Kitabu kipya: Tanzania na propaganda za udini na prof. Ibrahim Noor

Kitabu kipya: Tanzania na propaganda za udini na prof. Ibrahim Noor

Ahsante Mohammed Said tutasoma kuongeza ilm.
Suala hili propaganda wakati nipo darasa la 4 mwalimu wa siasa siku moja alitutolea historia ya kujengwa Beit el ajab kuwa kila nguzo moja kabla ya kuwekwa basi warabu walimtia ndani ya shimo mwafrika mmoja. Huku mwalimu yule akiwasumbulia watoto wa kiarabu mle darasani.
Ni chuki na fitna chafu sana.
Hali ile ilinifanya nimuulize mzee wangu kuwa haya kweli yametendwa na warabu? Mzee wangu alhamdulilah amesoma na alikua na alikua daktari anajua mengi alikua akipenda sana kusoma. Alikua akijua mengi kuona hali ile huko shule kuanzia siku ile kila kabla ya kulala alikua akitupa historia ya kweli ya Zanzibar . Nilikua mdogo lakini ilinisaidia sana kuona ukweli wa proolpaganda zile chafu dhidi ya waislam..
Katika picha za kubuni zs uongo ni zile za warabu wakubeba pembe za tembo.
Ukiangalia zile picha utaona pembe in ukubwa kuliko tembo wenyewe !
 
Last edited by a moderator:
Sasa wewe ni mbaya zaidi kufikiria mambo hata hujakisoma kitabu na kuanza chokochoko, sioni kama kinauzwa misikitini ni duka lililo nje ya msikiti, na misikitini sio sehemu ya kufanya biashara ni sehemu ya ibada.

Masomo bookshop ni mbali kabisa na msikiti. kwanini una chuki zilizowaziwazi na uislam?
binaadamu hatakiwi kuwa hivyo lol
PTER
 
Last edited by a moderator:
Kwa muonekano wa cover na muhtasari uliotolewa huyo profesa anaendeleza udini badala ya kinyume chake.

Hivi kwa nini hawa jamaa zetu hata wakisoma vipi huwa inferiority complex haiwaishii? Na hii tabia yau-cry wolf ni mbaya sana..siku wolf wa kweli akija sijui wataliaje?
 
Kabla hujasoma historia yeyote soma historia ya mwandishi. Maudhui ya kitabu yako wazi, kinapigiwa debe na Mohammed Said!, kinauzwa msikitini!, kimeandikwa na mwarabu mwislamu, na kinaelezea mahusiano ya waafrika na waarabu (baba zake) wakati wa utumwa. Unategemea aandikeje?

angekaa kimya badala ya kuandika utumbo na kuushushia hadhi uprofesa wake
 
Ahsante Mohammed Said tutasoma kuongeza ilm.
Suala hili propaganda wakati nipo darasa la 4 mwalimu wa siasa siku moja alitutolea historia ya kujengwa Beit el ajab kuwa kila nguzo moja kabla ya kuwekwa basi warabu walimtia ndani ya shimo mwafrika mmoja. Huku mwalimu yule akiwasumbulia watoto wa kiarabu mle darasani.
Ni chuki na fitna chafu sana.
Hali ile ilinifanya nimuulize mzee wangu kuwa haya kweli yametendwa na warabu? Mzee wangu alhamdulilah amesoma na alikua na alikua daktari anajua mengi alikua akipenda sana kusoma. Alikua akijua mengi kuona hali ile huko shule kuanzia siku ile kila kabla ya kulala alikua akitupa historia ya kweli ya Zanzibar . Nilikua mdogo lakini ilinisaidia sana kuona ukweli wa proolpaganda zile chafu dhidi ya waislam..
Katika picha za kubuni zs uongo ni zile za warabu wakubeba pembe za tembo.
Ukiangalia zile picha utaona pembe in ukubwa kuliko tembo wenyewe !

