Kitabu kipya: Tanzania na propaganda za udini na prof. Ibrahim Noor

Kitabu kipya: Tanzania na propaganda za udini na prof. Ibrahim Noor

Ukiona kilasiku unaungwa mkono na kundi la walewale ulowabraish ujuwe mjinga tu Wewe.

Mpumbavu mwezio ambaye kwake udini ni sera na kila kitu anasahihisha makosa ya speling kichwan umemjaza ujinga na upumbavu kila unapokanyaga nayeye huyo kafika kukusapoti na kuturekibisha uchapaji nakutetea lolote mjinga wewe unaandika.

Wewe kazi yako kupeperusha madai ya udini muda wote unadhani Taifa hili kila mmoja akifanya madai tutaishi? Jifunze kuvumilia, faham kwamba kila mmoja wetu anamadai mjinga wewe.

Wakristu wakifanya kama wewe zezeta watadai yafutayo
-shule zao zamsingi na sekondari
-hospitali zao
-Ardhi zao nk
Vyote hivyo Nyerere aliwapokonya kwafaida yako, mimi na wengine.

Wasambaa watadai milima ya usambaa

Wachaga watadai mlima kilimanjaro

Budha watasema hapa kuchinja ng'ombe maana ni Mungu wao

Wapagani watapinga uapishwaji kwa kutumia biblia na kuruwan

Kila mmoja anamadai kwa ushenzi wako unachochea ilituvurugane, tuuwane alafu utapata nin wewe mtumwa wa chuki na ubaguzi wakidin?

Unataka ushahidi wakitugan yaani imefikia huna Akili kufaham unafanya nini na historia zako?

Mim naamin kabisa utasumbuka mpaka utakufa utaiacha Tanzania nawatanzani wote kwa ujumla wao (waislam,wakristu, iman zingine nawasioamin) wakiwa salama.

Mungu atakuadhibu maana hawezi acha ukafanya uchochezi kiasi hiki damu za watu wasio nahatia zikamwagika.

Adolay,
Unazidi kupandwa na hamaki na unazidisha matusi.

Narejea pale tulipoanzia mimi na wewe kuwa lete ushahidi wa tuhuma zako
hapa Majlis watu wazione.

Historia hizi si zangu.

Historia hizi ni historia za Afrika na ndiyo maana nikachapwa na Oxford University
Press, New York Dictionary of African Biography.

Historia hizi ni za Afrika ndiyo maana Northwestern University, Chicago
mabingwa wa historia ya Afrika dunia nzima wakanialika chuoni kwao nifanye
mnakasha na wao.

Mungu anaadhibu watu kwa dhambi haadhibu watu kwa kusoma na kusomesha
ilm yenye manufaa.

Damu haiwezi kumwagika kwa kusasahihisha historia iliyokosewa.
Huu mwaka wa 17 toka kitabu cha Abdul Sykes kilipochapwa Uingereza.

Haijawa lolote ila tumekwenda matoleo mawili kitabu cha Kiingereza na toleo
la tatu kitabu cha Kiswahili na kitabu kimejaa madukani tele kinasomwa.

Toleo la nne Kiswahili lipo njiani.
Narudia tena usijitishe bure wala huna sababu ya kuwatisha watu wengine.

Sasa nakuchukua kwa Maalim Faiza.
Mimi nimeliona hilo kosa lakini kwa kukuhurumia nimeliacha.

FaizaFoxy anakusahihisha saa saba mchana ili ujiangalie na upime uwezo wako
kama kweli wewe una makamu ya kupambana na watu katika mnakasha kama
huu.

Unajikwaa kwa kuwa kifua chako kinatokota kwa chuki na chuki huondoa umakini.
 
kwahiyo prof pamoja na taaluma yake bado anaamini katika jihad ?

Hivi wewe hauamini katika jihad? Jihad ni kufanya jitihada katika chochote ukifanyacho.

