Kitabu kipya: Dola, Kanisa na Tatizo la Udini Tanzania

Kitabu kipya: Dola, Kanisa na Tatizo la Udini Tanzania

Wengine walibadili dini ili wazee wake au makazi mjini au nafasi za masomo n.k
Na wapo waliobadili dini kwa kulazimishwa ili waweze kuoa katika koo zenye dini tofauti. Wengi wa hawa ni wale askari mamluki walioletwa na Wajerumani kupambana na Watanganyika na leo tunalazimishwa kuwatambua kama ndio wapiganaji wa uhuru Tanganyika.
Bagamoyo, Katika Uislam hakuna kushurutishana katika mambo ya dini.
Mtu muongo na mfitini katika ubora wake. Kuoa binti wa Kiislaam nyakati hizo ilikuwa ni lazima ubadili dini. Ndio maana tunakutana na majina Abdulwahid Sykes na wengineo. Na adhabu kwa binti wa Kiislaam anayebadilisha dini ilikuwa ni kifo.
 
Kwa hiyo naweza kwenda Saudia tena Maka nikafungua Kanisa na kuanza kueneza Injili kwa vibali pasipo kujali katiba yao inasema nini na wakanikubalia?
Khaligraph,
Hayo maswali unaniuliza mimi sina ujuzinayo.

Mimi hapa niulize kuhusu political history ya Tanganyika nk.
Nimefanya utafiti na nimeandika vitabu kadhaa.

Hapa ndipo ulipo ujuzi wangu hayo ya Saudi Arabia na kujenga makanisa ni nje ya upeo wangu.
 
January 6, 2020
Ujiji, Kigoma

Mzee Juma Ambrose na Simulizi za vuguvugu la kutambuliwa uasili wao kuelekea Uhuru
Wabembe na Wagoma wa Ujiji wakataa kutupa utambulisho na utamaduni wao mbele ya Waarabu na Waingereza. Harakati za Mzee Omari Buhoro aliyetumia ndumba za kienyeji ili vijana wa Ujiji wasiweze kulazimishwa kujiunga na jeshi la mkoloni kwa ajili ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia WWII

Mzee Juma Ambrose asilimulia jinsi wazee wa Ujiji walivyowadindia Waingereza na Waarabu, kisa majina yao kutotamkwa vyema na haiwezekani washurutishwe watupilie mbali Miungu yao ya kiasili kirahisi rahisi na kukumbatia Miungu ya Dini za kuja.

Wazee wa Kigoma Ujiji wanasema Miungu yao ya Asili ndiyo kitambilisho chao, mfumo wao na ndiyo salama yao. Nyumba maarufu ya Tanganyika House na milango ya vyumba vyake asili yake ni nini. Magonjwa ya Mizimu ya Kale dini hizi za kuja haziwezi kuyapoza lazima utaratibu wa mila ufuatwe Mzee Juma Ambrose anaendelea ktk simulizi sahihi za sisi ni kina nani kama waTanganyika...na matokeo yanakuwa mazuri watu wanaishi salama bila bughudha za dini za kuja...
Ujiji-Kigoma Tanzania
Ngoma ya Kibembe kushukuru Miungu ya Asili kupata mtoto

Mambo haya ya asili yanatuunganisha kwani yanafanana ktk jamii ya kiTanganyika hata unaweza kukabidhiwa mikoba uwashikie watani zako kujilinda hawa watu wa kuja na mashua wakikubadilikia anaendelea kuelezea umuhimu kuweka asili mbele Mzee Juma Ambrose...wa Ujiji Kigoma Tanganyika.

Chemchem ya Lutale na maajabu yake bila kumsahau Kamchape mtu aliyeeneza amani katika jamii na mchango wake kwa Tanganyika. Treni za ajabu usiku wa manane mali za Mzee mmoja. Simulizi kali zetu wenyewe toka ktk mazingira tunayoyajua na kuyaishi.

Sasa natambua kwanini waTanzania wanakuja juu kutambulishwa kwa makundi ya dini za kuja badala ya mchango wao kama wao ktk kuunda nchi huru Tanzania.
Source: Dar24 Media

Upendo mkubwa wa Kajiji wa Ujiji Kigoma

Historia ya Ujiji Kigoma Mzee Bilali anayeishi miaka 94 mfululizo ktk mji huu maarufu wenye simulizi kibao
 
Khaligraph,
Hayo maswali unaniuliza mimi sina ujuzinayo.

