Kitambulisho cha Mjasiriamali kilivyoleta mateso katika jamii

Kitambulisho cha Mjasiriamali kilivyoleta mateso katika jamii

Unamlaumu sky ushawahi fanya biashara wewe,unajua mama anaepika maandazi anapata faida isiyozidi 1000tu kwa siku,Tena hapo maandazi yaishe,huyu atapata lini 20000 ya kulipia kitambulisho? Elfu moja inatosha kwa mahitaji ya siku ya mtanzania? Au unadhani wanapata hela nyingi Sana?
Acha uongo maandazi ya unga nusu kilo (sh 800) yana faida ya sh kati ya 2500 hadi elfu 2000 ( bila gharama za uendeshaji ) kwa siku. Sasa kwa mwezi hiyo 2000 ni elfu kama mtu atapika nusu kilo( wengi hua wanapika kuanzia kilo moja na nusu) maana yake kwa mwezi atapata 60000, kwa mwaka ni 720000, hii ni faida bila gharama ya mtaji, hapo atoe elfu 20 anabaki na laki 7 kama mtaji.

Tofauti na zamani tulipokua tunalipia 500 kila siku ambayo ni 500 x 30 x 12= 180000/= .Hili jambo liachine tu halina matobo. Watu tunajua wapi tumetoka na watoza ushuru.
 
Hizi 20K zimeingia kwenye mfuko gani manake inasemekana Kwenye fuko kuu "Hazina "Hazipo.Halafu Jiwe alishasema ni hiyari,Ingawa si Kweli.Inakuwaje wewe unatokwa povu hapa?
'halafu jiwe alishasema ni hiari'
 
Wewe mama huna point hapa. Kama kwa siku anaingiza 5000, kwa mwaka anaingiza 1,590,000/=. Kuna ubaya gani akichangia 20,000 kwa mwaka kwa ajili ya ulinzi wa nchi, huduma za jamii na miundombinu kwa manufaa yetu wenyewe?

Wenzetu huko mbele huona fahari kulipa kodi, sisi tunaona ni adhabu.

Chadema mtajenga nchi kwa fedha kutoka wapi? Kodi mmsema mnafuta, madini mnaweka rehani. Au misaada ya kuhimiza ushoga?
Moja ya matatizo lukuki anayokabiliwa mlipa Kodi wa Tanzania.

Ulipoamviwa tu anaweza kuingiza 5000 kwa Siku mama huyo anayotoka kuuza mboga ,wewe bila kutumia common sense umeichukua Kama ilivyo na kuizidisha Mara mwaka, hujazingatia jumapili hujazingatia Kuna Siku biashara inakuwa mbovu anapata hasara n.k yaani maingizo ghafi wewe ndio umeyachukua Kama kikokotoo Cha kodi
 
Ndugu yangu ni mkulima wa jembe la mkono. Analima shamba lake na analimia watu ili kupata pesa ya sukari na sabuni. Kuna siku kazi za kulimia watu zinakosekana. Ikifika hali hii mke wake anataka alfajiri kuwahi soko la matunda. Ananunua ndizi na machungwa anatembeza kwenye beseni lake kichwani.

Mtaji wake ni sh 10,000 na ikifika jioni anakuwa amepata sh 15,000. Hii ni pesa ya kununua unga na mboga akapikie familia. Fikiria huyu mama ili atembeze beseni lake la ndizi na machungwa inabidi anunue kitambulisho cha mjasiliamalu 20,000.

Mama huyu siku za mvua hawezi kufanya biashara. Katika faida anayopata inabidi aweke kidogo senti zitakazosaidia siku akikosa biashara pia watoto wakiugua.
Huyu mama hana watoto wanaoweza kumtafutia elfu 20 ya kitambulisho? Au ni kutafta huruma ya kijinga?

Ukilipishwa 1,000 kila siku na manispaa kwa mwaka mzima na ukalipa 20,000 mara moja kwa mwaka mzima kipi ni afadhali?

1,000*365 = 365,000
20,000*1= 20,000

Kipi ni nafuu?
 
