Uchaguzi 2020 Kitanzi cha CCM Kawe: Watia nia 176 wa ubunge dhidi ya Halima Mdee CHADEMA

Wewe unajua uchawi tuu hesabu wala huzijui... tufanye tuu kwa mfano hapo kawe Halima mdee amepigiwa na wajumbe 71 halafu papo hapo watia nia tuu wa CCM hapo kawe wameshafika 120 yani zaidi ya wajumbe walio mpigia kura Mdee! Kwa kifupi tuu....Kawe kuna wana chama wa CCM wengi kuliko chadema ba uwezekano wa CCM kulipata jimbo hilo ni mkubwa sana kuliko chadema......


Halafu wana CCM kujitokeza wengio sio kawe tuu ni majimbo mengi ya Dares-salaam na ni demokrasia...
 

Napata tabu kuelewa kuhusu maana halisi ya neno Demokrasia, neno uhuru wa mtu binafsi, neno uwazi, neno maamuzi nk

Napata tabu sana Leo mwezi wa saba, mwanachama wa CHadema badala ya kunadi sera na matarajio ya wagombea wa chama chake, yeye anajadili kuhusu watia nia tu. Deductively Hapo Ni wanachama 80 wa hiyo CCM and so hiyo CCM Ina idadi kubwa ya wanachama.

Napata Shida mpinzani anashindwa kuonyesha kwa data Mafanikio ya mbunge Wake aliyekuwa Hapo ili watu waelewe why wamchague,!wewe sio tu kwamba unaandika yasiyokuhusu Lakini pia unaweka na mipasho. Then unaitaka Tz iendelee.

Watanzania Ni Nini Priorities zenu. Mipasho au maendeleo. Huwezi kuwa na yote hasa kwa watz wavivu na wapiga majungu as if uchaguzi unafanyika kila mwaka. Ukiingiia Insta ndo utajua mind za watz na Sasa JF. Kila mtu anajua kuongea Tz. It’s time kuongelea mikakati zaidi kuliko watu. Mdee amefanya Nini? Hao watu wa Kawa wamchague MDEEE kwa nini nk. Emperical evidence.

Mwisho wa siku utaskia Kura zimeibiwa Lakini hamsemi kwa sifa gani za mgombea. Sasa mmeanza kuhusu Mdee. Kafanya Nini.
 
Karibu upate tiba
 
Mdee amegombea nafasi ya jimbo na nafasi ya vitu maalum; ni kweli kwamba CHADEMA wanajua kitakachotokea na wamejiandaa tayari. Ni hakika kwamba Mdee atapoteza jimbo mbele ya mzee wa Amfifiro na yeye anatinga bungeni kwa tiketi ya viti maalum.
 
Mdee angefanya kama Mnyika na Kubenea tu. Kawe na majimbo mengine ya Dar yapo kimkakati, hata kwa faulu tatanishi lazima mengi yaende kwa mataga.
 
Unaweza kusema kwamba wamechukua fomu ili kujenga majina kwa awamu ijayo lakini utajengaje jina kati ya watu 80
 
Watia nia wengi wenye njaa wengi. katika kugombea basi lazima kusumana kuumia si ajabu!
 
Tunaomba Karatasi Majina ya Wagombea wote isije ikawa ni Propaganda!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…