Mimi hapa niulize kuhusu political history ya Tanganyika nk.
Nimefanya utafiti na nimeandika vitabu kadhaa.

Hapa ndipo ulipo ujuzi wangu hayo ya Saudi Arabia na kujenga makanisa ni nje ya upeo wangu.
Hiki ndicho ulicho kiandika mzee M.S

Bagamoyo,
Katika Uislam hakuna kushurutishana katika mambo ya dini.

Bwana Ambrose ana haki ya kuamini akitakacho na hairuhisiwi kumbughudhi madam yeye hajawafanyia uadui wengine.

Haya ndiyo mafunzo ya Uislam.
1. Unasahau uislamu unawataka mpambane na imani zingine kivita (jihad) tena ni lazima.
2. Unasahau uislamu unatamka waziwazi aliye amini katika imani hiyo akitoka auwawe.
3. Unasahau uislamu una lengo la kuitawala dunia kwa namna yeyote.
4. Unasahau mimi nikitaka kumuoa binti wa kiislamu itanibidi nisilimu na ikitokea nimemvuta huyo binti kuja kwenye Ukristo basi ni mwendo wa laana na midua mibaya juu yake.
.
Mfano mzuri ni mwanamuziki Kadjanito aliyeolewa na kijana wa Kikristo na kuamua kuokoka. familia yake imemtenga hadi waleo na imemtamkia laana na kumnenea mabaya mno kisa midini ya kuletewa😢
.
Mzee M.S kwa makusudi kabisa unaamua kulipotosha hili eti uislamu haulazimishi kitu katika mambo ya imani kisa tu ni kitu unachokiamini pole sana
 
Na wapo waliobadili dini kwa kulazimishwa ili waweze kuoa katika koo zenye dini tofauti. Wengi wa hawa ni wale askari mamluki walioletwa na Wajerumani kupambana na Watanganyika na leo tunalazimishwa kuwatambua kama ndio wapiganaji wa uhuru Tanganyika.
Mtu muongo na mfitini katika ubora wake. Kuoa binti wa Kiislaam nyakati hizo ilikuwa ni lazima ubadili dini. Ndio maana tunakutana na majina Abdulwahid Sykes na wengineo. Na adhabu kwa binti wa Kiislaam anayebadilisha dini ilikuwa ni kifo.
Mag3,
Ungeuliza swali tu bila ya maneno makali ingekuwa ustaarabu na tungefanya mjadala wa kupendeza.

Baada ya kufika Tanganyka na Wajerumani kuituliza nchi hawa Wazulu wakatiwa katika jeshi lililopewa jina, ''Germany Constabulary,'' na mkuu wa jeshi hili alikuwa Affande Plantan ambae huko kwao Kwa Likunyi, Imhambane Mozambique alijulikana kama Chief Mohosh.

Germany Constabulary waliishi kwenye kambi za jeshi na watoto wao walijengewa shule pale ilipo leo Ocean Raod Hospital.

Ilikuwa mtoto akizaliwa Wajerumani wanamsajili na kutoa jina hii ndiyo ilikuwa kawaida yao na wakiwapa watoto majina ya Kijerumani ambayo ni ya Kikristo.

Ndiyo maana watoto wao walikuwa na majina ya Kleist, Schneider, Thomas, Mashado nk ingawa wazazi wao walikuwa Waislam.

Lakini wakifika nyumbani watoto hawa baba zao huwapa majina ya Kiislam.
Kleist jina lake ni Abdallah, Schneider ni Abdillah, Mashado ni Ramadhani nk.

Hakuna anaelazimisha historia hii ya uhuru hivi nilivyoandika ndivyo ilivyokuwa.
Babu yangu Salum Abdallah ni mtoto wa Abdallah Samitungo Muyukwa askari mamluki kutoka Belgian Congo.

Lakini huyu mtoto wa mamluki wa Wajerumani ni mmoja wa waasisi wa TANU na akaunda chama cha wafanyakazi wa reli - Tanganyika Railways African Union (TRAU) kama rais muasisi na kashiriki katika kuigania uhuru wa Tanganyika.

Hatuwezi kubadili historia hii.

