Kitabu kipya: Tanzania na propaganda za udini na prof. Ibrahim Noor

Kitabu kipya: Tanzania na propaganda za udini na prof. Ibrahim Noor

Kama nimemisunderstand i take back my word, kimsingi sinashida na uislam hata jina kiweje so long as theme haiki biased ila kinacho nisikitisha huwa kila kitabu ama maandishi wanayoandija kuhusu uislam huwa ni malakaniko tu, utasikia historia ya waislam imepotoshwa, mara mambo ya waislam yalinyanganywa kitu ambacho binafsu sikiamini kwani naamini hao waislqm wakipindi hicho nao walikuwa na akili timamu,

Kama kuna mambo waislam wa sasa wanatakiwa kuyafanya ni kurekebisha kasoro walizofanya waislam waliotangulia kwa kuweka vitu kwenye maandishi......

Na hili lilitokea pale walipopuuzia kusoma elimu ya hii ya maisha ya kawaida kwani kwenye elimu hii ndipo watu wanapopata fulsa hata ya kuandika maishayao kabla hata ya kuwa historia.....

Nampongeza sana mwandishi kwa kusoma vizuri mpaka ngazi aliyofikia na pia natiwa moyo na waislam wa siku hizi kwan wengi sana wanapeleka watoto wao shule na pia wao wanasoma.....

That great for future peace of the world.
Mbarikiwe
Ukweli siku zote hufichwa na mdhulumu ili aweze kudhulumu vizuri
Sasa watu hasa watz wanaogopa kuelezwa Ukweli kwan wapo wanao dhulumu.
2. Waislam walisoma, wamesoma, na wanasoma ndio mama akionekana msomi watu wanashangaa. Hapo nyuma wakati Wa ukoloni na baada ya Uhuru waislam walobanwa kupata elimu kwa kisingizio hawataki kusoma !!!??
Sasa ukitolewa Ukweli wamaendelea na kutuhofisha
Washaishiwa tumeamka
 
Yaani Mwarabu ametangulia Afrika ya Mashariki maelfu ya miaka iliyopita na Wabantu ndio wakaja ile karne ya 16 B.K akimaanisha ndio waliowakuta Waarabu!. Hili ni chapisho la spin doctor kutaka kutuamini kuwa Waarabu hapa ndio kwao, na Wabantu ndio wamewakuta!!. Kwa Waarabu sio wageni bali ni wenyeji wenye haki sawasawa na wenyeji wengine!. OMG!.
Katika hatua hii, jambo zuri la pekee kwangu mimi katika kitabu hiki ni kule tuu kutambua kuwa miaka ya zamani inatambulishwa properly 16 B.K na kwa herufu kubwa, kumaanisha miaka hiyo meanza kuhesabiwa kwa reference ya Kristu!.

Pasco

Wacha kupindisha maneno, soma tena ulichokiandika

"Hiki kitabu kinataka kueleza uongo kuwa eti Waarabu walihamia Pwani ya Afrika ya Mashariki karine ya 16 BC hawakukuta wenyeji wowote"

Hicho umekitoa wapi?
 
Pasco Waarabu hawakuja Afrika, Waarabu asili yao ni Afrika.

Inasikitisha sana kuona kuwa historia iliyowajaza ujinga ikisema Waarabu wamekuja Afrika.

Kwanza kabisa ningependa ufahamu kuwa Uarabu si kabila wala rangi, Uarabu simply ni lugha.

Waarabu wengi leo hii wako Afrika, lugha ya kwanza kuongewa na wengi Afrika ni Kiarabu na haijawahi kuwa vinginevyo, jana , juzi , majuzi, rudi nyuma miaka mia, elfi, maelfu upendavyo utakuta ni hayo hayo. Utapofikia katika usomi wako ukakuta "wamekuja" nioneshe nami nipaelewe.

Tatizo kubwa sana linakuja pale mnapoamini, kwa ujinga tu, kuwa Uarabu ni tabaka la kabila au rangi ya watu fulani. La hasha, huko ni kule mimi nnapokuita kusomea ujinga.

Historia yoyote ile uipendayo, haioneshi na haitoweza kuonesha Mwarabu Afrika alikuja lini kwanza, isipokuwa kuna dhanna tu ya "tarikh" historia inayoonesha Mwaarabu alikutwa lini Afrika, jee na nani? na kwanini akutwe? Fikiri.

Unaanza kuponda "itroduction" iliyowekwa hapa kabla hujakisoma kitabu, jee, ni kwa jina tu la aliyetunga kitabu?