Sky Eclat kulipa hao akina wachuuzi wadogo hapo kabla walikuwa wakilipa kwa siku ushuru wa shilingi 100/= hadi 500/= kwa siku kutegemea na halmashauri. Hapo bado 100/= nyingine kwa siku kama ushuru wa usafi. Piga hesabu kwa mwezi tu alikuwa analipa shilingi ngapi?

Baada ya kuingia Rais Magufuli akaagiza walipe 20,000/= tu kwa mwaka kupitia vitambulisho vya mjasiriamali.

Kwa muktadha huo juu, nani anawatetea wajasiriamali; Lissu au Magufuli? Wajasiriamali, za kuambiwa changanya na zako!!!
Mtu Ni machinga analipa ushuru wapi,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chadema ni wapuuzi Sana,hoja zao za kijinga jinga.

Hebu pita kwa wamachinga useme hili wakupasue ukauguzwe na nyumbu wenzio wa ufipa.

Hujui hata ukombozi wa hivi vitambulisho kwa wamachinga.
 
Kuchangia chochote kwenye nchi yako ni fahari kubwa. 20K kwa mwaka ni Sawa na 1800 approx kwa mwezi, na 56Tsh kwa siku. Ni program inayofaa na nyepesi zaidi kwa mjasiriamali kuliko ile inayotozwa holela masokoni. Ila hapa uliandika, ili ionekane Serikali ya JPM inawanyanyasa wajasiriamali, sio Sawa hata kidogo.
Mjifunze kuvaa viatu vya umasikini, hii itakufanya uwaonee huruma japo kidogo, Kuna watu hiyo 20000 ni mzigo mkubwa na haipatikani kirahisi, na anaweza akapitisha miezi hajaishika 20000 ya pamoja , kuchangia kweli ni fahari Ila sio Kila mtu yupo kwenye position hiyo
 
Huyu mama hana watoto wanaoweza kumtafutia elfu 20 ya kitambulisho? Au ni kutafta huruma ya kijinga?

Ukilipishwa 1,000 kila siku na manispaa kwa mwaka mzima na ukalipa 20,000 mara moja kwa mwaka mzima kipi ni afadhali?

1,000*365 = 365,000
20,000*1= 20,000

Kipi ni nafuu?
Huyu mama ana watoto wadogo, ninachoona hapa ni kuwa huyu mama anazidi kukandamizwa. Waliopaswa kulipa 20,000 wawe wenye mitano kuanzia 100,000
 
Wapi wanatibiwa bure?
Wanajifungua bure? Andika uhalisia weka pembeni mahaba ya chama
Vituo vyote vya serikalii, kiwango wanachochangia hakilingani na garama za hospitali binafsi. Chanzo zote ni buree, huduma za wajawazito ni buree, hata kama akiambiwa achangie bado nikiwango kidogoo saana ukiilinganisha na hospitali za watu binafsi
 
Huyu mama ana watoto wadogo, ninachoona hapa ni kuwa huyu mama anazidi kukandamizwa. Waliopaswa kulipa 20,000 wawe wenye mitano kuanzia 100,000
Wewe kwanini usimlipie sasa hio 20,000 ili umuondoe kwenye hio adha?
 
Unamlaumu sky ushawahi fanya biashara wewe,unajua mama anaepika maandazi anapata faida isiyozidi 1000tu kwa siku,Tena hapo maandazi yaishe, huyu atapata lini 20000 ya kulipia kitambulisho? Elfu moja inatosha kwa mahitaji ya siku ya mtanzania? Au unadhani wanapata hela nyingi Sana?
Wewe ni wale wale nyumbu mnaojipa tumaini feki, hamna mlijualo na mnadhihirisha chuki zenu tu Bila kufanya uchunguzi.Eti mandazi yauzwe faida buku.

Ushawahi hata kukanda unga wa mandazi wewe?

