Ukimuuliza huyu mchochezi kwamba kati ya wazee wake hapo mtaa wa Gerezani amtaje shehe hata moja aliyetiwa kash kash au kuswekwa korokoroni na Wakoloni kwa uanaharakati wa kudai/kupigania uhuru wa Tanganyika ama na Wajerumani au Waingereza atabaki tu mdomo wazi!
Kuwaenzi hawa mamluki (askari waliokodiwa na Wakoloni) eti ndio wapigania uhuru wa Tanganyika ni dhihaka kubwa inayoweza kulinganishwa tu na dai la kutaka kuwaenzi Makaburu wa Afrika kusini kuwa ndio walikuwa wapigania uhuru wa Afrika Kusini ukiwadhihaki wazalendo kama Marehemu Nelson Mandela na wazalendo wengine.
Mfano mzuri ni hapa kwa jirani zetu visiwani mpaka leo wanakataa kata kata kumtambua Field Marshall John Okelo kama kiongozi wa vita ya mapinduzi kuwatimua Wakoloni Waarabu. Dai la wazawa ni kuwa alikuwa ni askari wa kukodi tu lakini hapa bara tunalazimishwa kuwatambua mamluki wa aina hiyo hiyo.
Hizi ngano za
Mohamed Said abaki tu akiwalisha hao wenye uelewa mdogo wanaozimeza tu bila kuzitafuna na kuhoji lakini wenye uelewa mkubwa lazima watauliza, kulikoni? Je Tanganyika haikuwa na wazawa wapigania uhuru hadi mamluki waliohifadhiwa mtaa wa Gerezani ndio wawe vinara katika mapambano ya uhuru dhidi ya wakoloni?
Mfano mwingine ni huyu Abdulwahid Sykes anayedaiwa kuwa askari wa kukodi aliyepelekwa Burma na serikali ya kikoloni ya Waingereza. Fikiria kama angebaki huko halafu akajitokeza mtu anaandika historia na kudai aenziwe kama mpigania uhuru wa huko Burma? Bila shaka wananchi wa Burma hawangenyamazia upuuzi kama huo.
Kuna maswali chungu nzima ya kumuuliza huyu muongo na mchochezi lakini tatizo ni kuwa anapoulizwa anajibu kwa kunukuu maneno yale yale aliyoyaandika kwenye kitabu chake yeye mwenyewe...eti huo ndio ushahidi kuwa anayoyaandika ni kweli. Utadhani Tanganyia haikuwa na watu...
believe this and you'll believe anything!
Tukiacha hilo
Mohamed Said, haelezi kwamba hawa wazee wake walikuwa wapi toka TANU inaundwa hadi uhuru. Je nyakati hizo Mwalimu Nyerere alikuwa na uwezo gani wa kuhakikisha hawachaguliwi kushika nafasi za juu ndani ya chama pamoja na wingi wao na sifa kibao wanazosukumiziwa? Kwa kweli huyu mtu ni mchochezi na mtu hatari sana.
Muda si mrefu ataingia humu na kudai ninaandika kwa
ghadhabu na kumnukuu Mwalimu wake alivyomkanya kuwa mtulivu! Yaani hizi santuri zake zimechuja hadi zinatia kinyaa. Kila akichangia JF ni wazee wake, mashehe wake, Wazulu wake, Wamanyema wake na Wanubi wake. Hata siku moja hachangii mada zinazohusu Tanzania ya leo na huu ukoloni mamboleo.
Mohamed Said, huu ni mwaka 2020, amka!