Kitambi kimeharibu muonekano wangu, wadada hawanitaki tena

Kitambi kimeharibu muonekano wangu, wadada hawanitaki tena

Hivi nikisema nifunge kula, wiki nzima nisile kitu wala kunywa, niwe nakunywa red wine tu ile ya kanisani iliyoombewa na Padre si kitambi kinaweza kuroweka kabisa?
Hapo ndo unajiongezea matatizo



Unapofunga kula unajitengenezea magonjwa kwasababu mwili unakua unatumia calories zilizohifadhiwa ndani ya mwili kama fat and proteias source of energy.
 
View attachment 2453416
Mimi ni handsome sana, mitaani kote wananisifu. Hata wanawake wananiambiaga. Lakini hawaachi kunikosoa tumbo langu hadi nimeanza kujichukia.

Kwa kweli nakosa sana raha, namtongoza msichana ananiambia na huo mtumbo wako kama umemeza kifaru cha jeshi ntakupeleka wapi mimi?

Six pack sio kwamba sijawahi kuwa nazo, nilikuwa nazo ila nikapata binti wa Kizaramo, asubuhi ananipa chai kikombe kimoja na andazi moja. Mchana hatuli anasema tubane matumizi.
Usiku anapika wali, maharage, nyama, mchicha, dagaa wa bukubuku, miguu ya kuku na supu ya mapupu inakuwepo.

Anasema kwanini tulale na njaa? Tunalala tukiwa tumeshiba sana hadi tunashindwa kupumua.

Tunajambiana huku tukikoroma, wachawi kila siku wanakuja kutukaba kwasababu ya kutuonea wivu mavitu tunayokula la kulala tukiwa tumeshiba matumbo ndiii.

Sasa wachawi wakanionea wivu six packs zangu, wakanuroga nimepata kitambi, sina six packs tena nina mtumbo mkubwa ambao ni single pack.

Mzaramo wangu ananiambia kwao Maneromango kuna mganga anaweza kunitoa hiki kitambi ambacho ni kama nina mpira wa madaso, au kinyengo au chandimu ndani ya tumbo.

Nimemkatalia nimemwambia JF kuna watalaam wa kila sekta.

Wanamitindo wenzangu, naombeni ushauri ili fashenista mwenzenu nirudie utanashati wangu.
To yeye, mzabzab, Baba Swalehe , Mwifwa naamini mtanisaidia
Kama unakunywa sana acha,kama hufanyi mazoezi bas nitakuwezesha...niruhusu tu tufanye wote😉
 
Hapo ndo unajiongezea matatizo



Unapofunga kula unajitengenezea magonjwa kwasababu mwili unakua unatumia calories zilizohifadhiwa ndani ya mwili kama fat and proteias source of energy.
Wale walokole wanafunga tatu kavu, usiku na mchana niki apply mbinu yao inaweza kunivusha?
 
Back
Top Bottom