Inakua hata yanavyochomwa,au mnataka kujidai kuvaa uhusika bandia
 
Kumbukeni mjasiriamali naye anafamilia, inayosomeshwa bure na kujifungua bure kwenye hospitali na shule za serlikali, hivyo na yeye kwa sehemu yake ndogo ya kipato anawajibu wa kuchangia maendeleo ya taifa. Kwani mjasilia mali huyohuyo, anahitaji barabara ya lami, umeme wa uhakika, maji, ulinzi wa vyombo vya dola, matibabu hospitalini , n.k, n.k. Hivyo anawajibu wa kuchangia sehemu ndogo ya pato lake kama mtanzania. Kwahiyo kuja kubwabwaja hapa eti kitambulisho cha mjasiliamali ni mateso, huu ni uelewa wako mdogoo saanaa. Na kwa hali hiiii husitahili hata kuwa kiongozi wa familia. Maendeleo ya taifa lolote, yanajengwa na wanataifa lile kwa kuzingatia uwezo wao wa kipato chao.
Watu wanatibiwa bure na kujifungua bure kwenye hospitali ipi mkuu? Nami nifunge safari ya huko?
 
Wewe mama huna point hapa. Kama kwa siku anaingiza 5000, kwa mwaka anaingiza 1,590,000/=. Kuna ubaya gani akichangia 20,000 kwa mwaka kwa ajili ya ulinzi wa nchi, huduma za jamii na miundombinu kwa manufaa yetu wenyewe?

Wenzetu huko mbele huona fahari kulipa kodi, sisi tunaona ni adhabu.
Chadema mtajenga nchi kwa fedha kutoka wapi? Kodi mmsema mnafuta, madini mnaweka rehani. Au misaada ya kuhimiza ushoga?
Hii Nchi bado haijafika huku tatizo jamaa amefakamia miradi mingi kwa wakati mmoja na kusababisha maumivu kwa watu wengi sana.
 
Wewe kwanini usimlipie sasa hio 20,000 ili umuondoe kwenye hio adha?
Nikifa leo nitamuacha na dhiki Kama nitaanza kumlipia. Lakini ni halali kwake kulipa hiyo pesa ilhali mtaji wake ni mdogo na ana tafuta unga wa watoto.
 
Ndugu yangu ni mkulima wa jembe la mkono. Analima shamba lake na analimia watu ili kupata pesa ya sukari na sabuni. Kuna siku kazi za kulimia watu zinakosekana. Ikifika hali hii mke wake anataka alfajiri kuwahi soko la matunda. Ananunua ndizi na machungwa anatembeza kwenye beseni lake kichwani.

Mtaji wake ni sh 10,000 na ikifika jioni anakuwa amepata sh 15,000. Hii ni pesa ya kununua unga na mboga akapikie familia. Fikiria huyu mama ili atembeze beseni lake la ndizi na machungwa inabidi anunue kitambulisho cha mjasiliamalu 20,000.

Mama huyu siku za mvua hawezi kufanya biashara. Katika faida anayopata inabidi aweke kidogo senti zitakazosaidia siku akikosa biashara pia watoto wakiugua.
Machadema shida Sana nchi hii, kila mkiamka mnawaza kupinga pinga tuu. Mnatafuta mpinge Nini badala ya kuwaza mambo ya maendeleo yasaidie watanzania.
 
Wewe mama huna point hapa. Kama kwa siku anaingiza 5000, kwa mwaka anaingiza 1,590,000/=. Kuna ubaya gani akichangia 20,000 kwa mwaka kwa ajili ya ulinzi wa nchi, huduma za jamii na miundombinu kwa manufaa yetu wenyewe?

Wenzetu huko mbele huona fahari kulipa kodi, sisi tunaona ni adhabu.
Chadema mtajenga nchi kwa fedha kutoka wapi? Kodi mmsema mnafuta, madini mnaweka rehani. Au misaada ya kuhimiza ushoga?
Sidhani kama wewe ni mfanyabiashara ama unajua misingi ya biashara....ukiingiza elfu tano kwa siku kwenye biashara ndani yake kuna
Mtaji
Matumizi
Faida
Tozo ama ushuru
Baki
Hapo kitambulisho ni nje ya hayo yote na kimechomekewa tu bila kuzingatia hali halisi ya wananchi
 
Back
Top Bottom