Crabat,
Muhimu sana sasa sisi tukaandika historia yetu wenyewe.
 
kwa muhtasari huo uliowekwa kitabu ni one-sided na kimelenga kujenga kuwa uislam unangamizwa kwa propaganda nchini, mbaya zaidi kinauzwa sehemu za misikiti hii maana yake hadhira iliyolengwa ni waislamu wasome waanzishe chokochoko zisizo na mashiko.
kwa maoni yangu Prof kachemsha sana na anachembechembe za udini zaidi hafai kuwa fani katika hadhira jisomeeni wenyewe hukohuko upesi mjilipue kwa sababu huwa hamchelewi kujilipua.

unamfanyia favor kusema ana chembechembe za udini..ni mdini through and through..na hicho kitabu wasome, may be it will make them feel better..besides what else have they zaidi ya hizo feelings zao?
 
Kabla hujasoma historia yeyote soma historia ya mwandishi. Maudhui ya kitabu yako wazi, kinapigiwa debe na Mohammed Said!, kinauzwa msikitini!, kimeandikwa na mwarabu mwislamu, na kinaelezea mahusiano ya waafrika na waarabu (baba zake) wakati wa utumwa. Unategemea aandikeje?
Binafsi siwezi kujihangaisha maana najua ni yale yale ya kina Mohamed Said (Mtu anafanya uchambuzi wa kitu ambacho yeye binafsi ana maslahi nacho then unategemea awe huru.Kwanza kwa muhtasari kidogo huo hapo juu inaonesha...."Waislam wanaonewa,Waarabu wamebambikiwa uovu wa biashara ya utumwa.Muslims were right,are righta and they will always be.Non muslims have never done anything good.Kwa ufupi nimegrasp hayo..
 
Last edited by a moderator:
Kitabu kingine kilichoandikwa na muislamu ambaye elimu haikumsaidia. Anachochea udini kwa kujaribu ku insinuate kuwa wafuasi wa allah wanaonewa.
Ukiangalia picha ya jalada imelenga kuonesha eti wakristo wanaua watu. Huo si uchochezi?
 
Jamaa limeenda shule na elimu aliyoweza kuiambulia ni ile ya kwamba waarabu walitangulia kufika pwani. Calling it stupid is to give the book a compliment
 
Hiyo "cover" ndo imenivuruga kwakweli. Jamaa seems to be so BIAS ktk analysis yake.
Ngoja tukitafute.
 
[/B][/B]Mkuu Maalim , kwanza asante kutupatia taarifa hizi, sisi wapenzi wa kusoma vitabu, tutakinunua na kukisoma hiki kitabu cha Tanzania na Propaganda za Udini, ila hata kabla sijakinunua na kukisoma, kiukweli kabisa toka ndani ya nafsi yangu, the sixth sense inanieleza the 'motive behind' mwandishi wa kitabu hiki, Prof. Ibrahim Noor Shariff, ni 'ill motive!'. Tangu Mlango wake wa Kwanza unaohusu “Taarikh ya Kuwasili Kwa Wabantu, Washirazi na Waarabu Pwani ya Afrikaya Mashariki.” ameanza na maurongo yaliyokubuhu!, hapa anadanyanya wazi mchana kweupe kwa maushahidi yake ya uongo kwamba eti Waarabu wamefika Pwani ya Afrika Mashariki maelfu ya miaka iliopita kabla ya Wabantu, tangu karne ya 16 B.K!. The ill motive ya mlango huu ni kuonesha kwamba Waarabu si wageni bali ni wenyeji wenye haki hapa sawasasa kwenye Pwani ya Afrika Mashariki sawa na wenyeji wengineo.

Yaani hapa huyu Mwarabu, anataka kuwafanyia Afrikanization hawa wavanizi wa Kiarabu ili kuwahalaliasha eti na wao, ni wenyenyeji halali wa Afrika Mashariki, na wakati huo huo, kuwaondolea Wabantu, uenyeji wao wa asili, kwa kuonyesha kuwa hata hao Wabantu, Afrika ya Mashariki sio kwao asili bali nao pia ni wahamiaji tuu kama Waarabu!. Huu ni uongo uliokubuhu wa mchana kweupe!.

