Kitambulisho changu cha NIDA Kinafutika Kila siku. Je wanaweza kuniprintia kipya.

Kitambulisho changu cha NIDA Kinafutika Kila siku. Je wanaweza kuniprintia kipya.

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
9,514
Reaction score
23,523
Hapa nakitambulisho cha mpiga kura tangu 2015 hakina hitilafua hata nukta.

Miezi kadhaa iliyopita nimepokea kitambulisho changu cha NIDA. Tena nawashukuru maana aliniletea mjumbe wangu wa Nyumba KUMI wa Chama cha Mapinduzi.
NIDA Tanzania
Jambo ambapo sijapenda haijapita hata mwaka herufi zinabanduka. Naenda kukitumia watoa huduma wanakikataa maana umri tarehe inaonekana nusu, jina herufi mbili hazipo.

Nimeamua kukiweka pembeni ili kisiaharibike zaidi. Maana hata ukikiweka kwenye Wallet kikiguswa kidogo tu maandishi yanapukutika.


Nauliza kama ninaweza kubadilishiwa na kupewa kingine Bora au Hadi nipitie mchakato ule ule wa mwanzo?

Nauliza hapa public ili iwe faida KWA wengine.
 
Hapa nakitambulisho cha mpiga kira tangu 2015 hakina hitilafua hata nukta.

Miezi kadhaa iliyopita nimepokea kitambulisho changu cha NIDA. Tena nawashukuru maana aliniletea mjumbe wangu wa Nyumba KUMI wa Chama cha Mapinduzi.
NIDA Tanzania
Jambo ambapo sijapenda haijapita hata mwaka herufi zinabanduka. Naenda kukitumia watoa huduma wanakikataa maana umri tarehe inaonekana nusu, jina herufi mbili hazipo.

Nimeamua kukiweka pembeni ili kisiaharibike zaidi. Maana hata ukikiweka kwenye Wallet kikiguswa kidogo tu maandishi yanapukutika.


Nauliza kama ninaweza kubadilishiwa na kupewa kingine Bora au Hadi nipitie mchakato ule ule wa mwanzo?

Nauliza hapa public ili iwe faida KWA wengine.
Nenda ofisi za nida iliyokaribu nawe
 
Sijajua ni baada ya muda gani, ila utaratibu wake ni kama mtu aliepoteza kitambulisho. Kwahiyo ukienda NIDA utapewa control namba ya kulipia.
Ila KWA nini nilipoe gharama ambayo walitakiwa kulipa wao kunitengekezea kitu kisicho na kiwango. Yaani hata Sasa hivi nikisema nifute na kidole jina lote linafutika.

Ila kama ni kuchangia gharama za printing KWA sababu mwanzoni nilipata Bure hapo sawa.
 
Hivi vitambulisho sijui waliviprint kwa technology gani yan vingi vyao maandishi yanafutika na bado vipya kabisa...

Hapa kulikua na upigaji mkubwa sana.
Hapo kweli walitukosea. Warekebishe hiyo KWA vingine vijavyo maana NIDA ni ishu siriasi.
 
Hivyohivyo chakwangu nilikiweka kwenye wallet kwa muda mrefu kidogo na sikuwa nimekiangalia kwa mda, siku nimekikagua kimekuwa kama Kadi ya refa, afadhali Cha mpiga kura.
Hilo warekebishe. Vitu vya kitaifa vinatakiwa KUWA vimenyooka kuonyesha nchi Iko siriasi.
 
Ila KWA nini nilipoe gharama ambayo walitakiwa kulipa wao kunitengekezea kitu kisicho na kiwango. Yaani hata Sasa hivi nikisema nifute na kidole jina lote linafutika.

Ila kama ni kuchangia gharama za printing KWA sababu mwanzoni nilipata Bure hapo sa
Unashanga Hilo!! Kuna watu kwenye fomu waliandika majina yao vizuri kabisa ila kitambulisho linatoka majina yamekosewa. Ukienda ili urekebishe unatakiwa utoe elfu 20.
 
Mimi changu kimekuja kimefutika vitu vingi hadi sehemu ya picha Kuna mikwaruzo.

Kwa ufupi vitambulisho vyetu vya Nida Quality yake ndogo havina Uimara kabisa.
Ukienda ofisi za nida wanakubadilishia ila andaa elfu 20 ndani ya wiki unakipata kipya
 
Back
Top Bottom