Hivi huna jitihada yoyote uifanyao katika maisha yako? au umeaminishwa kuwa jihad ni nini?
 
adolay;

Unazidi kupandwa na hamaki na unazidisha matusi.

Narejea pale tulipoanzia mimi na wewe kuwa lete ushahidi wa tuhuma zako
hapa Majlis watu wazione.

Historia hizi si zangu.

Historia hizi ni historia za Afrika na ndiyo maana nikachapwa na Oxford University
Press, New York Dictionary of African Biography.

Historia hizi ni za Afrika ndiyo maana Northwestern University, Chicago
mabingwa wa historia ya Afrika dunia nzima wakanialika chuoni kwao nifanye
mnakasha na wao.

Mungu anaadhibu watu kwa dhambi haadhibu watu kwa kusoma na kusomesha
ilm yenye manufaa.

Damu haiwezi kumwagika kwa kusasahihisha historia iliyokosewa.
Huu mwaka wa 17 toka kitabu cha Abdul Sykes kilipochapwa Uingereza.

Haijawa lolote ila tumekwenda matoleo mawili kitabu cha Kiingereza na toleo
la tatu kitabu cha Kiswahili na kitabu kimejaa madukani tele kinasomwa.

Toleo la nne Kiswahili lipo njiani.
Narudia tena usijitishe bure wala huna sababu ya kuwatisha watu wengine.

Sasa nakuchukua kwa Maalim Faiza.
Mimi nimeliona hilo kosa lakini kwa kukuhurumia nimeliacha.

FaizaFoxy anakusahihisha saa saba mchana ili ujiangalie na upime uwezo wako
kama kweli wewe una makamu ya kupambana na watu katika mnakasha kama
huu.

Unajikwaa kwa kuwa kifua chako kinatokota kwa chuki na chuki huondoa umakini.
 
Last edited by a moderator:
Sasa wewe ni mbaya zaidi kufikiria mambo hata hujakisoma kitabu na kuanza chokochoko, sioni kama kinauzwa misikitini ni duka lililo nje ya msikiti, na misikitini sio sehemu ya kufanya biashara ni sehemu ya ibada.

Masomo bookshop ni mbali kabisa na msikiti. kwanini una chuki zilizowaziwazi na uislam?
binaadamu hatakiwi kuwa hivyo lol
PTER

SeliSelina,
Ungemfahamisha kuwa kuna Cathedral Bookshop pale St. Joseph's Cathedral, Dar es Salaam.
Hapo hapo pia kuna Mkombozi Bank na vyote viko ndani ya uwanja wa Kanisa.
 
Hicho kitabu ni propaganda tu! Hakuna jipya hapo
Shadowalker,
Je ushakisoma hicho kitabu utupe maudhui yake?
Inapendeza mtu kujadili kitu ambacho unakifahamu.

Yapo mengi sana katika kitabu hicho na yenye manufaa katika jamii.
Kisome utafaidika.

Hebu soma utangulizi huu Prof. Noor amavyotuingiza katika chombo
chake tuanze safari:

"Tokea utotoni mwangu nilikuwa nikipenda sana kuwasikiliza waliokuwa mahodari wa kuchezea lugha nilizozifahamu. Walumbi hawa waliniweka mdomo wazi kila nilipowasikia wakitumia ubingwa wao wa lugha khasa katika kuelezea au kujadili jambo. Nilipovuta umri na kuwa kijana, shauku hii niliyokuwa nayo ilinifanya nihudhurie mikutano mingi ya kisiasa ya vyama vyote tokea zilipoanza siasa za viyama vingi Zanzibar mnamo mwaka wa 1957. Kwa jumla, wasemaji wakuu wa vyama hivyo walikuwa wengi lakini wachache wao ndiwo waliokuwa na kipawa cha kupigiwa mfano kwa umalenga waliokuwa nao. Baadhi ya walumbi hawa walikuwa hata kusoma hawajui lakini ufasaha wao wa kusema ulikuwa wa kupigiwa mfano na walipokuwa wakikhubiri nilikuwa nikisisimkwa na mwili na kuchemkwa na akili kwa uhodari wao mkubwa sana wa kuichezea lugha na kuweza kuchezea akili za wafuasi wao na kuweza kuwapeleka wengi kule watakako hawa wanasiasa.

Siku moja katika mwaka wa 1960 Mzee Abedi Amani Karume alikuwa akikhubiri katika kiwanja kilioko karibu na Kanisa la Anglikana, maarufu kwa jila na "Kwa Kimoto," kiwanja kilichopeewa jina la jina la "Kwa Khamisi Machungwa." Mimi nilikuwa nimesimama upande wa pili wa barabara, upande wa Kisiwandui, huku nimeishika baiskeli yangu. Maudhui aliyoyazungumzia Mzee karume siku hiyo yalikuwa juu ya biashara ya utumwa iliyofanywa katika karne iliyopita..."

Wanamajlis,
Simulizi inayoendelea hamjapatapo kuisoma wala kusikia popote katika historia ya Zanzibar.

Kila ninapopindua ukurasa katika kitabu hiki na kuyasoma mengi ambayo sikuwa nayajua kamwe
yananijia maneno ya Prof. Mohamed Bakari aliposema:

"Tuandike historia yetu sisi wenyewe na endapo tutawaachia watu wengine watuandikie wataandika
mambo ambayo sisi hatutayapenda."

Prof. Noor katika kitabu hiki chake amesahihisha uongo ulioingizwa na wakoloni katika historia yetu kwa
nia ya kutugawa na kutufitinisha ili tutawalike vizuri.

Kitabu hiki ni muhimu tukakisoma.

2015%2B-%2B1


Kushoto: Prof. Mohamed Bakari na mwandishi ofisini kwake Fatih University Istanbul, Turkey
 
Page namba ngapi? weka nukuu.

1. Mlango wa Kwanza unahusu
“Taarikh ya Kuwasili Kwa
Wabantu, Washirazi na
Waarabu Pwani ya Afrikaya
Mashariki. ” Hapa anaeleza
kwa ushahidi wa taarikh
usiokatalika kwamba Waarabu
wamefika Pwani ya Afrika
Mashariki maelfu ya miaka
iliopita na Wabantu wamefika
pwani hiyo katika karne ya 16
B.K. Makusudio ya mlango
huu ni kuonesha kwamba
Waarabu si wageni bali ni
wenyeji wenye haki hapa
sawasasa na wenyeji
wengineo.
2. Mlango wa Pili unazungumzia
“Propaganda za Siasa za
Chuki na Athari Zake .”Humo
tunaona uovu wa propaganda
za udini zilizowatuhumu
Waarabu na Waswahili
Waislamu peke yao kukamata,
kuuza na kumiliki watumwa.
Propaganda hizo zimepelekea
kuuliwa maelfu ya Waislamu
bure bila ya sababu
ilipovamiwa Zanzibar, nchi
yenye Waislamu wengi, na
kumezwa na Tanganyika 1964.
 
Yote Ni malalamiko tu na kutafuta sympathy kwa watu flani, which is not wise. No offense sir, but I expected a professor to be more intelligent and concerned about the wellbeing of his country......not spreading some BS like you just did
Please use your education in some more productive things like let's say spreading Tanzanian culture and Language to other nations etc etc utakua umefanya jambo la maana sana.
What you are trying to do is unataka kufanya baadhi ya raia wawe na inferiority complex, which is very bad & it can lead to violence....... I hope u understood me sir
 
kbosho;

Sasa hapo wapi anahalalisha chochote kile?

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?

Wewe tueleze Waarabu walikuja lini pwani ya Afrka Mashariki badala ya kuleta porojo. Ukimaliza, utueleze kuhusu wa Iraqw.
 
Last edited by a moderator:
The problem is hiyo historia mnayotaka kuandika Iko too biased na inaonyesha kwamba huyo prof ana agenda zake ambazo zinaweza zikaleta uvunjifu wa amani
 
The problem is hiyo historia mnayotaka kuandika Iko too biased na inaonyesha kwamba huyo prof ana agenda zake ambazo zinaweza zikaleta uvunjifu wa amani

Umeshasoma kitabu kinachoongelewa hapa au ndiyo upo katika kujijaza ujinga tu? au jina tu limekutisha?

Historia ya mzungu ndiyo haipo biased? au ile ya kivukoni?
 
Mohamed Said;

Hakuna haja ya kutoa droo na kanisa, hoja yangu ni kuwa kuuza katika maduka yaliyo na uhusiano na Misikiti kunaanza kuleta picha tofauti kwa watu ambao wanataka kusoma hicho kitabu.

Nadhani umenielewa!
 
Last edited by a moderator:
MR UNINFORMED;

Nimekuelewa, mimi naelewa hilo mkuu.

Lakini kila Mtanzania ni muelewa wa kiwango hicho? Mimi ni Mwafrika kwa imani yangu lakini huwa naenda kupata maakuli jirani na msikiti wa Kiblatan, sina shida na misikiti wala watu wake, ila nahofia akili za Watanzania ambao tayari zimeshaathirika na Ukristu vs Uislamu.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu PTER, naomba kutofautiana na wewe, kwa sisi watu wa kutafuta maarifa na kupata ufahamu, kila kinachoandikwa is worth reading, ndio maana kina sisi tumesoma hadi Kuruani na kuidismiss, vivyo hivyo wanazuoni wa Kiislamu wamesoma Biblia na kuidismiss!. Nawashauri wale schollars wetu wa humu, tukisome kitabu kisha ndipo turudi humu with facts.

Mwanzo tuu niliisha smell hiki kitabu is a problem, namna ya ku deal na problem is facing the problem, not running away from the problem, hivyo nashauri tukisome ndipo kisha tuje humu kukibonda!.

Pasco
much obliged your honour.
 
Mphamvu,
Ibn Hazim Media Centre haina uhusiano wowote na Msikiti.

Ungekuwapo upo ningekueleza kwani si kosa kwa msikiti kuwa na
biashara.

Kuhusu "picha" kwa wasomaji wa kitabu hiki...mimi hununua vitabu
nivipendavyo Cathedral Bookshop na Dar es Salaam Bookshop na
haya yote ni maduka Kanisa.

Nimekuwa mteja wa maduka haya toka niko mtoto hadi leo
nimekuwa mzee.

Nadhani umenielewa!
 
Waarabu ni Waarabu kwa kuwa wanaongea Kiarabu. Simpo, si rangi, si taifa, si kabila, ni kama kusema "gypsies".

Maana ya Arabiya ni "Caravan" au msafara, hawa walikuwa ni watu wa misafara toka enzi na enzi na lugha yao ndiyo hicho Kiarabu, ndiyo maana kikazagaa sana Mashariki ya kati na barani Afrika, Magharibi ya Asia walienda tu kwa kuwa kulikuwa hakuna kizuizi cha kuwafikisha huko. Kumbuka kuwa mpaka wa asili wa makotinenti ni bahari, na baina ya Afrika na Asia Mashariki kulikuwa hakuna mpaka wa bahari mpaka juzi jzui tu ulipochombwa mfereji wa Suez.

Waarabu Afrika na Asia Mashariki hawakuja kama wazungu, Waarabu kwingine ndiyo walikwenda, Afrika na Asia ni "wondering ground" ya misafara "Arabiya" (from time immemorial).

Kwa maana hiyo Waarabu /Msafara sijui wa Mapunda ulifika mpaka Africa-sasa sijui walitoka kunakoitwa Uarabuni kwa sasa sijui.
Ila tukubaliane wote hao Wazungu na Wasafiri/Waarabu waliwachukua Waafrika kama watumwa.
Na mbaya zaidi inaonekana kwamba hawa Wasafiri mwisho wa Siku waliwachinja Waafrika waliokuwa mateka wao maana hakuna masalia hata mmoja inayoishi bega kwa bega na Waarabu hawa na haya ndiyo yalifaa hawa the so called Maprofesa kututafutia majibu hata ya kinadharia tu.

Endeleeni na propaganda zenu mwisho wa siku mtamchomoa nyoka Pangoni.
 
Haaa haaa Mohamed Said asipoutukuza uarabu basi atajibanza kwenye uislam ambao umeletwa na hao waarabu wavamizi afadhali umemwelewa mapema na hizo ajenda zake za hovyo.


[/B][/B]Mkuu Maalim , kwanza asante kutupatia taarifa hizi, sisi wapenzi wa kusoma vitabu, tutakinunua na kukisoma hiki kitabu cha Tanzania na Propaganda za Udini, ila hata kabla sijakinunua na kukisoma, kiukweli kabisa toka ndani ya nafsi yangu, the sixth sense inanieleza the 'motive behind' mwandishi wa kitabu hiki, Prof. Ibrahim Noor Shariff, ni 'ill motive!'. Tangu Mlango wake wa Kwanza unaohusu “Taarikh ya Kuwasili Kwa Wabantu, Washirazi na Waarabu Pwani ya Afrikaya Mashariki.” ameanza na maurongo yaliyokubuhu!, hapa anadanyanya wazi mchana kweupe kwa maushahidi yake ya uongo kwamba eti Waarabu wamefika Pwani ya Afrika Mashariki maelfu ya miaka iliopita kabla ya Wabantu, tangu karne ya 16 B.K!. The ill motive ya mlango huu ni kuonesha kwamba Waarabu si wageni bali ni wenyeji wenye haki hapa sawasasa kwenye Pwani ya Afrika Mashariki sawa na wenyeji wengineo.

Yaani hapa huyu Mwarabu, anataka kuwafanyia Afrikanization hawa wavanizi wa Kiarabu ili kuwahalaliasha eti na wao, ni wenyenyeji halali wa Afrika Mashariki, na wakati huo huo, kuwaondolea Wabantu, uenyeji wao wa asili, kwa kuonyesha kuwa hata hao Wabantu, Afrika ya Mashariki sio kwao asili bali nao pia ni wahamiaji tuu kama Waarabu!. Huu ni uongo uliokubuhu wa mchana kweupe!.

Lengo ni kuzuia kinachoweza kuja kuwapata Waarabu wa Afrika Mashariki na sana sana Waarabu wa Zanzibar ambao wametoka kwao Omani juzi juzi tuu mwaka 1832 wakiongozwa na Sultan Seyyed Said aliye yahamisha makao yake makuu toka Oman hadi Zanzibar!. Huyu sio tuu ni mvamizi bali pia ndiye mporaji mkuu, aliyejitwalia visiwa hivyo kama ameviokota as if hakumkuta mtu yoyote ili hali wenyeji walikuwepo!. Siku ile ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar, siungi mkono mauaji yoyote ya Waarabu, bali wangeambiwa tuu kistaarabu, wafungeshe kilicho chao, wao na wazalio wao, wajirudie kwao Omani walikotoka na kutuachia visiwa vyetu!.

Hili swali la Waarabu wamekujaje Pwani ya Afrika Mashariki, litakuja kurudi tuu mbele ya safari hivyo ushauri wangu, ni kujituliza tuu na kuishi kwa unyenyekevu wa hali ya juu sana kwa kujihesabu wanaishi hapo kwa hisani tuu, vinginevyo watatimuliwa warudi kwao Oman walikotoka, wao na vizalia vyao!.

Hizi historia za kutunga tunga kutaka kuwahalalisha madhalimu hawa waliowauza mababu zetu kama bidhaa!, hazitasaidia kitu!, no wonder kila siku wanashinda uchaguzi lakini kamwe hawatakabidhiwa nchi, na 2015 watashinda tena na moto ni ule ule!. Mwarabu atoke kwao, aje akutawale, babu zako awauze, kisha mumpindue halafu leo mumrudishe eti kisa amechaguliwa!, hii haitakaa itokee!.

Kesho ni sikukukuu ya Muungano, tutakukumbusheni hiyo Zanzibar ilikuwa ni sehemu ya Tanganyika, hivyo huu muungano ni wa milele.

As long as hii ni lilterally work, ngoja nikitafute na kukisoma halafu turudi humu kumwaga mbichi na mbivu!, ila kiukweli lazima hata mtoto wa darasa la 4 akiisikia hii acheke, ati Waarabu nao kwao ni Afrika Mashariki, na Wabantu nao pia ni wageni!. OMG!.

Pasco
 
Last edited by a moderator:
Mphamvu,
Unajitisha pasi na sababu.
Huko kula karibu na Quiblatein hukuanza wewe hii leo watu wa dini
tofauti wameishi mtaa huo miaka na miaka.

Huo msikiti mlango wake umeelekezana na mlango wa nyumba ya
marehemu Mzee Khube.

Karibu na hapo ilikuwa ofisi ya Tanganyika Federation of Labour (TFL).
Hapo ni Mtaa wa Aggrey na Sikukuu kuna nyumba ya bibi yangu na
nyumba ya marehemu Mzee Maleta.

Nyumba ya Mzee Maleta iko ubavu na nyumba ya Abdul Sykes sasa
hivi ni office block ya gorofa tano.

Hapo ndipo palipokuwa "main station" ya harakati za kupigania uhuru
ukitoa ofisi ya TANU New Street.

Mbele kwenye kona ya Mtaa wa Swahili ilikuwa nyumba ya Tewa Said
Tewa mmoja kati ya wale wazalendo 17 walioasisi TANU na jirani ya
nyumba ya Tewa Said Tewa kuna nyumba ya Mzee Ramadhani Fundikira.

Sasa wewe kula kwako mitaa hiyo si chochote kwangu mimi.
Nadhani umenifahamu.
 
Madafu,
Katika mambo ambayo mimi binafsi nimekutananayo na hakika yamenisikitisha
ni jinsi jamaa zetu walivyoathirika na propaganda.

Hicho kitabu wala si cha dini lakini kilichomkera ni hilo jina la mwandishi.
Kitabu hicho mathalan kingekuwa na jina la John Esposito asingejali.

Juu hayo ningependa ajue kuwa, "Islam," hivi sasa ni "Field of Enquiry,"
muhimu katika vyuo vingi sana hasa Marekani.

Aingie kwenye Google ataona mengi.

Kitabu changu kimepata umaarufu mkubwa sana katika vyuo vya Marekani
kwa kuwa nilikuja na, Islamic movement in nationalist politics ..." katika
Tanganyika ya 1950s.

Wenye akili daima husimama kutetea ukweli bila kutaja dini zao na kuziinua,nashawishika kusema hzo dini mnazokesha kuzitetea na kuandika maandiko kila kukicha hazina maana na hazitamkomboa mwanadamu kamwe.
Hakuna dini iliyoanzishwa na MUNGU ikalazimika kutetewa na mwanadamu anayeishia kufa,kimsingi hzo dini na watu wake wote wamepotoka na tusipoteze muda kuwaona wenye hekima zaidi ya pharao.
 
Wenye akili daima husimama kutetea ukweli bila kutaja dini zao na kuziinua,nashawishika kusema hzo dini mnazokesha kuzitetea na kuandika maandiko kila kukicha hazina maana na hazitamkomboa mwanadamu kamwe.
Hakuna dini iliyoanzishwa na MUNGU ikalazimika kutetewa na mwanadamu anayeishia kufa,kimsingi hzo dini na watu wake wote wamepotoka na tusipoteze muda kuwaona wenye hekima zaidi ya pharao.
Johnson Alex Otieno,
Siku zote binadamu tutapishana katika fikra.
Nimekusoma na nina heshimu mawazo yako.
 
Back
Top Bottom