Unataka kutuaminisha kuwa "sixth sense" yako yakufikirika ina maana zaidi ya kitabu ambacho hujakisoma?

nono.gif

Acha kujidanganya. Uarabu ni lugha,rangi na zaidi ni historia ya familia yako. kama unabisha nenda Sauidi na pua yako ya kibantu alafu uwaambie wewe ni muarabu kwasababu unajua lugha ya kiarabu. Wabantu wa wanaoishi somalia wenye asili ya kizigua wanabaguliwa mpaka leo na wasomali kuwa wao sio waarabu wakati hata waarabu wenyewe wanasema wasomali sio waarabu. Tatizo wabantu wengi wa bwani ya afrika wanakasumba ya kujitambulisha kama waarabu na anaejiona ndio muarabu zaidi basi anaona ndio wa maana zaidi na anahaki zaidi ya wabantu wenzake. hii tabia ndio inao wamaliza somalia kwakuuana maana wote waislam ila koo tofauti lakini wanauana kwa kuona koo zao ni bora na niwazawa wa mtume muhammad. kama unabisha mfatilie Dr. Omar Eno na kaka yake kwenye mijadala ya Bantu Somali. na mfano moja ni huu hapa chini wa Somali Identity
.
https://www.youtube.com/watch?v=UNQbQseoRIU

https://www.youtube.com/watch?v=kRfIUpJGUn8
 
Don't judge a book by its cover
1st pass through it
Tupate muda Wa kukipitia tuache negative attitude huu ya jambo laweza kukusaidia wewe najamii
Tukisome kwanza kukurupuka marufuku
Tupo jukwaa hili la Fikra tuzitumie Fikra Zetu vizuri
 
Vinauzwa sana maeneo ya misikitini hata jana nimekiona pale msikiti wa Ujumaa miyomboni.
Sijajua sababu ni nini?
 
Acha kujidanganya. Uarabu ni lugha,rangi na zaidi hata historia ya familia yako. kama unabisha nenda Sauidi na pua yako ya kibantu alafu uwaambie wewe ni muarabu kwasababu unajua lugha ya kiarabu. Wabantu wa wanaoishi somalia wenye asili ya kizigua wanabaguliwa mpaka leo na wasomali kuwa wao sio waarabu wakati hata waarabu wenyewe wanasema wasomali sio waarabu. Tatizo wabantu wengi wa bwani ya afrika wanakasumba ya kujitambulisha kama waarabu na anaejiona ndio muarabu zaidi basi anaona ndio wa maana zaidi na anahaki zaidi ya wabantu wenzake. hii tabia ndio inao wamaliza somalia kwakuuana maana wote waislam ila koo tofauti lakini wanauana kwa kuona koo zao ni bora na niwazawa wa mtume muhammad. kama unabisha mfatilie Dr. Omar Eno na kaka yake kwenye mijadala ya Bantu Somali. na mfano moja ni huu hapa chini wa Somali Identity
.

https://www.youtube.com/watch?v=kRfIUpJGUn8

Wewe unaongelea ubaguzi> ubaguzi hata Afrika ndio kwenyewe, au huna habari zinazoendelea Afrika ya Kusini? Huko nako ni Waislam wanabaguana na kuuana?

Hata maana ya Saudi Arabia hauijuwi halafu unataka kuongelea Saudi Arabia? Unajuwa ni lini hiyo nchi iliitwa hivyo?

Wacha kuhororoja na kubwabwaja bila mpango, nisome tena, saidiana na Pasco kisha mjibu hili:

Waarabu wengi leo hii wako Afrika, lugha ya kwanza kuongewa na wengi Afrika ni Kiarabu na haijawahi kuwa vinginevyo, jana , juzi , majuzi, rudi nyuma miaka mia, elfi, maelfu upendavyo utakuta ni hayo hayo. Utapofikia katika usomi wako ukakuta "wamekuja" nioneshe nami nipaelewe.
 
Nadhani kitabu kinawasafisha walioleta dini ya uislam...
 
Kabla hujasoma historia yeyote soma historia ya mwandishi. Maudhui ya kitabu yako wazi, kinapigiwa debe na Mohammed Said!, kinauzwa msikitini!, kimeandikwa na mwarabu mwislamu, na kinaelezea mahusiano ya waafrika na waarabu (baba zake) wakati wa utumwa. Unategemea aandikeje?

Historia uliyosoma wewe iliandikwa na nani?
 
