Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Mkuu xiexie, asante, nitaufuata ushauri wako.Mkuu, unajuwa ili uweze kuingiza idea mpya kichwani mwako ni MUHIMU kufanya ubongo wako uko BLANK ili kuruhusu mawazo mapya kuingia na kuchakata kile ambacho kilikuwepo kabla kisha baadae ndio uamue kipi ni kipi. Sasa wewe unaposema mwandishi amesema urongo kuanzia sura ya kwanza ni kwamba unashikilia msimamo wa kile ambacho ulikijua kabla ya kusoma alichoandika mwandishi.
Nikushauri tu, uwe na tabia ya kisomi tena usomi wa kutafuta ukweli: soma kwanza alichokiandika mwandishi ukiwa na blank mind, usiwe tayari na mtizamo hasi, HUTAELEWA. Hata mimi ni mwanahistoria na nimesoma THE PEOPLING OF EAST AFRICA na pengine tulichofundishwa wengi ndicho hicho unachokijua wewe ,lakini LET THE FACT SPEAK FOR ITSELF , tusome mtazamo wa mwandishi kisha tulinganishe kile tunachokijua, halafu ndio tufikie hitimisho. SI KILA WAKATI TULICHOFUNDISHWA VYUONI NI SAHIHI. Tusikaririshwe, tuwe wasomi wa kuchambua mambo.
Ntakupa mfano: kwa miaka mingi sana, tumekuwa tukifundishwa vyuoni kuwa FANI NA MAUDHUI HAVIWEZI KUTENGANISHWA, huu ni mtizamo ambao ulikubalika na wasomi nguli kama kina prof. SENKORO (Kasome kitabu cha FASIHI alichoandika), lakini ni huyu huyu Prof baada ya miaka na mikaka kupita SASA HIVI ANAYAKANA MAANDISHI NA MTIZAMO WAKE WA ZAMANI na ANAKUBALI kuwa fani na maudhui ni vitu vinavyoweza kutenganishwa akitolea mfano wa nyimbo za kubembelezea watoto hasa katika jamii zinazofuata mfumo wa kibaba
Pasco