1578337386023.png

Frederick Mchauru

Soma kisa cha babu yangu Salum Abdallah na Fredrick Mchauru 1947 upime kati ya hawa wawili nani alikuwa kibaraka wa Waingereza na nani alikuwa mzalendo mpigania haki ya Watanganyika:

1578337642323.png

Kulia Salum Abdallah na viongozi wa TRAU Tabora wanaonyesha picha ya kuchora ya Katibu wa TRAU Kassanga Tumbo wakati wa kupigani uhuru wa Tanganyika

Nini michango ya watoto hawa wa Wazulu na Wamanyema?

Schneider Abdillah Plantan ndiye aliyesaidia sana kuwaingiza madarakani Dr. Vedasto Kyaruzi na Abdul Sykes kuongoza TAA 1950 kwa nia ya kuunda chama cha siasa.

Wananchi kwa mara ya kwanza walisoma jina la Nyerere katika gazeti Zuhra lililokuwa likimilikiwa na Mashado Ramadhani Plantan na ndiye alikuwa mhariri wake mwaka wa 1953.

TANU ilipoundwa Zuhra ndiyo gazeti likitumiwa na TANU kujitangaza kwa wananchi.

Sihitaji kukueleza Kleist Sykes na wanae wamefanya nini katika ukombozi wa Tanganyika.
Lakini wote hawa walizaliwa Tanganyika chini ya utawala wa Waingereza.
 
Tusipoenda msikitini hicho kitabu hatukipati? Kwa nini kiuzwe misikitini tu? Nia ya kukiuza misikitini ni nini?

Vv

Sent using Jamii Forums mobile app
Vyamavingi,
Vitabu haviuzwi msikitini.

Mfano wa maduka haya ni kama mafano wa Cathedral Bookshop ndani ya kanisa la St. Joseph's.

Ndani ya eneo la kanisa hili kuna bookshop ya miaka mingi sana na mimi nimenunua vitabu hapo toka nasoma shule hapo.

Ibn Hazm Media Centre maduka yake ya vitabu wala huwezi kufananisha na Cathedral Bookshop.

Haya maduka yako katika mitaa ambako iko misikiti hiyo na maduka haya ni vijumba vidogo tu vya kupangisha katika hali duni na mnunuzi haingii ndani ya duka kama lile la Cathedral ambako kuna viyoyozi nk.

Mnunuzi anasimama barabarani kama yuko katika duka lolote na pilipili bizari Manzese au Buguruni.

Duka la Msikiti wa Mtoro liko katika kichochoro kinachounganisha Mtaa wa Narung'ombe na Mahiwa ulipo msikiti duka ni nyumba ya kupanga jirani na msikiti.

1578340155386.png

1578339850627.png

Ibn Hazm Media Centre Msikiti wa Mtoro
Unaweza kufananisha kiduka hiki na Cathedral Bookshop?
 
Uko msikitini ndipo penye wafuasi wake wa vitabu vyake anawaandaa ili siku moja wakinukishe anaamini uhuru wa tanganyika uliletwa na masheik eti mapadiri hawakuonekana.
The boy tz,
Historia ya TANU na uhuru ndivyo ilivyokuwa ingawa unaandika kwa kejeli mimi nakuchukulia labda ni kijana mdogo na ujana una matatizo yake.

Katika mjadala mzito kama huu lugha za ''kinukishe,'' si mahali pake.
 
Hiki ndicho ulicho kiandika mzee M.S

1. Unasahau uislamu unawataka mpambane na imani zingine kivita (jihad) tena ni lazima.
2. Unasahau uislamu unatamka waziwazi aliye amini katika imani hiyo akitoka auwawe.
3. Unasahau uislamu una lengo la kuitawala dunia kwa namna yeyote.
4. Unasahau mimi nikitaka kumuoa binti wa kiislamu itanibidi nisilimu na ikitokea nimemvuta huyo binti kuja kwenye Ukristo basi ni mwendo wa laana na midua mibaya juu yake.
.
Mfano mzuri ni mwanamuziki Kadjanito aliyeolewa na kijana wa Kikristo na kuamua kuokoka. familia yake imemtenga hadi waleo na imemtamkia laana na kumnenea mabaya mno kisa midini ya kuletewa😢
.
Mzee M.S kwa makusudi kabisa unaamua kulipotosha hili eti uislamu haulazimishi kitu katika mambo ya imani kisa tu ni kitu unachokiamini pole sana
Khaligraph,
Huwa nataabika sana ninapokutana na watu kama wewe.
Huwa na sijui kwa nini kutaka mimi nijibu maswali ya fikh yaani sheria katika Uislam.