Lengo ni kuzuia kinachoweza kuja kuwapata Waarabu wa Afrika Mashariki na sana sana Waarabu wa Zanzibar ambao wametoka kwao Omani juzi juzi tuu mwaka 1832 wakiongozwa na Sultan Seyyed Said aliye yahamisha makao yake makuu toka Oman hadi Zanzibar!. Huyu sio tuu ni mvamizi bali pia ndiye mporaji mkuu, aliyejitwalia visiwa hivyo kama ameviokota as if hakumkuta mtu yoyote ili hali wenyeji walikuwepo!. Siku ile ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar, siungi mkono mauaji yoyote ya Waarabu, bali wangeambiwa tuu kistaarabu, wafungeshe kilicho chao, wao na wazalio wao, wajirudie kwao Omani walikotoka na kutuachia visiwa vyetu!.

Hili swali la Waarabu wamekujaje Pwani ya Afrika Mashariki, litakuja kurudi tuu mbele ya safari hivyo ushauri wangu, ni kujituliza tuu na kuishi kwa unyenyekevu wa hali ya juu sana kwa kujihesabu wanaishi hapo kwa hisani tuu, vinginevyo watatimuliwa warudi kwao Oman walikotoka, wao na vizalia vyao!.

Hizi historia za kutunga tunga kutaka kuwahalalisha madhalimu hawa waliowauza mababu zetu kama bidhaa!, hazitasaidia kitu!, no wonder kila siku wanashinda uchaguzi lakini kamwe hawatakabidhiwa nchi, na 2015 watashinda tena na moto ni ule ule!. Mwarabu atoke kwao, aje akutawale, babu zako awauze, kisha mumpindue halafu leo mumrudishe eti kisa amechaguliwa!, hii haitakaa itokee!.

Kesho ni sikukukuu ya Muungano, tutakukumbusheni hiyo Zanzibar ilikuwa ni sehemu ya Tanganyika, hivyo huu muungano ni wa milele.

As long as hii ni lilterally work, ngoja nikitafute na kukisoma halafu turudi humu kumwaga mbichi na mbivu!, ila kiukweli lazima hata mtoto wa darasa la 4 akiisikia hii acheke, ati Waarabu nao kwao ni Afrika Mashariki, na Wabantu nao pia ni wageni!. OMG!.

Pasco

Kaka hv wale makaburu wa south....wao kwao ni wapi??! Yaan mfano wakiulizwa watasema kwao ni wapi???!
 
Duh kweli wanajamvi tuna safari ndefu, Yaani kuna watu humu ndani wanatia huruma sana, hawaelewi hata kidogo. Hii jamii hii, kweli ni jamii kichaa.
 
Naam acha dawa iwaingie. .. wataanza kumwaga povu muda si mrefu
 
Kaka hv wale makaburu wa south....wao kwao ni wapi??! Yaan mfano wakiulizwa watasema kwao ni wapi???!
Kasome historia ya makaburi wa Afrika ya kusini, halafu leo atokee kaburu mmoja, aandike historia kuwa Afrika Kusini japo wao ni wahamiaji, walipofika hawakukuta mtu, na hao Wabantu nao pia ni wahamiaji tuu kama wao! hivyo wote wako sawa!.

Hiki kitabu kinataka kueleza uongo kuwa eti Waarabu walihamia Pwani ya Afrika ya Mashariki karine ya 16 BC hawakukuta wenyeji wowote, kwa sababu muda huo ndio huo huo Wabantu walihamia Afrika, ili kujenga hoja kuwa Waarabu Afrika Mashariki ni kwao kama ilivyo kwa Wabantu!. Kama Waarabu walihamia na Wabantu pia walihamia!, hivyo Bara la Afrika Waarabu walipohamia walilikuta tupu kabisa halina wenyewe!.

