Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Ndugu yangu ni mkulima wa jembe la mkono. Analima shamba lake na analimia watu ili kupata pesa ya sukari na sabuni. Kuna siku kazi za kulimia watu zinakosekana. Ikifika hali hii mke wake anadamka alfajiri kuwahi soko la matunda. Ananunua ndizi na machungwa anatembeza kwenye beseni lake kichwani
Mtaji wake ni sh 10,000 na ikifika jioni anakuwa amepata sh 15,000. Hii ni pesa ya kununua unga na mboga akapikie familia. Fikiria huyu mama ili atembeze beseni lake la ndizi na machungwa inabidi anunue kitambulisho cha mjasiliamalu 20,000.
Mama huyu siku za mvua hawezi kufanya biashara. Katika faida anayopata inabidi aweke kidogo senti zitakazosaidia siku akikosa biashara pia watoto wakiugua.