Kitambi na mwanaume wa Kitanzania

Kitambi na mwanaume wa Kitanzania

Sio kila mwenye tumbo lililotokeza mbele ni kitambi, wengine ni sababu ya constipation, constipation ikiisha utashangaa na tumbo linaisha.
 
Huyo chriss christie hapo ana hela sijui kwann asiende kufanya surgery aondoe kitambi hicho na mazoezi yaani anauwezo hata wakua na mtu wa mazoezi private
inawezekana anaogopa gharama, atapata hasara
 
Wanaume wengine wanaamini eti kitambi ni heshima!!@!
 
Nimeona vitambi hapo mpaka nimeogopa sasa vipi kwenda kuvaa soksi mguu wakati wa asubuhi nadhani ukweli ni kero.
 
kiukweli mimi ninacho na sio mvivu. napiga kazi haswaa. sikitaki lakini kipo tu. nishaurini basi nifanyeje?

Unajua unauliza watu wenye mtindio wa elimu kwa hiyo majibu utakayopata ni rahisi rahisi sana!Wengi hawajui kuwa kuna watu hata ufanyeje huwezi kuondoa obesity na ukiendelea kupigana na hiyo hali unaweza ukawa hata kichaa.Je umewahi kujiuliza kuhusu gigantism?Kuna yule mcheza mieleka mjapan yeye naye hafanyi mazoezi?Kuna mtu aaliwahi kusema ni rahisi sana kuwa tajiri kuliko ambavyo ni ngumu kuwa maskini!ukimuuliza kivipi mbona maskini ni wengi sasa?atakupa principle za kuwa tajiri sasa unaweza kuniambia matokeo yake yatakuwaje!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Ukienda bush vitambi ni kama hakuna, na hata wanaoshinda wwakicheza bao, hawana vitambi. WHY?

Ni msosi. Mlo mmoja kwa siku, mafuta mpaka siku ya sikukuu ukipikwa wali na maharage. Sukari mpaka mwezi wa ramadhani; vitambi vitoke wapi?

Kina mama,r every other day wanapanda milima kmutafuta kuni (6 hrs walk) bado kuchota maji daily na shamba kipindi cha kulima na kuvuna.

Hivyo kwa bongo vitambi vibahusiana na pesa, uwezo wa kula milo 3 kwa siku, elimu duni ya makundi ya chakula na athari zake, kutoona au kutojua faida ya mazoezi au uvivu (naangukia kundi hili) na kutochukia vitambi.

Kwa ufupi vitambi ni mafuta ya ziada yaliyotunzwa kwa matumizi ya baadaye. Neno kubwa ni ZIADA, ili uondoe kitambi basi unguza hayo mafuta ya ziada kwa kujizuia kuongeeza carbs na fat kupitia chakula. Na utumie zaidi kwa kufanya mazoezi au hata kazi (kulima, kubeba mizigo, kutembea badala ya kukodi taxi au kuweka gas kwa gari. With time kitambi kitaisha.
Ukishapata size/shape uitakayo maintain it kwa kubalance carbs unazokula ziwe sawa na unazounguza kwa shughuli zako za kila siku.
 
Sasa wewe unataka kutukanwa na watanzania wenzako, yaani unadhalilisha black americans wakati wenzako wanaona ujiko kufananishwa nao hapa Bongo? Mtu kama huyo Rick Ross hapa Tanzania ni mwisho, yaani popularity yake ya kunuka mdomo na kuwa na kitambi cha kijinga inashinda hata Kikwete na chama chake. Ukimuuliza kwanini wewe unanuka mdomo na kuwa na mtambi kama kifaru anakujibu, 'Uhhh?'
 
Ukienda bush vitambi ni kama hakuna, na hata wanaoshinda wwakicheza bao, hawana vitambi. WHY?

Ni msosi. Mlo mmoja kwa siku, mafuta mpaka siku ya sikukuu ukipikwa wali na maharage. Sukari mpaka mwezi wa ramadhani; vitambi vitoke wapi?

Kina mama,r every other day wanapanda milima kmutafuta kuni (6 hrs walk) bado kuchota maji daily na shamba kipindi cha kulima na kuvuna.

Hivyo kwa bongo vitambi vibahusiana na pesa, uwezo wa kula milo 3 kwa siku, elimu duni ya makundi ya chakula na athari zake, kutoona au kutojua faida ya mazoezi au uvivu (naangukia kundi hili) na kutochukia vitambi.

Kwa ufupi vitambi ni mafuta ya ziada yaliyotunzwa kwa matumizi ya baadaye. Neno kubwa ni ZIADA, ili uondoe kitambi basi unguza hayo mafuta ya ziada kwa kujizuia kuongeeza carbs na fat kupitia chakula. Na utumie zaidi kwa kufanya mazoezi au hata kazi (kulima, kubeba mizigo, kutembea badala ya kukodi taxi au kuweka gas kwa gari. With time kitambi kitaisha.
Ukishapata size/shape uitakayo maintain it kwa kubalance carbs unazokula ziwe sawa na unazounguza kwa shughuli zako za kila siku.

Hivi The Boss kitambi chake kimetokana na mpangilio mbovu wa mlo au uvivu wa kufanya mazoezi?
Kuna wanawake 'wengine' wanasema vitambi vinawa-turn on!!!
 
Last edited by a moderator:
kiukweli mimi ninacho na sio mvivu. napiga kazi haswaa. sikitaki lakini kipo tu. nishaurini basi nifanyeje?

epuka junky foods , vyakula vya nyama nyama na mafuta mengi...........

ukimaliza kula usilale mpaka masaa mawili yapite ,,,,,,,,,,,,,,,,

fanya mazoezi na kunywa maji mengi...............

usisahau kutupia Grants na konyagi , achana na mibeer
 
Back
Top Bottom