Wazungu walipokuja angalau walikuwa na ustaarabu fulani wa recognition ya waliowakuta, hivyo hawakujichukulia tuu maeneo kama wameokota!, waliyanunuatoka kwa wenyeji waliowakuta!. Tumesoma historia ya Karl Peters na ile mikataba yake na Sultani wa Msovero, japo ni ya kitapeli, lakini ni mikataba!.

Tumesema jinsi Hassan Bin Amiri alivyokinunua kisiwa cha Kilwa toka kwa wenyeji na kukilipia kwa kitambaa kinachozunguka kisiwa kizima!.

Huyu Mwarabu wa Zanzibar, alipokuja ile juzi juzi tuu, aliingia mkataba na nanni wa kuvimiliki hivyo visiwa?!. Yaani kwa kifupi alivitwaa tuu kama vile ameviokota!, hivyo lugha rasmi ni alivivamia na kwa kawaida mvamizi huingia kwa nguvu na mwisho wake hufurushwa kwa nguvu, hiki ndicho kilichofanywa na yale Mapinduzi Matukufu ya 1964!.

Anayekuja pasi na hodi, huondoka pasi kuaga!.

Pasco
 
Pasco Waarabu hawakuja Afrika, Waarabu asili yao ni Afrika.

Inasikitisha sana kuona kuwa historia iliyowajaza ujinga ikisema Waarabu wamekuja Afrika.

Kwanza kabisa ningependa ufahamu kuwa Uarabu si kabila wala rangi, Uarabu simply ni lugha.

Waarabu wengi leo hii wako Afrika, lugha ya kwanza kuongewa na wengi Afrika ni Kiarabu na haijawahi kuwa vinginevyo, jana , juzi , majuzi, rudi nyuma miaka mia, elfu, maelfu upendavyo utakuta ni hayo hayo. Utapofikia katika usomi wako ukakuta "wamekuja" nioneshe nami nipaelewe.

Tatizo kubwa sana linakuja pale mnapoamini, kwa ujinga tu, kuwa Uarabu ni tabaka la kabila au rangi ya watu fulani. La hasha, huko ni kule mimi nnapokuita kusomea ujinga.

Historia yoyote ile uipendayo, haioneshi na haitoweza kuonesha Mwarabu Afrika alikuja lini kwanza, isipokuwa kuna dhanna tu ya "tarikh" historia inayoonesha Mwaarabu alikutwa lini Afrika, jee na nani? na kwanini akutwe? Fikiri.

Unaanza kuponda "itroduction" iliyowekwa hapa kabla hujakisoma kitabu, jee, ni kwa jina tu la aliyetunga kitabu?

Unataka kutuaminisha kuwa "sixth sense" yako yakufikirika ina maana zaidi ya kitabu ambacho hujakisoma?
 
Kasome historia ya makaburi wa Afrika ya kusini, halafu leo atokee kaburu mmoja, aandike historia kuwa Afrika Kusini japo wao ni wahamiaji, walipofika hawakukuta mtu, na hao Wabantu nao pia ni wahamiaji tuu kama wao! hivyo wote wako sawa!.

Hiki kitabu kinataka kueleza uongo kuwa eti Waarabu walihamia Pwani ya Afrika ya Mashariki karine ya 16 BC hawakukuta wenyeji wowote, kwa sababu muda huo ndio huo huo Wabantu walihamia Afrika, ili kujenga hoja kuwa Waarabu Afrika Mashariki ni kwao kama ilivyo kwa Wabantu!. Kama Waarabu walihamia na Wabantu pia walihamia!, hivyo Bara la Afrika Waarabu walipohamia walilikuta tupu kabisa halina wenyewe!.

