumbukumbu ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, tutayalinda kwa gharama yoyote.

Nawatakia maadhimisho mema ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Kazi Iendelee!.

Paskali
Unasemaje wakidokeza ilikuwa uvamizi na uasi wa watu kuoka bara? Si ya wenyeji?
 
huo ni urongo!
P
Unajuaje? Wewe kijana sivyo? Ulikuwepo?

Karume hakuandaa mapinduzi; Petterson (balozi wa Marekani wakati ule) anaandika katika kitabu chake Karume mwenyewe aliwahi kusikia kwa mbali tu akamwambia afisa Mwingereza kabla ya 12 Januari 1963 kutakuwa na vurugu akaona vema kuondoka kwenda bara. Aliyeendesha uasi alikuwa Okello aliyeongoza pia mauaji ya hovyo
("He recruited volunteers for a revolutionary force. Of the 330 men he said he had enlisted in the cause, most were mainlanders. .......... He told his men that when the fighting began, they were to kill all Arabs between the ages of eighteen and fifty-five. Young, old, and pregnant women were to be spared. Europeans, he ordered, were not to be attacked. Virgins and women whose husbands had been killed or detained should not be raped (all others, presumably, were fair game)" - Don Petterson, Revolution in Zanzibar, uk. 27)

Hii ni kweli "mapinduzi tukufu"?
 
Hilo ni jina la Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
P
 
Hilo ni jina la Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
P
Mzee Mallya, umekimbia na kuepukana na jibu. Unaleta jibu lako kwa Mohamed Said. Sina kazi na dhana za utukufu katika Uislamu. Si shauri yangu.
Nilikuletea taarifa ya mtu aiyeshuhudia mapinduzi (Petterson) anayemnukuu Okello aliyesema mwenyewe kundi lake lilikuwa hasa na watu kutoka bara - na wewe ulisema "uwongo" nilipouliza eti si wenyeji, ni watu wa bara waliendesha mapinduzi haya?

Halafu nilitaja maagizo ya kuchinja wanaume waliotazamiwa kuwa "Waarabu" lakini kutochinja wale wadogo na wazee juu ya miaka 55. Na kutobaka makundi fulani kati ya wanawake yao.
Nikauliza kuhusu utukufu wa maagizo hayo.
Hapa umekimbia kwa Mohammed Said, lakini mimi si huyu.
 
Ninachokisema mimi, ni jina la Mapinduzi ya Zanzibar yanaitwa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na jina hilo sikulitunga mimi, hivyo kuniuliza mimi kuhusu Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yana utukufu gani, ni kunionea bure!. Hili swali waulizwe wanao yaita Mapinduzi Matukufu na sio akina sisi tuliokuta yanaitwa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, badala ya kuwauliza waliyoyaita, mnatuuliza sisi!. Huku ni kutuonea bure!.

Asante. Ila nisipokosei, ni watu fulani tu wanaotumia lugha "mapinduzi matukufu". Kwa hiyo ni azimio kuchagua lugha yao?

Basi lakini hatujaanza na utukufu. Niliuliza kuhusu hoja kwamba haikuwa mapinduzi ya watu wa Zanzibar, lakini zaidi maasi ya watu kutoka bara. Hapa ulijibu "huo ni urongo!"
Nimeleta ushahidi wa balozi aliyekuwepo kiswani wakati ule na jinsi anayvomnukuu Okello.
Petterson anaandika: "He recruited volunteers for a revolutionary force. Of the 330 men he said he had enlisted in the cause, most were mainlanders. .......... He told his men that when the fighting began, they were to kill all Arabs between the ages of eighteen and fifty-five. Young, old, and pregnant women were to be spared. Europeans, he ordered, were not to be attacked. Virgins and women whose husbands had been killed or detained should not be raped (all others, presumably, were fair game)" - Don Petterson, Revolution in Zanzibar, uk. 27)

Kwa nini ulisema "uwongo!" ?
 
Back
Top Bottom