Kitabu kipya: Tanzania na propaganda za udini na prof. Ibrahim Noor

Kitabu kipya: Tanzania na propaganda za udini na prof. Ibrahim Noor

Unautukuza sana uarabu ukitaka ushahdi pitia mabandiko yako vizuri utaona bila shida.Nadhani labda unamwomba Mungu akubadili ngozi nyeusi na nywele ngumu.

Ngongo,
Toa ushahidi hapa Majlis kuwa mimi natukuza Uarabu.
 
Ngongo,
Hili halina maana.
Tusijifunge hapa tusonge mbele na mnakasha.
 
Huko "South America" unaweza kupata tarehe yao walivyoanza safari ya kwenda huko.

Sasa nisome tena, unielewe:

Waarabu wengi leo hii wako Afrika, lugha ya kwanza kuongewa na wengi Afrika ni Kiarabu na haijawahi kuwa vinginevyo, jana , juzi , majuzi, rudi nyuma miaka mia, elfi, maelfu upendavyo utakuta ni hayo hayo. Utapofikia katika usomi wako ukakuta "wamekuja" nioneshe nami nipaelewe.

Basically, waarabu walianza kusettle kwa kiasi kikubwa Africa Kaskazini pale mtoto wa beki tatu Ismail alipotimuliwa pamoja na mamake..wakakimbilia maeneo ya Masri (Misri)
 
mimi sina chuki na uislam lakini maudhui ya mchambuzi yana akisi kuwa kitabu kinajenga dhana kuwa kunapropaganda katika elimu ambazo zinaminya uislam,

samahani sana kama nimegusa imani yako halikuwa lengo langu, pengine mchambuzi kaweka ya kwake ngoja nikakitafute nijisomee mwenyewe nimejaribu online hakipo

“Watu wema ni watu wema wawe wa dini yoyote na watu waovu ni waovu; wawe wa dini yoyote ile. Kama watu wema wenye kupendelea viumbe wenzao mema hawashikamani, basi waovu wenye kumfuata Shetani watashinda na watatawala.”

Ibrahim Noor Shariff
 
Nimekubali, andiko limeeleza kuwa Waarabu ndio waliotangulia kufika Pwani ya Afrika ya Mashariki, halafu Wabantu ndio wakaja ile karne ya 16, ikimaanisha ndio waliowakuta Waarabu!.

Admission "hawakukuta wenyeji wowote" ni my own insertion!.

Pasco

Pasco,
Nimepokea salaam zako kutoka kwa Prof. Ibrahim Noor.
Salaam ni hizi hapa chini zisome:

Siku zote, lengo kuu la propaganda ni kuzibaka akili za watu na kugandisha katika bongo zao yale wanayoyataka wana-propaganda; na wana propaganda hupendelea sana kuwapata watoto wakiwa wangali wadogo kuwajaza hizo propaganda zao ili hata wakiwa watu wazima uwe mgando huo umeshatapakaa kama kensa katioka bongo za walengwa ili zisiweze tena kuganduka. Hawakukosea wavyele wetu waliponena kuwa “udongo upatilize ungali umaji.”
Na vipi unaweza kumtambua mtu aliyelishwa propaganda kali, khasa za ubaguzi/ugozi na za udini? Kwanza utamwona ni mtu ambaye huwezi kumwambia lolote tafauti na zile sumu alizolishwa akalikubali, hata likiwa na ukweli na mantiki ya hali ya juu kabisa. Propaganda walizogandishwa bongoni mwao tokea utotoni huwafanya wajione wanajua kila kitu na wewe huelewi chochote! Wakati ni wao walioseelea na mtizamo finyu.

Mawazo ya mtu kama huyo hakika ni ya kusikitisha sana khasa kwa vile wengi wao, baada ya kuharibiwa akili zao shuleni, uwezo wao wa kufikiri kama bin Adam anavyotakiwa afikiri kwa kutumie akili yake ili kumtafautisha na mnyama, hupewa nafasi na wadhifa wa kuweza kuwaathiri watu wengi kwa fikra zao zilizojaa ubaguzi, kwani fikra zao hujikita katika ufinyu wa propaganda walizomiminiwa bongoni mwao tokea walipokuwa shuleni utotoni mwao na kuwafanya wakawa hawana haja ya kujua mengineyo ambayo huenda yakawatoa katika gereza la mawazo mgando waliyonayo; yaani, wametosheka na yale waliyosomeshwa shuleni hata yakiwa si ya kweli na yamejaa ubaguzi na udini na yana khatari kwa nchi. Kwa mfano, kiwango na mgando wa “ilimu” alionao Pasco umempelekea kuandika yafuatayo:

“Tangu Mlango wake wa Kwanza unaohusu “Taarikh ya Kuwasili Kwa Wabantu, Washirazi na Waarabu Pwani ya Afrikaya Mashariki.” ameanza na maurongo yaliyokubuhu!”

Anatuelezea haya hata kitabu hajakisoma! Lakini tusistaajabu, kwani, kama nilivyoeleza, hii ndio athari na lengo khasa la propaganda. Waliotekwa na propaganda hawahitajii kusoma chochote kwanza, wao wameshafanywa, kwa njia za kipropaganda, waamini tokea utotoni mwao fikra fulani, basi wametosheka nayo. Bila ya kuzisoma hoja na ushahidi uliotolewa kitabuni na bila ya yeye kututolea ushahidi wowote wenye kuonesha kuwa yaliyoelezewa kitabuni ni ya “maurongo yaliyokubuhu!” anatutaka tuzikubali kauli zake kama yeye alivyokubali kumiminiwa propaganda za udini na ubaguzi alipokuwa shuleni hata ikamfanya yeye binafsi, kuwa na chuki kubwa sana dhidi ya wale alioambiwa awachukie na kuwabagua. Soma barua yake kwa makini na utamuona vipi alivyotopea katika chuki na vipi yeye (na wengine kama yeye) alivyokuwa hahitajii kusoma kwanza kabla hajaamua kumshambulia mwandishi wa kitabu pamoja na anayodhania ameyaandika! Ni muhimu kwake binafsi kuendelea na fikra mgando za chuki kuliko kuutafuta ukweli na kuwa mtu huru kimawazo.

La kusikitisha pia ni kumwona mtu huyohuyo anajinata kuwa kasoma sana na anaelewa vya kutosha hadi kufika kuwa na “sixth sense.” Mahabusi wa propaganda, khasa zikiwa za udini na ubaguzi, hawezi kabisa kutumia akili yake na akili hiyo kumwongoza hadi kufikia uamuzi unaokubali ushahidi wowote wala hoja yoyote inayopingana ufinyu wa propaganda za ubaguzi na za udini alizojazwa nazo. Nakariri, propaganda haimruhusu hata kuwa na “comon sense” wacha kuwa na “sixth sense” kwani mtu huyo huwa kama kasuku anayerejelea yaleyale ya chuki alizojazwa nazo tokea utotoni mwake. Jinginelo lolote, hata likitolewa ushahidi gani, hawawezi kulikubali kwani propaganda huwaondoshea hata “common sense."

Sifa ya pili waliyonayo ni kuwa daima kiumbe kama huyo anataka kulazimisha tukubali tu yale anayoyaamini yeye. Kwa mfano, lazima iwe ni Wabantu ndio wenyeji asilia wa pwani ya Afrika Mashariki. Wala hana hamu ya kutaka kujua nini wameandika mabigwa wa taarikh ya uhamiaji wa Wabantu na lini wamewasili katika upwa huo, ingawa siku hizi huna haja ya kuvitafuta na kuvisoma vitabu vya mabingwa wenye kuijua taarikh ya Afrika. Fungua hata mitandao na uangalie wajuzi wanatuelezea nini kukhusu uhamiaji wa Wabantu na khasa wapi walipotokea. Hakuna hata mmoja katika mabingwa hao anayedai kuwa Wabantu walitokea Afrika Mashariki na kuelekea Afrika Magharibi. Wote wanatuelezea kuwa ama wametoka Afrika Kati na kuelekea mashariki na Kusini, au wametokea Afrika Magharibi na kuelekea Mashariki na Kusini, na mabingwa wenye kusema haya ndio wengi zaidi. Fungua mtandao uandike “Bantu Migration” ujionee mwenyewe kwa maneno na kwa ramani kukhusu uhamiaji wao Wabantu. Lakini, kama nilivyosema kabla, waliolishwa vidonge vya sumu ya propaganda za udini na ubaguzi hawawezi kukubali lolote hata likiwa na ukweli wa aina gani ila propaganda ile ile waliosomeshwa tokea utototoni. Inasikitisha kushuhudia namna na kadiri ya vidonge vya sumu na chuki zilivyofanya kazi ya kuharibu akili za watoto wetu katika kuwasomesha historia.

Jambo linalomuuma zaidi ni kwanini Waarabu waweze kuwa wenyeji wa pwani ya Afrika Mashariki; hawezi kukubali Mwarabu awe raia wa Tanzania wa daraja ile ile moja sawa na Mbantu na Mtanzania yoyote yule. La! Hasha. Wao walivyokuwa wabaguzi kweli, wanataka pawe na matabaka ya uraia. Angalia mfano wa manenno yake mwenyewe:
“Yaani hapa huyu Mwarabu, anataka kuwafanyia Afrikanization hawa wavamizi wa Kiarabu ili kuwahalalisha eti na wao, ni wenyenyeji halali wa Afrika Mashariki…”

Angalia na mfano mwingine wa ugozi wake:

“Lengo ni kuzuia kinachoweza kuja kuwapata Waarabu wa Afrika Mashariki na sana sana Waarabu wa Zanzibar ambao wametoka kwao Omani juzi juzi tuu mwaka 1832 wakiongozwa na Sultan Sayyid Said aliye yahamisha makao yake makuu toka Oman hadi Zanzibar! Huyu sio tuu ni mvamizi bali pia ndiye mporaji mkuu, aliyejitwalia visiwa hivyo kama ameviokota as if hakumkuta mtu yoyote ili hali wenyeji walikuwepo! Siku ile ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar, siungi mkono mauaji yoyote ya Waarabu, bali wangeambiwa tuu kistaarabu, wafungashe kilicho chao, wao na wazalio wao, wajirudie kwao Omani walikotoka na kutuachia visiwa vyetu!.”

Yaani huyu mbaguzi kutoka Bara ambaye Zanzibar si kwao hata chembe anafika kusema kwa ujeuri kabisa na kwa kinywa kipana kuwa mwenye asili ya Kiarabu hata akiwa ni wa kizazi cha ngapi hapo Zanzibar asiwe na haki yoyote ya uraia na uananchi, bali yeye Pasco mzalia na mkaazi wa Bara ana haki zaidi na kamili Zanzibar kuliko huyo Mzanzibari! Kama maneno haya ya Pasco na wenziwe kama Wahishimiwa akina Lukuvi na Sitta si onyo kubwa sana kwa Wazanzibari kukhusu nia zao na lengo lao hawa Wabara wenye chuki dhidi ya Wazanzibari, basi Wazanzibari endeleeni kulala mkione cha mtema kuni. Ishara zote za ubaguzi wao ziko wazi kabisa, na mwenye macho haambiwi “tazama.”

Waarabu wengi, na wengi walikuwa watu wa kawaida tu na wengine walikuwa mafakiri, waliuwawa kwa ghadhabu kubwa sana na wabara kama hawa, kwa bunduki, mapanga na mashoka kama nguruwe mwitu, ikisha anatuambia kuwa yalikuwa “Mapinduzi matukufu.” Yatakuwaje matukufu na ilihali roho za raia wengi sana ziliteketezwa na wavamizi kutoka Tanganyika ambao tumewashuhudia kwa macho yetu na kuwasikia kwa lafdhi zao za kibara wakipita mitaani mwetu na kunadi: “Arabu uwa, Muhindi uwa Muzungu siguse.” Utukufu ni sifa ya Mwenye-enzi Mungu. Mauwaji ya halaiki ya raia na uraruwaji wa wanawake, ufungwaji wa wengi bila ya sababu, unyanyasaji, unyang’anyi wa mali za raia, uadhibishwaji wa watu waliokuwa hawana kosa lolote ila kuwa hawakubaliani na siasa za Karume na Kambarage, zinakhusiana nini na “utukufu”? Nini kilichotukuka katika kutenda maovu haya yaliyokatazwa na Mwenye-enzi Mungu Mtukufu?

Pasco anendelea na haya yafuatayo:

“Prof. Ibrahim Noor Shariff, ni 'ill motive!' Tangu Mlango wake wa Kwanza unaohusu “Taarikh ya Kuwasili Kwa Wabantu, Washirazi na Waarabu Pwani ya Afrikaya Mashariki,” ameanza na maurongo yaliyokubuhu!, hapa anadanganya wazi mchana kweupe kwa maushahidi yake ya uongo kwamba eti Waarabu wamefika Pwani ya Afrika Mashariki maelfu ya miaka iliopita kabla ya Wabantu, tangu karne ya 16 B.K! The ill motive ya mlango huu ni kuonesha kwamba Waarabu si wageni bali ni wenyeji wenye haki hapa sawasasa kwenye Pwani ya Afrika Mashariki sawa na wenyeji wengineo.”
Kwanza anaanza kwa kunishambulia binafsi kwa dhana zake mwenyewe wala si kwa hoja nilizozitoa alipoandika kuwa mimi “ni 'ill motive!'” Tukiacha na Kiingereza chake chenye makosa, suala ni: amejuaje kama mimi nina sifa mbovu hiyo? Kitabu hajakisoma alau akadai kuwa amenisoma vizuri kabla hajautoa uamuzi wake huo, maajabu haya! Aliyekuwa "ill-motivated" ni nani hapa!

Anaonesha wazi kuwa taarikh ya Waarabu haijui zaidi ya hiyo aliyosomeshwa shuleni iliyojazwa chuki ndani yake. Hajui kabisa kuwa Waarabu ni watu walioanza kusafiria Bahari ya Hindi miaka elfu nyingi kabla, na walielewa taratibu za pepo za Musim na kufikia nchi zote ziliko pwanipwani ya Bahari ya Hindi. Haelewi kuwa taarikh ya Bara Arabu na nchi za Afrika kama Habash/Ethiopia zimefungamana kwa zaidi ya miaka elfu kumi. Taarikh kama hiyo haingii katika hisabu za akili yake! Kama sabini katika mia ya Waarabu wanaasili ya Afrika na wanaishi Afrika kama ni wenyeji makwao kutoka Sudan hadi Moroko.

Haelewi pia kuwa Waarabu wengi ni Wasemiti, na jamaa zao wako kutoka nchi za Ghuba hadi Nigeria. Kuwa Wahausa wa Afrika Magharibi ni katika jamaa zao Waarabu, na Waethiopia ni jamaa zao wa karibu sana, na hawa wote wako mbali kabisa kiujamaa na Wabantu. Afrika haina watu wa asili moja tu. Kuna makundi mengi mbalimbali ambayo Waingereza huita “race.” Nikupe mfano mmoja utakaokufanya ufikiri. Unadhani Wabaka (mbilikimo) na Watutsi wana asili moja kwa sababu rangi za ngozi zao zimekoza?

Barua yake yote Pasco ni mfano dhahiri kabisa wa mtu aliyefunzwa propaganda za udini na chuki zilizotopea khasa dhidi ya wenye asili ya Kiarabu. Soma na haya aliyoyaandika kwa kifua mbele:

“Hili swali la Waarabu wamekujaje Pwani ya Afrika Mashariki, litakuja kurudi tuu mbele ya safari hivyo ushauri wangu, ni kujituliza tuu na kuishi kwa unyenyekevu wa hali ya juu sana kwa kujihesabu wanaishi hapo kwa hisani tuu, vinginevyo watatimuliwa warudi kwao Oman walikotoka, wao na vizalia vyao!.”

“Hizi historia za kutunga tunga kutaka kuwahalalisha madhalimu hawa waliowauza mababu zetu kama bidhaa! hazitasaidia kitu! no wonder kila siku wanashinda uchaguzi lakini kamwe hawatakabidhiwa nchi, na 2015 watashinda tena na moto ni ule ule! Mwarabu atoke kwao, aje akutawale, babu zako awauze, kisha mumpindue halafu leo mumrudishe eti kisa amechaguliwa! hii haitakaa itokee!.”

Huyu kiumbe kutoka Bara anawaambia Wazanzibari wenye asili ya Kishirazi, Kiarabu, Kihindi na nyinginezo, kuwa hawana haki yoyote ile kwao Zanzibar. Wenye haki ni wao Wabara! Kama huu si ujeuri mkubwa sana na ubeberu akhasi ya ukoloni, basi sijui tuuitaje! Ikisha anawaambia Wazanzibari hao kuwa hata wakishinda chaguzi vipi, wao wakoloni ndio watakaoamua, na wameamua kuwa Zanzibar itabakia kuwa koloni lao hata Wazanzibari wote wakitaka kutokana na ubeberu huo unaowakandamiza. Kwa hivyo akina Sefu na Jussa na Mansuri na Moyo na wafuasi wenu ndiyo mmeshapewa tahadhari na mabeberu wakoloni wepya kutoka bara wanaotaka kukutieni nyote vitanzi wakunyongeni, msiseme hamkutahadharishwa na waliyoyakusudia. Kivitendo wameshawauwa Wazanzibari 1961, 1964 na kuendelea. Wanadhani ukhabithi wao na mauwaji wanayoyafanya mara kwa mara ndiyo yatawawezesha kuitawala Zanzibar milele. Yaguju!

Huwezi kuzungumza na mtu ambaye kwake yeye taarikh ya Waarabu Zanzibar na pwani ya Afrika Mashariki imeanzia na Sayyid Said mnamo Karne ya Kumi na Tisa tu! Ni shida kubwa sana kumsomesha mtu taarikh asiyotaka kuisikia, na hakuna viziwi zaidi kuwashinda wale wasiotaka kusikia. Na uziwi unakufika upesi sana iwapo utotoni umepikwa na propaganda za chuki zinazokusudia kuufunga ubongo wako usiweze kufikiri kama mwana Adamu anavyotakiwa afikiri.

Ibrahim Noor
 
Pasco,
Nimepokea salaam zako kutoka kwa Prof. Ibrahim Noor.
Salaam ni hizi hapa chini zisome

Ibrahim Noor
Mkuu Maalim Mohamed Said, sorry my sixth sense tells me aliyeandika salam hizi sio Prof. Ibrahim Noor bali ni wewe!.
Maadam kujiunga na jf ni bure, mkaribishe ajiunge azijibu hoja zake, ila kwa vile wewe ndie uliyemleta humu, uko huru kumjibia, ila mimi sitokujibu kitu maaa nakumbuka matokeo ya kujibishana na baadhi ya watu humu, sometimes it is better kujikalia kimya!.

Pasco.
 
Pasco,
Nitakuwa na sababu gani mie kujificha nyuma ya Prof. Noor? Huyo ni mwenyewe Prof. Ibrahim Noor ondoa hofu. Huoni hiyo siyo style yangu ya uandishi? Angalia na hicho Kiswahili huoni anaandika Kiunguja? Prof. atakusoma na ikiwa atapenda kujiunga na sisi hapa Majlis itakuwa vyema sana. Mimi ningefurahi sana kwa faida yetu sote kama ungemjibu.
 
Alama Mohamed Said, Professor Noor kaelezea kidiplomasia katika kumjibu Pasco kuwa wamejazwa "propaganda" kile ambacho mimi huwauliza watu kama huyu Pasco siku zote, "hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?".

Kwa "argument" kama hii ya Pasco wanazidi kunipatia jibu na kujidhihirisha kuwa ni kweli walisomea ujinga. Ikiwa hata hawajuwi kuwa Wabantu ni wahamiaji tu hii pwani ya Afrika Mashariki na waliwakuta wenyeji wako bukheir kabisa, basi sina budi kusema, kwa hakika wamesomea ujinga.

Ngoja nimpe Pasco kipande hiki kidogo kutoka kwa wana historia wengine na asione kuwa Professor Noor kusema Wabantu ni wahamiaji tu pwani ya Afrika Mashariki ni kituko alichojitungia tu, aelewe kuwa huo ni ukweli wa Kihisitoria.

Na hii ni kutoka chuo cha Makerere, wala si mbali na ni somo linalofundishwa wala si kituko:

BANTU MIGRATION

Between 1000-1800 AD, East Africa experienced a wave of migrations from different parts of Africa. The Bantu from the Congo or the Niger Delta Basin were the first to arrive, followed by the Luo from Bahr el Ghazel in Southern Sudan and then the Ngoni from Southern Africa.

Who were the Bantu?

The term Bantu refers to group of people who speak the same or similar language with common word "NTU" which means a person. The Bantu-speaking groups include the Baganda, Banyoro, Batoro in Uganda, Kikuyu, Akamba, Meru, Embu, Taita, Giryama, Digo in Kenya and Pokomo, Chagga, Yao, Segeju, Zaramo in Tanzania, as well as many other smaller groups.

Origin

There are two versions explaining the migration of the Bantu. The first version asserts that the Bantu came from West Africa around the Cameroon Highlands and Baunchi plateau of Nigeria; therefore, this points to the Niger basin as the possible cradle land of the Bantu. The second version posits that the Bantu came from the Katanga region in Southeastern Congo. Gradually they spread eastward north of the forest and southward to the forest's edge near the lower Congo or Zaire and lower Kasai. The occupation of the north western (Cameroon- Gabon) was fairly slow due to difference in languages. Else where especially in eastern and southern Africa beginning at the edge of the forest, the spread must have been fast due to the relationship in languages.

The study of migrations will help the learners to understand their origin and settlement patterns, appreciate the interrelationship between the different peoples of East Africa like cultures, customs, etc. They will also understand change and continuity in societies i.e. life is not static but dynamic and this explains the current movements of people to different parts of East Africa.

Soma zaidi: ELATE
Pasco, unazidi kunihakikishia kuwa shule ulienda kusomea ujinga.
 
Mkuu Maalim Mohamed Said, sorry my sixth sense tells me aliyeandika salam hizi sio Prof. Ibrahim Noor bali ni wewe!.
Maadam kujiunga na jf ni bure, mkaribishe ajiunge azijibu hoja zake, ila kwa vile wewe ndie uliyemleta humu, uko huru kumjibia, ila mimi sitokujibu kitu maaa nakumbuka matokeo ya kujibishana na baadhi ya watu humu, sometimes it is better kujikalia kimya!.

Pasco.

Fortunately or unfortunately your "sixth sense" has never been right, at least to me, for quite sometime now I've seen you mentioning it and never seen when or where it was right even once. I doubt if it will ever be.

You know why? sorry to tell you, because you simply lack the gift of ESP (Extra Sensory Perception) no matter how much you try to force or to make yourself believe that you have it, its just not there.

ESP is a unique gift gifted to very few and you'll never hear them talk of their abilities or their sixth or any other senses, they will just perceive, comment and move on. They have no reason to prove anything to anyone.

By the way, talking about sixth sense? its only the limited ones (stupid ones) who limit themselves at the "sixth sense", a simple normal human being possesses far more senses then the so called "sixth sense" let alone the gifted ones.

Pole sana, lakini imebidi nikupe hilo darsa dogo kuhusu "sixth sense" kwa kuwa upeo wako ulipofikia umekufanya uone kama unaongea kitu cha maana sana kwa kuwa tu umesoma pahala kuhusu "sixth sense". Unanikumbusha kisa cha kipofu aliyeona punda.

Una mengi sana ya kujifunza.
 
The problem is hiyo historia mnayotaka kuandika Iko too biased na inaonyesha kwamba huyo prof ana agenda zake ambazo zinaweza zikaleta uvunjifu wa amani

Nakuomba soma historia inayofundishwa na Chuo Kikuu Cha Makerere ambacho wasomi wetu wa zamani wamesoma huko, nimeweka kipande kidogo hapo kwenye post namba 129 halafu utueleze kulikoni?
 
FaizaFoxy,

Mimi nimeikuta mada hii ipo kati na nimeshindwa kufuatia yote humu kwa sababu nina maswali machache tu sitopenda kuchanganya na wengine. Kwa huyo mwenye taaluma juu ya swala zima la Udini ningependa anijuze, kwa sababu kinachonishangaza miye, amechanganya sana Uarabu, utawala na Udini kiasi kwamba nimeshindwa kumuelewa lengo la la kitabu chake haswa ni lipi maana dini imekuja baadaye kabisa na utawala wa Kiarabu kufuatia na vyote hivi havikutoka sehemu moja.

Wakati waarabu wakija pwani ya Mashariki ya bara la Afrika karne hizo walikuja fanya biashara na wenyeji wa bara hilo (sijui kina nani atueleze) hata wakaliita bara la weusi, leo inakuwaje mfanya biashara awe na haki sawa na mkazi kwa kutumia vigezo gani maana hawakuja kuleta dini wala kutawala.

Dini ya kiislaam imekuja barani karne ya 14 kama sio 15 wakati waarabu (Washihir na Pashtun) tayari wakifanya biashara hiyo na hawakuwa waislaam maana hapakuwepo na dini hiyo. Na historia inatuonyesha wazi kwamba kulikuwepo na Utawala wa Sultan ulokuja baadaye karne ya 18 iweje vitu hivi vihusishwe na kutungwa kama vina historia moja?
 
Pasco,
Nitakuwa na sababu gani mie kujificha nyuma ya Prof. Noor? Huyo ni mwenyewe Prof. Ibrahim Noor ondoa hofu. Huoni hiyo siyo style yangu ya uandishi? Angalia na hicho Kiswahili huoni anaandika Kiunguja? Prof. atakusoma na ikiwa atapenda kujiunga na sisi hapa Majlis itakuwa vyema sana. Mimi ningefurahi sana kwa faida yetu sote kama ungemjibu.
Mkuu Maalim Mohamed Said, kwa posti hii, nakuamini, nakuomba radhi kwa ku ku doubt mwanzo kwa sababu sometimes hii sixth sense sio sauti ya Mungu bali ni ibilisi shetwaan ana ji disguise as God!.

Kwa vile mjadala umeuleta humu jf, mimi nimejibia humu, jf, na kujiunga na jf ni bure, mkaribishe Prof. Noor aje humu in person, tuhangaike nae!, and not through a third party!.

Ahasanta.

Pasco
q
 
FaizaFoxy,

Mimi nimeikuta mada hii ipo kati na nimeshindwa kufuatia yote humu kwa sababu nina maswali machache tu sitopenda kuchanganya na wengine. Kwa huyo mwenye taaluma juu ya swala zima la Udini ningependa anijuze, kwa sababu kinachonishangaza miye, amechanganya sana Uarabu, utawala na Udini kiasi kwamba nimeshindwa kumuelewa lengo la la kitabu chake haswa ni lipi maana dini imekuja baadaye kabisa na utawala wa Kiarabu kufuatia na vyote hivi havikutoka sehemu moja.

Wakati waarabu wakija pwani ya Mashariki ya bara la Afrika karne hizo walikuja fanya biashara na wenyeji wa bara hilo (sijui kina nani atueleze) inakuwaje leo mfanya biashara awe na haki sawa na mkazi kwa kutumia vigezo gani maana hawakuja kuleta dini wala kutawala.

Dini ya kiislaam imekuja barani karne ya 14 kama sio 15 wakati waarabu tayari wakifanya biashara hiyo na hawakuwa waislaam maana hapakuwepo na dini hiyo. Na historia inatuonyesha wazi kwamba kulikuwepo na Utawala wa Sultan ulokuja baadaye karne ya 18 iweje vitu hivi vihusishwe na kutungwa kama vina historia moja?

Dini ya Kiislam haikuja Afrika Mashariki karne ya 14 au 15 kama unavyodhani, historia inasema Kilwa baina ya mwaka 960 na 1000 AD tayari kulikuwa na mtawala kwa jina Ali ibn Al Hassan Al Shirazi. Na kabla ya hapo ukienda deep utakuta kuna mabaki (ruins) za Waislam wa kabla ya mwaka huo katika pwani ya Afrika Mashariki.

Source: http://en.wikipedia.org/wiki/Kilwa_Sultanate

Vasco Da Gama ndiyo alifika pwani hii mwaka 1497 na alikuta maajabu ambayo hata Uropa alipotoka yalikuwa hakuna. Alikuta kuna nyumba za ghorofa, alikuta kuna nyumba zinapakwa rangi (Ulaya ilikuwa bado), alikuta watu wanatumia vifaa vya kauri za kutoka China (Ulaya ilikuwa bado) , alikuta watu wanavaa libasi za hariri kutoka China (Ulaya ilikuwa bado), alikuta watu wana sarafu za dhahabu. Alikuta watu wana dini yao Uislam, alikuta watu wanajuwa kusoma na kuandika, na alikuta watu walioelezea kuhusu Taifa la Ukristo lililopo Kaskazini (Habashi).

Ukiisoma historia ya Vasco Da Gama, utakuta kuwa alipofika Kilwa au Sofala (sikumbuki vizuri) viongozi wa huko wa siku hizo tayari wakiijuwa njia na namna ya kufika Hindi mpaka Uchina na kwa kumsaidia tu na kumtambia kwa kuwa alikuwa haijuwi njia ya kufika huko, alipewa baharia wa kuwaongoza msafara wao, cha ajabu alipewa nahodha kipofu na alimwelekezea merikebu zake kwa kusikiliza upepo, kunusa na kuonja maji ya baharini. Ajib. Malipo yake? akaja kuwapiga aliporudi mara ya pili. Kisa? walikuwa Waislam na yeye yuko kwenye kurusedi.

Hayo yapo kwa ushahidi kabisa, tafuta kitabu kinaitwa "Empires of The Monsoon" cha Richard Hall. Utafaidi sana utakuwa hutaki kukiweka chini jinsi mwandishi huyo alivyoweka vizuri historia.

Kwa hayo machache utaona kuwa Uislam ulikuwepo kabla ya hizo karne ulizozitaja.

Alama Mohamed Said, kitabu hicho cha Empires of The Monsoon niliazimwa na Ammi yangu Faraj Tamim nami nikakipiga copy, na ndani kilikuwa na jina lako. Ammi Faraj Tamim anajuwa nnapenda History kwa hiyo akipata kipya hunikumbuka.
 
Fortunately or unfortunately your "sixth sense" has never been right, at least to me, for quite sometime now I've seen you mentioning it and never seen when or where it was right even once. I doubt if it will ever be.

