Hapa nakitambulisho cha mpiga kura tangu 2015 hakina hitilafua hata nukta.
Miezi kadhaa iliyopita nimepokea kitambulisho changu cha NIDA. Tena nawashukuru maana aliniletea mjumbe wangu wa Nyumba KUMI wa Chama cha Mapinduzi.
NIDA Tanzania
Jambo ambapo sijapenda haijapita hata mwaka herufi zinabanduka. Naenda kukitumia watoa huduma wanakikataa maana umri tarehe inaonekana nusu, jina herufi mbili hazipo.
Nimeamua kukiweka pembeni ili kisiaharibike zaidi. Maana hata ukikiweka kwenye Wallet kikiguswa kidogo tu maandishi yanapukutika.
Nauliza kama ninaweza kubadilishiwa na kupewa kingine Bora au Hadi nipitie mchakato ule ule wa mwanzo?
Nauliza hapa public ili iwe faida KWA wengine.