Najitahidi kuwaeleza kuwa mimi elimu yangu ni ya Kizungu lakini watashikilia tu kunitwisha mzigo nisioweza kuubeba.

Lakini sina ujinga katika dini yangu ila unaponipa maswali ya fikh hapo lazima nikueleze ukweli kuwa si fani yangu.

Kuna mtu alipata kuniuliza kuwa lugha ya Kiingereza ninayoandika katika vitabu vyangu naandika kwanza kwa Kiswahili kisha mtu anatafsiri kwa Kiingereza?

Yapo mengi na yanachekesha sana.
Nakuelewa.
 
Uko msikitini ndipo penye wafuasi wake wa vitabu vyake anawaandaa ili siku moja wakinukishe anaamini uhuru wa tanganyika uliletwa na masheik eti mapadiri hawakuonekana.
Ukimuuliza huyu mchochezi kwamba kati ya wazee wake hapo mtaa wa Gerezani amtaje shehe hata moja aliyetiwa kash kash au kuswekwa korokoroni na Wakoloni kwa uanaharakati wa kudai/kupigania uhuru wa Tanganyika ama na Wajerumani au Waingereza atabaki tu mdomo wazi!

Kuwaenzi hawa mamluki (askari waliokodiwa na Wakoloni) eti ndio wapigania uhuru wa Tanganyika ni dhihaka kubwa inayoweza kulinganishwa tu na dai la kutaka kuwaenzi Makaburu wa Afrika kusini kuwa ndio walikuwa wapigania uhuru wa Afrika Kusini ukiwadhihaki wazalendo kama Marehemu Nelson Mandela na wazalendo wengine.

Mfano mzuri ni hapa kwa jirani zetu visiwani mpaka leo wanakataa kata kata kumtambua Field Marshall John Okelo kama kiongozi wa vita ya mapinduzi kuwatimua Wakoloni Waarabu. Dai la wazawa ni kuwa alikuwa ni askari wa kukodi tu lakini hapa bara tunalazimishwa kuwatambua mamluki wa aina hiyo hiyo.

Hizi ngano za Mohamed Said abaki tu akiwalisha hao wenye uelewa mdogo wanaozimeza tu bila kuzitafuna na kuhoji lakini wenye uelewa mkubwa lazima watauliza, kulikoni? Je Tanganyika haikuwa na wazawa wapigania uhuru hadi mamluki waliohifadhiwa mtaa wa Gerezani ndio wawe vinara katika mapambano ya uhuru dhidi ya wakoloni?

Mfano mwingine ni huyu Abdulwahid Sykes anayedaiwa kuwa askari wa kukodi aliyepelekwa Burma na serikali ya kikoloni ya Waingereza. Fikiria kama angebaki huko halafu akajitokeza mtu anaandika historia na kudai aenziwe kama mpigania uhuru wa huko Burma? Bila shaka wananchi wa Burma hawangenyamazia upuuzi kama huo.

Kuna maswali chungu nzima ya kumuuliza huyu muongo na mchochezi lakini tatizo ni kuwa anapoulizwa anajibu kwa kunukuu maneno yale yale aliyoyaandika kwenye kitabu chake yeye mwenyewe...eti huo ndio ushahidi kuwa anayoyaandika ni kweli. Utadhani Tanganyia haikuwa na watu... believe this and you'll believe anything!

Tukiacha hilo Mohamed Said, haelezi kwamba hawa wazee wake walikuwa wapi toka TANU inaundwa hadi uhuru. Je nyakati hizo Mwalimu Nyerere alikuwa na uwezo gani wa kuhakikisha hawachaguliwi kushika nafasi za juu ndani ya chama pamoja na wingi wao na sifa kibao wanazosukumiziwa? Kwa kweli huyu mtu ni mchochezi na mtu hatari sana.

Muda si mrefu ataingia humu na kudai ninaandika kwa ghadhabu na kumnukuu Mwalimu wake alivyomkanya kuwa mtulivu! Yaani hizi santuri zake zimechuja hadi zinatia kinyaa. Kila akichangia JF ni wazee wake, mashehe wake, Wazulu wake, Wamanyema wake na Wanubi wake. Hata siku moja hachangii mada zinazohusu Tanzania ya leo na huu ukoloni mamboleo. Mohamed Said, huu ni mwaka 2020, amka!
 