You know why? sorry to tell you, because you simply lack the gift of ESP (Extra Sensory Perception) no matter how much you try to force or to make yourself believe that you have it, its just not there.

ESP is a unique gift gifted to very few and you'll never hear them talk of their abilities or their sixth or any other senses, they will just perceive, comment and move on. They have no reason to prove anything to anyone.

By the way, talking about sixth sense? its only the limited ones (stupid ones) who limit themselves at the "sixth sense", a simple normal human being possesses far more senses then the so called "sixth sense" let alone the gifted ones.

Pole sana, lakini imebidi nikupe hilo darsa dogo kuhusu "sixth sense" kwa kuwa upeo wako ulipofikia umekufanya uone kama unaongea kitu cha maana sana kwa kuwa tu umesoma pahala kuhusu "sixth sense". Unanikumbusha kisa cha kipofu aliyeona punda.

Una mengi sana ya kujifunza.
Mkuu FaizaFoxy, kwanza asante kwa genuinity ya bandiko hili, na yote usemayo ni kweli, kuhusu Sixth Sense, nimeisoma tuu nilipokuwa India, na pia ni kweli wenyewe wenye nazo, they never boast about their possessing ESP, bali sisi tusonazo!.
Hili ni moja ya majibu yako yenye ile objectivity ya yule FaizaFoxy, niliyemfsahamu nilipojiunga na jf, ambaye ni tofauti na yule wa kuhororoja humu, ila kwa vile mimi ni muumini wa the principle ya Me & I, then kuna wa mwezi mpevu ambaye ni mmoja, wa full moon ni mwingine, na wa moonless ni mwingine tena!. Asante!.

Ila pia karibu unitembelee hapa
[h=3]Psychic Powers: Ni Nguvu za Kufanya Miujiza. Wengi wanazo
[/h][h=3]Life after death: What Happens After Death?
[/h][h=3]"Will Powers!", "Faith Healing!"-Ni Nguvu ya Kufanya Miujiza Ya Uponyaji kwa Imani.
[/h]Ukiwa na la kuchangia changia!.

Pasco
 
Mkuu FaizaFoxy, kwanza asante kwa genuinity ya bandiko hili, na yote usemayo ni kweli, kuhusu Sixth Sense, nimeisoma tuu nilipokuwa India, na pia ni kweli wenyewe wenye nazo, they never boast about their possessing ESP, bali sisi tusonazo!.
Hili ni moja ya majibu yako yenye ile objectivity ya yule FaizaFoxy, niliyemfsahamu nilipojiunga na jf, ambaye ni tofauti na yule wa kuhororoja humu, ila kwa vile mimi ni muumini wa the principle ya Me & I, then kuna wa mwezi mpevu ambaye ni mmoja, wa full moon ni mwingine, na wa moonless ni mwingine tena!. Asante!.

Ila pia karibu unitembelee hapa
Psychic Powers: Ni Nguvu za Kufanya Miujiza. Wengi wanazo

Life after death: What Happens After Death?

"Will Powers!", "Faith Healing!"-Ni Nguvu ya Kufanya Miujiza Ya Uponyaji kwa Imani.

Ukiwa na la kuchangia changia!.

Pasco

Akutukanae hakuchagulii tusi.

Hizo nyuzi nilizipitia zamani, ingawa umejitahidi kuelezea lakini zipo to "amateurish" na "too shallow for my liking". Ndiyo maana nikashindwa hata ku comment, nadhani kama sikusahau, nili comment kwenye moja sikumbuki ipi.

Leo ni mwezi upi?
 
Dini ya Kiislam haikuja Afrika Mashariki karne ya 14 au 15 kama unavyodhani, historia inasema Kilwa baina ya mwaka 960 na 1000 AD tayari kulikuwa na mtawala kwa jina Ali ibn Al Hassan Al Shirazi. Na kabla ya hapo ukienda deep utakuta kuna mabaki (ruins) za Waislam wa kabla ya mwaka huo katika pwani ya Afrika Mashariki.

Source: Kilwa Sultanate - Wikipedia, the free encyclopedia

Vasco Da Gama ndiyo alifika pwani hii mwaka 1497 na alikuta maajabu ambayo hata Uropa alipotoka yalikuwa hakuna. Alikuta kuna nyumba za ghorofa, alikuta kuna nyumba zinapakwa rangi (Ulaya ilikuwa bado), alikuta watu wanatumia vifaa vya kauri za kutoka China (Ulaya ilikuwa bado) , alikuta watu wanavaa libasi za hariri kutoka China (Ulaya ilikuwa bado), alikuta watu wana sarafu za dhahabu. Alikuta watu wana dini yao Uislam, alikuta watu wanajuwa kusoma na kuandika, na alikuta watu walioelezea kuhusu Taifa la Ukristo lililopo Kaskazini (Habashi).

Ukiisoma historia ya Vasco Da Gama, utakuta kuwa alipofika Kilwa au Sofala (sikumbuki vizuri) viongozi wa huko wa siku hizo tayari wakiijuwa njia na namna ya kufika Hindi mpaka Uchina na kwa kumsaidia tu na kumtambia kwa kuwa alikuwa haijuwi njia ya kufika huko, alipewa baharia wa kuwaongoza msafara wao, cha ajabu alipewa nahodha kipofu na alimwelekezea merikebu zake kwa kusikiliza upepo, kunusa na kuonja maji ya baharini. Ajib. Malipo yake? akaja kuwapiga aliporudi mara ya pili. Kisa? walikuwa Waislam na yeye yuko kwenye kurusedi.