Wazungu walipokuja angalau walikuwa na ustaarabu fulani wa recognition ya waliowakuta, hivyo hawakujichukulia tuu maeneo kama wameokota!, waliyanunuatoka kwa wenyeji waliowakuta!. Tumesoma historia ya Karl Peters na ile mikataba yake na Sultani wa Msovero, japo ni ya kitapeli, lakini ni mikataba!.

Tumesema jinsi Hassan Bin Amiri alivyokinunua kisiwa cha Kilwa toka kwa wenyeji na kukilipia kwa kitambaa kinachozunguka kisiwa kizima!.

Huyu Mwarabu wa Zanzibar, alipokuja ile juzi juzi tuu, aliingia mkataba na nanni wa kuvimiliki hivyo visiwa?!. Yaani kwa kifupi alivitwaa tuu kama vile ameviokota!, hivyo lugha rasmi ni alivivamia na kwa kawaida mvamizi huingia kwa nguvu na mwisho wake hufurushwa kwa nguvu, hiki ndicho kilichofanywa na yale Mapinduzi Matukufu ya 1964!.

Anayekuja pasi na hodi, huondoka pasi kuaga!.

Pasco

Hapa hapa hata muda haujapita umeshabadili maandiko? ni wapi umeyasoma hayo uliyoyaandika, niliyokuwekea nyekundu? au kutoka kwenye "sixth sense" yako?

Inasikitisha sana.
 
Mdau...nadhan tatizo ni neno msikitini....lakin kikwel kabsa ni maduka ya vitabu yaliyoko karibu na msikiti....hiii haimananishii ni ndani ya msikiti. Either way...kuna vitabu vingi ambavyo vinapatikana katika aina flan.ya maduka na si mengineyo
...hii inaweza kuwa ni kwa sabb za kiitikadi au kukipinga aina flan ya vitabu...mfano...kitabu kama keys of this blood japo kimeandikwa na mtumishi wa miaka mingi wa vatikan...huwez kikuta hiki kitabu kwenye maduka mengi ya kanisa...so nadhan hofu yako isikufunge sana kuyaendea maduka yaliyoko misikitin....after all si mahali hatari sana kama inavofanywa kuonekana....just a thought...!

Walioua pale garissa zaidi ya wanafunzi 150 walitokea msikitini ! Na waliwaua wakristo pekee......
 
Hapa hapa hata muda haujapita umeshabadili maandiko? ni wapi umeyasoma hayo uliyoyaandika, niliyokuwekea nyekundu? au kutoka kwenye "sixth sense" yako?

Inasikitisha sana.
Mlango wa Kwanza unahusu "Taarikh ya Kuwasili Kwa Wabantu, Washirazi na Waarabu Pwani ya Afrikaya Mashariki." Hapa anaeleza kwa ushahidi wa taarikh usiokatalika kwamba Waarabu wamefika Pwani ya Afrika Mashariki maelfu ya miaka iliopita na Wabantu wamefika pwani hiyo katika karne ya 16 B.K. Makusudio ya mlango huu ni kuonesha kwamba Waarabu si wageni bali ni wenyeji wenye haki hapa sawasasa na wenyeji wengineo.
Yaani Mwarabu ametangulia Afrika ya Mashariki maelfu ya miaka iliyopita na Wabantu ndio wakaja ile karne ya 16 B.K akimaanisha ndio waliowakuta Waarabu!. Hili ni chapisho la spin doctor kutaka kutuamini kuwa Waarabu hapa ndio kwao, na Wabantu ndio wamewakuta!!. Kwa Waarabu sio wageni bali ni wenyeji wenye haki sawasawa na wenyeji wengine!. OMG!.
Katika hatua hii, jambo zuri la pekee kwangu mimi katika kitabu hiki ni kule tuu kutambua kuwa miaka ya zamani inatambulishwa properly 16 B.K na kwa herufu kubwa, kumaanisha miaka hiyo meanza kuhesabiwa kwa reference ya Kristu!.

Pasco

Back
Top Bottom