Ndugu wasomaji
Hadi sasa tumegonga 6K and counting...

Katika utafiti wa kitabu cha Abdul Sykes sikukuta popote ambapo masheikh walikamatwa na kutiwa misukosuko kwa ajili ya kufanya siasa.

Masheikh wengi walikuwa wajumbe katika Baraza la Wazee wa TANU lililokuwa na wajumbe 120 chini ya Mwenyekiti Sheikh Suleiman Takadir.

Halikadhalika sikukutana na wanaharakati katika TAA na TANU hata wale waliofahamika kwa ''ukorofi'' kama Ally Sykes, Zubeir Mtemvu na Mwalimu Steven Mhando ambao walipata kukamatwa na kuwekwa ndani ukiacha misukosuko waliyokuwa wakiipata kutoka Special Branch ya kuvamiwa majumbani kwao na kufanyiwa upekuzi.

1578429829006.png

Dennis Phombeah

Ally Sykes na Dennis Phombeah walikamatwa Salisbury, Southern Rhodesia (Zimbabwe) mwaka wa 1953 wakiwa njiani kuelekea Lusaka, Northern Rhodesia (Zambia) kuhudhuria mkutano ulioitishwa na Kenneth Kaunda, Katibu Mkuu wa African National Congress (ANC) kwa vyama vya siasa Kusini ya Sahara vilivyokuwa vinapigania uhuru wa nchi zao.

Walipigwa PI (wahamiaji haramu) walipowasili uwanja wa ndege na kufungwa kwenye banda la nguruwe usiku kucha hadi asubuhi walipopelekwa uwanja wa ndege na kutiwa ndani ya ndege kuelekea Blantyre, Nyasaland kwa safari ya kurudi Dar es Salaam.

Ally Sykes alikuwa Mzulu aliyezaliwa Tanganyika na Dennis Phombeah Mnyasa aliyehamia Tanganyika.

1578370128356.png

Nimepata kuandika kisa hiki kwa kirefu na kilichapwa katika gazeti la Raia Mwema:

Kuna kisa kingine cha kukamatwa Iddi Faiz Mafungo Turiani wakati anatoka Tanga kukusanya fedha za safari ya kwanza ya Mwalimu Nyerere UNO mwaka wa 1955.

Iddi Faizi Mafungo kadi yake ya TANU ni no. 24 na alikuwa ndiye Mwekahazina wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na pia Mwekahazina wa TANU.

Alipokuwa anarudi Dar es Salaam katika basi akitoka Tanga kwa Mwalimu Kihere aliyemkabidhi fedha alizochangisha Tanga, makachero wakalivamia basi na Iddi Faiz akakamatwa na kuletwa Dar es Salaam kwa mahojiano.

Iddi Faiz alikuwa Mmanyema aliyezaliwa Tanganyika.

Nini ushauri wenu wasomaji wangu.

Niifute historia hii katika kitabu cha Abdul Sykes matoleo yananayofuata?

Kadi ya TANU ya Ally Sykes ni no. 2 na Dennis Phombeah no. 5.

1578374438110.png

Mkono wa kulia wa Mwalimu Nyerere aliyevaa kanzu, koti na tarbush ni Iddi Faiz Mafungo Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam safari ya kwanza ya Nyerere UNO 1955
 
Waelimishe waislamu wafanyeje ili kujikwamua hapa sasa hivi walipo, sio kuwajaza chuki kwa mambo yaliyopita ambayo hayarekebishiki, wewe ni mchochezi mkubwa wa chuki, kwa iyo unataka waislamu wabebe mapanga wawakate waliowadhulumu, kuwa na busara hata kidogo
😆😆😆😆😆 Mkuu unafaidika nini na waislam kudhulumiwa ?
 
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38] Mkuu unafaidika nini na waislam kudhulumiwa ?
Erythrocyte,
Mimi nimeandika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Bahati mbaya imekutia hofu.

Unaniuliza maswali yasiyojibika kuwa kwa nini nimeandika historia hii na faida zake.

Nami naomba nikuulize swali.
Yapi ukiyajua?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom