Kitanda kinamalizwa na wadudu. Mwenye kujua dawa tafadhali

Kitanda kinamalizwa na wadudu. Mwenye kujua dawa tafadhali

Nchi Kavu

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2010
Posts
4,290
Reaction score
2,468
Wakuu za muda. Kuna hawa wadudu weupe hivi kama wale wa kahawa, wanakula mbao hatari. Sasa nawasikia kila leo wanakula kitanda na huwa nawachokona hadi kuwapata na kuwaangamiza ila bado wanazaliana. Mwenye kujua dawa anijulishe tafadhi

IMG_20210904_225117.jpg

IMG_20210904_225138.jpg
 
Ndugu yangu nikwambie tu ukweli, hicho kitanda kwisha habari yake. Utahangaika sana lakini, hao wadudu huwa wazazimia kwa muda tu kisha utawasikia tena wanafanya yao.

Chonga kitanda kwa mbao ngumu kama mninga (kuwa makini usiibiwe kwa mininga feki) au nunua cha chuma.

Pia hiyo iwe fundisho pale utakapokuwa unapauwa nyumba yako, hata wauza mbao wakushawishi vipi kuwa ziko treated usikubali, nunua dawa wazi treat upya mbele ya macho yako.
 
Bendera chuma, Mlingoti chuma na upepo chuma, na ikiwezekana godoro chuma
Hapo chumbani asitumie umeme shoti ikigusa kitandani, vyuma hupokea yeye na shemeji kwishne! Bora atumie kibatali nyumba ikiungua, hana hasara coz vyuma haviungui.
 
Ndugu yangu nikwambie tu ukweli, hicho kitanda kwisha habari yake. Utahangaika sana lakini, hao wadudu huwa wazazimia kwa muda tu kisha utawasikia tena wanafanya yao.

Chonga kitanda kwa mbao ngumu kama mninga (kuwa makini usiibiwe kwa mininga feki) au nunua cha chuma.

Pia hiyo iwe fundisho pale utakapokuwa unapauwa nyumba yako, hata wauza mbao wakushawishi vipi kuwa ziko treated usikubali, nunua dawa wazi treat upya mbele ya macho yako.
Pamoja sana mkuu. Ila inavyoonekana wanakula cover ya juu kama unavyoona hapo. Ndani kabisa hawajagusa
 
Back
Top Bottom