Kitambi kimeharibu muonekano wangu, wadada hawanitaki tena

Dona ya madukani naiogopa sana. Huyu Mzaramo wangu yeye anasema kichwa chake ni kidogo, hawezi kujitwisha mahindi kwenda kusaga mashineni, kichwa chake kitapasuka.

Kuhusu pombe kuna m'babu mmoja anaitwa Asprin, kaniambia kaenda migombani kuwachanja ma eksi gelofrendi chanjo maalum, akirudi tukutane naye Family Bar pale Tegeta, hatua chache kutoka Kibo Mall. Mimi akinunua ntakunywa soda tu, ila nitashika li K Vant nipige nalo picha
bora iyo K vant kuliko soda bujibuji
 
nilikua nafululiza kula mayai ya kukaanga, 6+ kila siku, baada ya miezi 3 naona kitumbo ichoo kimechomoza, na kinaendelea kuchomoza

nilistop nikawa nayachemsha, wiki kadhaa kikapotea
naungana na comment #33 Oils/Fats
 
Aah kwan huna watoto au wasaidizi? Dona mbona easy tu hata mashineni unaeza enda direct unapata

Soda pia sio nziri mkuu soda moja unaeza pata hata kg 1 ya sukari hii unayochemshia chai

More Water less Soda
"Soda pia sio nziri mkuu soda moja unaeza pata hata kg 1 ya sukari hii unayochemshia chai"

Hii inawezekanaje??? Mana soda moja inauzwa 600 afu sukari kilo moja inauzwa 2800. Kama kika soda moja ina kilo ya sukari je wanapataje faida?
 
Aah kwan huna watoto au wasaidizi? Dona mbona easy tu hata mashineni unaeza enda direct unapata

Soda pia sio nziri mkuu soda moja unaeza pata hata kg 1 ya sukari hii unayochemshia chai

More Water less Soda
Yaani kunywa soda moja ni sawa na kula sukari kilo moja?
 
View attachment 2453416
Mimi ni handsome sana, mitaani kote wananisifu. Hata wanawake wananiambiaga. Lakini hawaachi kunikosoa tumbo langu hadi nimeanza kujichukia.

Kwa kweli nakosa sana raha, namtongoza msichana ananiambia na huo mtumbo wako kama umemeza kifaru cha jeshi ntakupeleka wapi mimi?

Six pack sio kwamba sijawahi kuwa nazo, nilikuwa nazo ila nikapata binti wa Kizaramo, asubuhi ananipa chai kikombe kimoja na andazi moja. Mchana hatuli anasema tubane matumizi.
Usiku anapika wali, maharage, nyama, mchicha, dagaa wa bukubuku, miguu ya kuku na supu ya mapupu inakuwepo.

Anasema kwanini tulale na njaa? Tunalala tukiwa tumeshiba sana hadi tunashindwa kupumua.

Tunajambiana huku tukikoroma, wachawi kila siku wanakuja kutukaba kwasababu ya kutuonea wivu mavitu tunayokula la kulala tukiwa tumeshiba matumbo ndiii.

Sasa wachawi wakanionea wivu six packs zangu, wakanuroga nimepata kitambi, sina six packs tena nina mtumbo mkubwa ambao ni single pack.

Mzaramo wangu ananiambia kwao Maneromango kuna mganga anaweza kunitoa hiki kitambi ambacho ni kama nina mpira wa madaso, au kinyengo au chandimu ndani ya tumbo.

Nimemkatalia nimemwambia JF kuna watalaam wa kila sekta.

Wanamitindo wenzangu, naombeni ushauri ili fashenista mwenzenu nirudie utanashati wangu.
To yeye, mzabzab, Baba Swalehe , Mwifwa naamini mtanisaidia
Punguza kula michembe,maparachichi,supusupu na furu.😂😂😂😂
 
Hayo mayai hayakujazi gesi tumboni?hayakukinai?
Mayai sita ni mengi mbona
mvivu kupika, so nikipiga mayai mengi ( na wanga ) na-survive masaa mengi
kuhusu gesi usiku kama kawa, ni mwendo wa bombings tu kama za Kyiv
 
😆😆😆😆😆😆😆😂😂😂😂😂😂 Nilitka nishangae,mayai yakuache salama
 
Shida kubwa ya kitambi ni kwenye tendo la ndoa. Ukiwa na kitambi halafu mwanamke akuambie umemjeruhi vizuri ujue amekuheshimu Sana na hela yako anaihitaji Sana.
 
View attachment 2453416
Mimi ni handsome sana, mitaani kote wananisifu. Hata wanawake wananiambiaga. Lakini hawaachi kunikosoa tumbo langu hadi nimeanza kujichukia.

Kwa kweli nakosa sana raha, namtongoza msichana ananiambia na huo mtumbo wako kama umemeza kifaru cha jeshi ntakupeleka wapi mimi?

Six pack sio kwamba sijawahi kuwa nazo, nilikuwa nazo ila nikapata binti wa Kizaramo, asubuhi ananipa chai kikombe kimoja na andazi moja. Mchana hatuli anasema tubane matumizi.
Usiku anapika wali, maharage, nyama, mchicha, dagaa wa bukubuku, miguu ya kuku na supu ya mapupu inakuwepo.

Anasema kwanini tulale na njaa? Tunalala tukiwa tumeshiba sana hadi tunashindwa kupumua.

Tunajambiana huku tukikoroma, wachawi kila siku wanakuja kutukaba kwasababu ya kutuonea wivu mavitu tunayokula la kulala tukiwa tumeshiba matumbo ndiii.

Sasa wachawi wakanionea wivu six packs zangu, wakanuroga nimepata kitambi, sina six packs tena nina mtumbo mkubwa ambao ni single pack.

Mzaramo wangu ananiambia kwao Maneromango kuna mganga anaweza kunitoa hiki kitambi ambacho ni kama nina mpira wa madaso, au kinyengo au chandimu ndani ya tumbo.

Nimemkatalia nimemwambia JF kuna watalaam wa kila sekta.

Wanamitindo wenzangu, naombeni ushauri ili fashenista mwenzenu nirudie utanashati wangu.
To yeye, mzabzab, Baba Swalehe , Mwifwa naamini mtanisaidia
Huyu ni Mnyantuzu. Naomba nirekebishwe kama nimekosea. Wanyantuzu wanajulikana tu kwa mwonekano. Ama la, nimsukuma.
 
Back
Top Bottom