Da Lu
JF-Expert Member
- Jul 18, 2016
- 1,209
- 2,840
Habari za muda huu wapendwa...
Kuna tatizo la sasa la wanawake baada ya kujifungua tu, utakuta mtu anafumuka kama anakula amira.
Mwaka jana mwezi wa 1 nilibahatika kupata baby boy lakini kwa njia ya operation baada ya kukaa hospitali siku 3 lakini njia iligoma kufunguka nilimshukuru Mungu kutoka salama mimi na mwanangu, lakini nilikua na mawazo sana nikifikiria jinsi nitakavyozidi kufutuka na huu mwili wangu na tumbo litakavyozidi kua kubwa.
Nilivyoruhusiwa tu kurudi nyumbani nilifunga tumbo langu kwa chini niligoma kabisa kula mamtori na masupusupu, chakula changu ni chai ya viungo ya moto, uji mwepesi wa moto, ugali lain na maini, matunda hasa matikiti maji nilikua natafuna na mbegu zake kabisa kwa kweli yalikua yananisaidia kuondoa gesi tumboni.
Sasa mwanangu ana mwaka na miezi ukiambiwa nimezaa kwa operation huwezi amini utakuta mtu mwingine amezaa basi amepoteza mvuto wote kawa kama asha boko, hii inaweza ikafanya Mr kushindwa kuongozana na wewe au kupoteza kabisa ashki ya mapenzi juu yako wanawake wenzangu tujitahidini kuwa wasafi wakati wote na tupende miili yetu.
Ni hayo tu..