Kumbukeni mjasiriamali naye anafamilia, inayosomeshwa bure na kujifungua bure kwenye hospitali na shule za serlikali, hivyo na yeye kwa sehemu yake ndogo ya kipato anawajibu wa kuchangia maendeleo ya taifa. Kwani mjasilia mali huyohuyo, anahitaji barabara ya lami, umeme wa uhakika, maji, ulinzi wa vyombo vya dola, matibabu hospitalini, n.k, n.k.
Hivyo anawajibu wa kuchangia sehemu ndogo ya pato lake kama mtanzania. Kwahiyo kuja kubwabwaja hapa eti kitambulisho cha mjasiliamali ni mateso, huu ni uelewa wako mdogoo saanaa. Na kwa hali hiiii husitahili hata kuwa kiongozi wa familia. Maendeleo ya taifa lolote, yanajengwa na wanataifa lile kwa kuzingatia uwezo wao wa kipato chao.