Hayo yapo kwa ushahidi kabisa, tafuta kitabu kinaitwa "Empires of The Monsoon" cha Richard Hall. Utafaidi sana utakuwa hutaki kukiweka chini jinsi mwandishi huyo alivyoweka vizuri historia.

Kwa hayo machache utaona kuwa Uislam ulikuwepo kabla ya hizo karne ulizozitaja.

Alama Mohamed Said, kitabu hicho cha Empires of The Monsoon niliazimwa na Ammi yangu Faraj Tamim nami nikakipiga copy, na ndani kilikuwa na jina lako. Ammi Faraj Tamim anajuwa nnapenda History kwa hiyo akipata kipya hunikumbuka.
Kwanza inabidi nikuombe samahani lengo langu la kuandika ujio wa uislaam ulikuwa karne 4 hadi ya 5 nimefanya makosa ya kiuandishi.. Ndivyo nilivyo. Hilo nadhani tumelimaliza isipokuwa nachotaka kujua huyu mwandishi anapochanganya Ujio wa waarabu ma wahindi walokuja fanya biashara nchini walikuja fanya biashara na watu gani ikiwa Wabantu hawakuwepo? na kwa nini waarabu walilita bara letu bara la weusi. halafu anasahau kuna Utawala wa Kiarabu (Oman) tofauti kabisa na ujio wa WaYemen au Wa Afghan/Pakistan. Kuna swala la Dini kutoka Saudia kupitia Magadishu na kushuka kwetu vinahusiana vipi vyote hivi na biashara ya Utumwa au Mapinduzi ya Zanzibar.

Halafu nikwambie kitu, Ibrahim Noor anafanya makosa makubwa ya kujaribu kupamba historia mabya kwa mafuta, kwa sababu hata huku Marekani wapo wazungu wabaguzi na tunawajua, wanajaribu sana kusema hapakuwepo na Utumwa, hawakuwepo na mauaji ya watu weusi isipokuwa watu weusi ndio Thugs. Kwa hiyo mimi ananipa picha tofauti kabisa kwa sababu huwaona hawa wazungu wanavyojaribu kujikosha kwamba wao ni watu wazuri sana na kwamba yaloandikwa kuhusu wao ni uzushi mtupu, sisi waafrika ndio tuliuzana wenyewe ktk Utumwa..

Hii mbaya sana kuanza kutenganisha watu kwa rangi zao maana historia yetu haiandikwi kwa makundi ya rangi za watu ama imani zao ila kuna historia za makabila. na anapozungumzia Uislaam unazungumzia watu wote kwa sababu Uislaam ulisambazwa Afrika sio na waarabu bali wasomi walokwenda jifunza dini wengine walikuwa waafirka weusi waloijua dini kuliko waarabu wenyewe. Sio kila mwarabu aliujua Uislaam ama alikuwa mwalimu wa dini wengi walikuja kwa sababu ya biashara na wengine kutawala.

halafu biashara ya Utumwa inajulikana wazi kwamba wote wazungu, waarabu na wayahudi walishirikiana kufanya biashara hiyo hakuna mwenye nafuu zaidi ya mwenzake. Mwarabu akiwa mtawala alipewa deal la WATU kuwa wanatakiwa kwenda kufanya utumwa Ulaya na bara Amerika na kichwa ni Dollar 10,000. Mwarabu akaingia bara alikokubalika maana walikuwa wakifanya biashara za vito na spices wakakusanya watumwa na kuwaleta Coast kuwauzia Wazungu.

Ndio maana masoko yote ya Utumwa yalikuwa makanisa yenye undergraound kupitishia watumwa hadi ufukweni. Na Wayahudi ndio walokuwa na utajiri wa Melikebu zao wakinunua watumwa na kwenda wauza Ulaya, hii ni history ilofichwa na pande zote kwa sababu Muafrika haweki kumbukumbu zake na rahisi kudanganywa. Mimi sina sababu ya kumsma Ibrahim Alnoor kwa sababu anachokifanya ni makosa ni sawa kabisa na washawishi wa KKK wanaojaribu kuonyesha upendo kwa weusi huku ndani ya roho zao wakijua machafu yao hayasafishiki..

Uislaam has nothing nothing to do with Waarabu au Wahindi. Imani ya dini haihusiani na mambo waloyafanya waarabu au wahindi ama kuwapa uhalali juu ya bara hili isipokuwa tuishi pamoja na kwa mapenzi ya UTAIFA na kutojali tofauti zetu za rangi na imani maana leo hii wewe FaizaFoxy ukienda Arabuni hutapewa haki sawa na mwarabu hata kama babu wa mababu wako walikuwa na asili huko. Nenda Saudia, Pakistan, Afghanstan japo weusi walikuwepo kwa karne bado hawana haki sawa na warabu weupe. Hata Hadith za Mtume zimetueleza juu ya Bilal iwe hawa! what happen - happened tuyaache tusianze kukumbushana yalopita.
 
Back
Top Bottom