Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
- #221
''Ukimuuliza huyu mchochezi kwamba kati ya wazee wake hapo mtaa wa Gerezani amtaje shehe hata moja aliyetiwa kash kash au kuswekwa korokoroni na Wakoloni kwa uanaharakati wa kudai/kupigania uhuru wa Tanganyika ama na Wajerumani au Waingereza atabaki tu mdomo wazi!''
(Mag3)
Ndugu zangu,
Tuko 7K and counting...
Maswali hata kama yataambatana na lugha zisizopendeza huwa na faida yake.
Faida inakuja pale swali au maswali yanapokufanya ugeuze shingo kuangalia nyuma.
Babu yangu Salum Abdallah aliwahangaisha sana Waingereza wakati wa ukoloni lakini hawakumkamata na kumfunga.
Salum Abdallah alionja adha za jela mwaka wa 1964 katika Tanganyika huru.
Alifungwa Uyui Prison, Tabora pamoja na baadhi ya masheikh maarufu kati ya hao masheikh alikuwa Sheikh Jumanne Biasi.
Kama nilivyokwishaeleza Salum Abdallah aliongoza migomo mitatu ya wafanyakazi wa reli ambayo ilienea nchi nzima na kuwa ''general strike,'' mwaka wa 1947, 1949 na 1960 na huu mgomo wa 1960 ndiyo uliokuwa mkubwa kupita yote kwani ulidumu siku 82.
Miezi mitatu treni, meli na mabasi ya Tanganyika Railways vyote vilisimama.
Salum Abdallah alikuwa Rais na Christopher Kassanga Tumbo Katibu wa Tanganyika Railways African Union (TRAU).
Vipi waliweza kufanikisha mgomo huu?
Waliweza kufanikisha kwanza kwa kuwa na nidhamu ya hali ya juu ndani ya TRAU na pili kutokana na misaada ya fedha waliyopata kutoka Ujerumani ya Mashariki na kutoka kwa chama cha wafanyakazi wa reli Uingereza.
Fedha hizi ziliwawezesha kununua chakula na mahitaji muhimu kwa wafanyakazi ambao waligawiwa kwa kutumia kadi - chakula, mafuta ya kupikia, mafuta ya taa, viberiti nk.
Ilikuwa imebaki miezi michache Tanganyika ipate serikali ya madaraka ya ndani.
Ingawa TANU ilikuwa inaunga mkono harakati hizi lakini inaelekea Mwalimu Nyerere aliingiwa na hofu.
Kulia Christopher Kassanga Tumbo, Salum Abdallah na viongozi wengine wa TRAU
Nyerere alijua kuwa uhuru utakapopatikana mwaka wa 1961 ni lazima serikali yake itabidi ikabiliane na viongozi wa mfano wa Salum Abdallah na Kassanga Tumbo, viongozi ambao walikuwa wanapendwa na kusikilizwa na wananchi wafanyakazi.
Alipata hofu viongozi hawa watampa shida kama hii waliyokuwa wanaipa serikali ya Malkia.
Kukifanya kisa kirefu kuwa kifupi ni kuwa Salum Abdallah na viongozi wengine wa wafanyakazi walikamatwa na kuwekwa kizuizini mwaka wa 1964 mara baada maasi ya wanajeshi ili serikali ipate nafasi ya kuvunja vyama huru cha wafanyakazi na kuunda chama kipya kimoja NUTA kitakachokuwa chini ya TANU na serikali.
Harakati hizi hazijahifadhiwa katika historia ya uhuru wa Tanganyika wala katika historia ya vyama vya wafanyakazi wa Tanganyika.
Alfred Tandau ameandika kitabu, ''Historia ya Kuundwa Kwa TFL (1955-1962) na kuanzishwa kwa NUTA,'' (Dar es Salaam,1964) si babu yangu wala Kassanga Tumbo viongozi waliounda chama kilichokuja kuwa na nguvu na kikapigana bega kwa bega na TANU kudai uhuru wa Tanganyika wametajwa katika kitabu kile.
Nilikuwa nawashangaza sana walimu wangu Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam nilipokuwa nawaambia kuwa Tandau hajui historia ya vyama vya wafanyakazi aliyoandika katika kitabu chake na walipokuwa wananiomba ushahidi jibu langu lilikuwa rahisi na jepesi.
Nilikuwa nikisema babu yangu Salum Abdallah ni sehemu ya historia hiyo na historia ya TANU na juhudi za kudai uhuru wa Tanganyika.
Salum Abdallah alikuwa Mmanyema baba yake aliingia Tanganyika kama askari katika jeshi la Wajerumani.
Naomba ushauri wenu wasomaji wangu.
Nimfute Salum Abdallah katika historia ya uhuru wa Tanganyika kwa kuwa asili ya baba yake ni Belgian Congo?