Wacha kupindisha maneno, soma tena ulichokiandika

"Hiki kitabu kinataka kueleza uongo kuwa eti Waarabu walihamia Pwani ya Afrika ya Mashariki karine ya 16 BC hawakukuta wenyeji wowote"

Hicho umekitoa wapi?
Nimekubali, andiko limeeleza kuwa Waarabu ndio waliotangulia kufika Pwani ya Afrika ya Mashariki, halafu Wabantu ndio wakaja ile karne ya 16, ikimaanisha ndio waliowakuta Waarabu!.

Admission "hawakukuta wenyeji wowote" ni my own insertion!.

Pasco

 
saidiana na Pasco kisha mjibu hili:

Waarabu wengi leo hii wako Afrika, lugha ya kwanza kuongewa na wengi Afrika ni Kiarabu na haijawahi kuwa vinginevyo, jana , juzi , majuzi, rudi nyuma miaka mia, elfi, maelfu upendavyo utakuta ni hayo hayo. Utapofikia katika usomi wako ukakuta "wamekuja" nioneshe nami nipaelewe.
Nitasaidia kama ulivyoshauri, lakini subiri kwanza nikisome kitabu chenyewe, hayo maongo tuu ya mwanzo ni kichocheo tosha cha kesho asubuhi subuhi kitabu mkononi, ndipo tuendelee!.

Pasco
 
Wewe unaongelea ubaguzi> ubaguzi hata Afrika ndio kwenyewe, au huna habari zinazoendelea Afrika ya Kusini? Huko nako ni Waislam wanabaguana na kuuana?

Hata maana ya Saudi Arabia hauijuwi halafu unataka kuongelea Saudi Arabia? Unajuwa ni lini hiyo nchi iliitwa hivyo?

Wacha kuhororoja na kubwabwaja bila mpango, nisome tena, saidiana na Pasco kisha mjibu hili:

Waarabu wengi leo hii wako Afrika, lugha ya kwanza kuongewa na wengi Afrika ni Kiarabu na haijawahi kuwa vinginevyo, jana , juzi , majuzi, rudi nyuma miaka mia, elfi, maelfu upendavyo utakuta ni hayo hayo. Utapofikia katika usomi wako ukakuta "wamekuja" nioneshe nami nipaelewe.

Kunatofauti kubwa kati ya kinachoendelea Afrika kusini na kinachoendelea Sauidi Arabia. Kinachoendelea Afrika kusini ni Waafrika wenye njaaa wanao wafukuza Waafrika kutoka nchi nyingine bila kujali kuwa ni waafrika wenzao. Lal
kini Kinachoendelea saudi Arabia ni Kuwakataa waafrika kuwa sio waarabu wenzao kwa rangi, Tamaduni na hata kwenye kidini na ndio maana hata Alkaida walikuwa wakiwalipa familia ya wanao jilipua kutoka afrika hela ndogo kuliko familiya ya anaye jilipua kutoka Saudi Arabia. Wewe kama ni mzaramo uliebaatika kukijua kiarabu usijidanganye kuwa wewe ni Mwarabu bali wewe ni Mwarabukoko.

Umenangalia mbantu wa kizigua anvyobaguliwa somalia


 
Nimekubali, andiko limeeleza kuwa Waarabu ndio waliotangulia kufika Pwani ya Afrika ya Mashariki, halafu Wabantu ndio wakaja ile karne ya 16, ikimaanisha ndio waliowakuta Waarabu!.

Admission "hawakukuta wenyeji wowote" ni my own insertion!.

Pasco


Bado, si hilo tu, mimi naona hii sentensi yote ni yako na sijaiona popote kwenye "introduction":


"Hiki kitabu kinataka kueleza uongo kuwa eti Waarabu walihamia Pwani ya Afrika ya Mashariki karine ya 16 BC hawakukuta wenyeji wowote"


Wapi umeitoa hiyo kama si "spinning"?
 
Propaganda ikishatengenezwa na kuenezwa kwa muda mrefu....huwa ni ngumu sana kuja kubainisha urongo na ukweli....bahati mbaya zaidi...watu hupenda propaganda zaidi...niseme tu kuwa....katika oficial history...mambo mengi huwekwa katika kumbukumbu ambayo ynasupport au yanasaidia watawala kukakaa madarakani....ni mkakati wa kisaikolojia...tujipe muda tutafakari....kwasababu...uongo unaweza kusafiri dunia nzima wakati ukweli hata haujavaa viatu....!! Mfano rahisi ni ile kampeni ya kwenda vita vya iraq...ulimwengu wote uliamini sadam ana wmd....then baada ya vita ukweli ukawasili...loh!! At what cost??!!!! So let us think...and think again!!!
 
