Kitabu Kipya; Tabia za kitajiri za kuishi kila siku ili kufika kwenye utajiri mkubwa

Kitabu Kipya; Tabia za kitajiri za kuishi kila siku ili kufika kwenye utajiri mkubwa

Tatizo sio kisoma vitabu,bali tatizo ni kufanyia kazi vya kitabuni.

Na hapo ndipo tunapofeli ukiwemo wewe na mimi.
Aisee! Acha Kabisa nimepiga kazi kwa kufuata kanuni zote kwa miaka bila matokeo ya kuridhisha
 
Mkuu hautakiwi kubeza juhudi za watu,na tunatakiwa tutambue kwamba kuna watu wana maarifa mengi lakini kuyafanyia implementation ndio tatizo.

Ila wanaweza kuchota maarifa hayo wakampa mtu mwingine akaya implement na akapata matokeo chanya.

Mimi binafsi nilikuwa mvivu sana kusoma ila nilikuwa nampa motivesheni mdogo wangu kuhusu kuooma na akawa anafaulu vizuri na akawa anapenda kila siku niomgee nae kumpa motivesheni,lakini mimi niliyokuwa namuambia sikuwa nayafanyai kazi ila yeye yalimfaa akafaulu vizuri sana.

Sasa na yeye angeliniangalia mimi kwa nini sina matokeo mazuri alafu najifanya motivesheni spika basi asingefika pale alipo.

Tujaribu kuwa na mitazamo chanya wakuu tusiwe na hoja za kitoto kama hizi.
Hoja za kitoto unaachana nazo wewe unaleta za kikubwa.
 
Vitabu vya aina hiyo nimevisoma tangu nikiwa kijana na sasa ni mzee lakini sijaona matokeo mkuu.
Mkuu,
Kusoma kitabu ni jambo moja,
Kufanyia kazi yale uliyojifunza ni jambo jingine muhimu na la msingi kabisa.
Hakuna mtu anayejifunza kuogelea kwa kusoma vitabu tu, lazima uingie kwenye maji, uyanywe, ukaribie kuzama ndiyo ujifunze kweli.

Kama upo serious kweli unataka mabadiliko kwenye maisha yako, pata na usome kitabu hiki cha TABIA ZA KITAJIRI, halafu ukikimaliza tuwasiliane nitakupa Coaching ya mwezi mmoja bure kabisa kukusimamia kuziishi tabia hizo za kitajiri, nakuhakikishia utayaona mabadiliko.
Na kama kwa huo mwezi mzima ambao umeziishi tabia hizo za kitajiri hutapata manufaa yoyote, nitakurudishia fedha uliyonunulia kitabu.
Wasiliana sasa na watu wa mauzo kwa namba 0752 977 170 kujipatia nakala yako.
Kisha wasiliana na mimi moja kwa moja kwa namba 0717 396 253 kwa ofa ya coaching niliyokupa.
Karibu sana mkuu.
 
Back
Top Bottom