Kitambi kimeharibu muonekano wangu, wadada hawanitaki tena

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001

Mimi ni handsome sana, mitaani kote wananisifu. Hata wanawake wananiambiaga. Lakini hawaachi kunikosoa tumbo langu hadi nimeanza kujichukia.

Kwa kweli nakosa sana raha, namtongoza msichana ananiambia na huo mtumbo wako kama umemeza kifaru cha jeshi ntakupeleka wapi mimi?

Six pack sio kwamba sijawahi kuwa nazo, nilikuwa nazo ila nikapata binti wa Kizaramo, asubuhi ananipa chai kikombe kimoja na andazi moja. Mchana hatuli anasema tubane matumizi.
Usiku anapika wali, maharage, nyama, mchicha, dagaa wa bukubuku, miguu ya kuku na supu ya mapupu inakuwepo.

Anasema kwanini tulale na njaa? Tunalala tukiwa tumeshiba sana hadi tunashindwa kupumua.

Tunajambiana huku tukikoroma, wachawi kila siku wanakuja kutukaba kwasababu ya kutuonea wivu mavitu tunayokula la kulala tukiwa tumeshiba matumbo ndiii.

Sasa wachawi wakanionea wivu six packs zangu, wakanuroga nimepata kitambi, sina six packs tena nina mtumbo mkubwa ambao ni single pack.

Mzaramo wangu ananiambia kwao Maneromango kuna mganga anaweza kunitoa hiki kitambi ambacho ni kama nina mpira wa madaso, au kinyengo au chandimu ndani ya tumbo.

Nimemkatalia nimemwambia JF kuna watalaam wa kila sekta.

Wanamitindo wenzangu, naombeni ushauri ili fashenista mwenzenu nirudie utanashati wangu.
To yeye, mzabzab, Baba Swalehe , Mwifwa naamini mtanisaidia
 
Kama wewe ni handsome basi mimi ni legsome.

Na bado kina Unique Flower wananipiga kibuti.

Tulia we mzee, mabinti wanataka hela, sura sio raha.

Ukiuza utumbo, usiogope nzi
 
Tafuta ela mzee, wanawake wanapenda ela suala la 6 pack wanaweza kuvumilia
 
Mkuu Kama Ni wwe bas nimefurahi San kukuona ,live

Uko vzr mkuu mcheki mtu anajita ngosha fit. Anadawa zake za asili

Ila kwani kitambi hicho inakufanya ushindwe kuchakata ?
Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Km nakuona ulivyoooo na kibamiaaaa
 
Mkuu sijawai kukuona kbsa Kama Ni wee huyo bas nimefurahi Sana [emoji38]

Mcheki mtu anaitwa ngosha fit ,Instagram

VIP show unapiga vzr ama kitambi kinazuia na kulower performance

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Mzaramo wangu ananiambia kwao Maneromango kuna mganga anaweza kunitoa hiki kitambi ambacho ni kama nina mpira wa madaso, au kinyengo au chandimu ndani ya tumbo.[emoji23]
 
Na hilo nalo mkalitazame.
 
Mzaramo wangu ananiambia kwao Maneromango kuna mganga anaweza kunitoa hiki kitambi ambacho ni kama nina mpira wa madaso, au kinyengo au chandimu ndani ya tumbo.[emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…