Hivi kile kitabu kilichoandikwa na Salman Rushdie kinachoitwa "Aya za Shetani" kwanini kisiruhusiwe tu watu wengi wakapata kukisoma?au hata hapa jamii forum kikawekwa hadharani....ni katika kupanua maarifa tu!

Mbona umeona hicho cha mbali wakati cha karibu tu hapa hapa Tanzania kipo na walikifungia cha Prof. Njozi "The Mwembechai Killings and Political features of Tanzania "? Ungeomba wakiruhusu hicho kwanza uyajue ya nchini kwako kwanza kabla ya kujua ya mbali....lol
 

[/B][/B]Mkuu Maalim , kwanza asante kutupatia taarifa hizi, sisi wapenzi wa kusoma vitabu, tutakinunua na kukisoma hiki kitabu cha Tanzania na Propaganda za Udini, ila hata kabla sijakinunua na kukisoma, kiukweli kabisa toka ndani ya nafsi yangu, the sixth sense inanieleza the 'motive behind' mwandishi wa kitabu hiki, Prof. Ibrahim Noor Shariff, ni 'ill motive!'. Tangu Mlango wake wa Kwanza unaohusu “Taarikh ya Kuwasili Kwa Wabantu, Washirazi na Waarabu Pwani ya Afrikaya Mashariki.” ameanza na maurongo yaliyokubuhu!, hapa anadanyanya wazi mchana kweupe kwa maushahidi yake ya uongo kwamba eti Waarabu wamefika Pwani ya Afrika Mashariki maelfu ya miaka iliopita kabla ya Wabantu, tangu karne ya 16 B.K!. The ill motive ya mlango huu ni kuonesha kwamba Waarabu si wageni bali ni wenyeji wenye haki hapa sawasasa kwenye Pwani ya Afrika Mashariki sawa na wenyeji wengineo.

Yaani hapa huyu Mwarabu, anataka kuwafanyia Afrikanization hawa wavanizi wa Kiarabu ili kuwahalaliasha eti na wao, ni wenyenyeji halali wa Afrika Mashariki, na wakati huo huo, kuwaondolea Wabantu, uenyeji wao wa asili, kwa kuonyesha kuwa hata hao Wabantu, Afrika ya Mashariki sio kwao asili bali nao pia ni wahamiaji tuu kama Waarabu!. Huu ni uongo uliokubuhu wa mchana kweupe!.

Lengo ni kuzuia kinachoweza kuja kuwapata Waarabu wa Afrika Mashariki na sana sana Waarabu wa Zanzibar ambao wametoka kwao Omani juzi juzi tuu mwaka 1832 wakiongozwa na Sultan Seyyed Said aliye yahamisha makao yake makuu toka Oman hadi Zanzibar!. Huyu sio tuu ni mvamizi bali pia ndiye mporaji mkuu, aliyejitwalia visiwa hivyo kama ameviokota as if hakumkuta mtu yoyote ili hali wenyeji walikuwepo!. Siku ile ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar, siungi mkono mauaji yoyote ya Waarabu, bali wangeambiwa tuu kistaarabu, wafungeshe kilicho chao, wao na wazalio wao, wajirudie kwao Omani walikotoka na kutuachia visiwa vyetu!.

Hili swali la Waarabu wamekujaje Pwani ya Afrika Mashariki, litakuja kurudi tuu mbele ya safari hivyo ushauri wangu, ni kujituliza tuu na kuishi kwa unyenyekevu wa hali ya juu sana kwa kujihesabu wanaishi hapo kwa hisani tuu, vinginevyo watatimuliwa warudi kwao Oman walikotoka, wao na vizalia vyao!.

Hizi historia za kutunga tunga kutaka kuwahalalisha madhalimu hawa waliowauza mababu zetu kama bidhaa!, hazitasaidia kitu!, no wonder kila siku wanashinda uchaguzi lakini kamwe hawatakabidhiwa nchi, na 2015 watashinda tena na moto ni ule ule!. Mwarabu atoke kwao, aje akutawale, babu zako awauze, kisha mumpindue halafu leo mumrudishe eti kisa amechaguliwa!, hii haitakaa itokee!.

Kesho ni sikukukuu ya Muungano, tutakukumbusheni hiyo Zanzibar ilikuwa ni sehemu ya Tanganyika, hivyo huu muungano ni wa milele.

As long as hii ni lilterally work, ngoja nikitafute na kukisoma halafu turudi humu kumwaga mbichi na mbivu!, ila kiukweli lazima hata mtoto wa darasa la 4 akiisikia hii acheke, ati Waarabu nao kwao ni Afrika Mashariki, na Wabantu nao pia ni wageni!. OMG!.

Pasco

Mkuu, unajuwa ili uweze kuingiza idea mpya kichwani mwako ni MUHIMU kufanya ubongo wako uko BLANK ili kuruhusu mawazo mapya kuingia na kuchakata kile ambacho kilikuwepo kabla kisha baadae ndio uamue kipi ni kipi. Sasa wewe unaposema mwandishi amesema urongo kuanzia sura ya kwanza ni kwamba unashikilia msimamo wa kile ambacho ulikijua kabla ya kusoma alichoandika mwandishi.
Nikushauri tu, uwe na tabia ya kisomi tena usomi wa kutafuta ukweli: soma kwanza alichokiandika mwandishi ukiwa na blank mind, usiwe tayari na mtizamo hasi, HUTAELEWA. Hata mimi ni mwanahistoria na nimesoma THE PEOPLING OF EAST AFRICA na pengine tulichofundishwa wengi ndicho hicho unachokijua wewe ,lakini LET THE FACT SPEAK FOR ITSELF , tusome mtazamo wa mwandishi kisha tulinganishe kile tunachokijua, halafu ndio tufikie hitimisho. SI KILA WAKATI TULICHOFUNDISHWA VYUONI NI SAHIHI. Tusikaririshwe, tuwe wasomi wa kuchambua mambo.
Ntakupa mfano: kwa miaka mingi sana, tumekuwa tukifundishwa vyuoni kuwa FANI NA MAUDHUI HAVIWEZI KUTENGANISHWA, huu ni mtizamo ambao ulikubalika na wasomi nguli kama kina prof. SENKORO (Kasome kitabu cha FASIHI alichoandika), lakini ni huyu huyu Prof baada ya miaka na mikaka kupita SASA HIVI ANAYAKANA MAANDISHI NA MTIZAMO WAKE WA ZAMANI na ANAKUBALI kuwa fani na maudhui ni vitu vinavyoweza kutenganishwa akitolea mfano wa nyimbo za kubembelezea watoto hasa katika jamii zinazofuata mfumo wa kibaba
 
Mtu ambae shule ya msingi amesoma miaka kumi utamjua tu, unaanza kupotosha watu, vitabu vinapatikana na nje ya maduka yaliyo katika misikiti, hata kusoma haya tatu tu umeshindwa, utaweza kusoma ktabu kizima au kuona mantiki ya kiuandishi!.
Kabla hujasoma kitabu unaanza kusema ovyo, dalili ya ulevi na uvutaji bangi ovyo,hapo atajiita msomi.
Watu wabovu wa namna hii eti wanapewa madaraka katika nchi, ndiyo maana visomi uchwara vinaingia mikataba mibovu tu, kichwa cha mbu unafanaisha na cha professor! Ni msiba
 
Prof%2BIbrahim%2Bphoto.jpg


Usishangae nayeye anajiita mwarabu.....................................very fan

Kunaupotoshaji wa baadhi ya wachangiaji wanafanya hapa,

1. Uingereza na waingereza nivitu viliwi tofauti - Taifa & watu, mwengereza waweza mpata china, but no England in china

2. Uarabuni na waarabu nivitu viwili tofauti - Taifa na watu, mwarabu waweza mpata Kenya, No Arab nation in Kenya

3. Kiingereza na muengereza nivitu tofauti - Lugha na watu, unaweza kuongea English haimaanisha wewe ni mwengereza

4 kiarabu na mwarabu - Unaweza kuongea kiarabu haimaanishi wewe ni mwarabu

5. Pwani ya Afrika mashariki na Afrika nivitu viwili tofauti, pwani ya afrika ni sehemu tu ya bara la Afrika

-Kusema kiarabu kinaongewa na nchi nyingi zaidi Afrika haimaanishi pwani ya Afrika nao niwaarabu au wanaasili ya waarabu.

-Pwani ya Afrika haiwezi kuwa ya waarabu wala haiwezi kusimama kama nchi ya kiarabu

-Pwani ya Afrika niyawabantu na wabantu sio waarabu hususan pwan ya Afrika mashariki.

Tabia ya Mohamedi Said ya kufitinisha wakaazi wa Tanzania Kwa kisingizio cha Historia ni ukosefu wa adabu kwa watanzania na Taifa kwa ujumla. Huyu Mohamed na wafuasi wake niwachochezi na siku zote huokoteza ujinga popote na kuanzisha upotoshaji. Waathilika wa elimu na makuzi ya utotoni.
 
Back
Top Bottom