Uchaguzi 2020 Kitanzi cha CCM Kawe: Watia nia 176 wa ubunge dhidi ya Halima Mdee CHADEMA

Uchaguzi 2020 Kitanzi cha CCM Kawe: Watia nia 176 wa ubunge dhidi ya Halima Mdee CHADEMA

Mshana Jr kwa Maandalizi na Mikakati niliyoiona na ninayoiona kwa 2020 hii, Afe Mmaasai au Mmang'ati CCM analichukua Jimbo la Kawe rasmi.
Kwa kumsimamisha mcheza porno Gwaji au Mwijaku? Alitemeshwa kiazi cha Moto kipi ndio wataweza wacheza porno?
 
tuseme ukweli tu kwa jinsi binti Halima alivyoisumbua sirikali bungeni njia zote za halali na haramu zitatumika kumuengua, kama Halima akishinda itakuwa ule msemo Jitihada haishindi Kudura!! yaani Ngamia atapita kwenye tundu la sindano!!

Kuna muvi inaitwa Gladiator ambapo unajifunza humo kuwa mtazame vizuri adui yako kabla hujaingia nae vitani sababu itakusaidia kurudisha mpira kwa golikipa kama Mnyika

Halima itabaki stori aliwahi kuwa mbunge machachari wa Kawe!! hawezi kushinda by any means and she should start to prepare to face that reality and get used to it!!

pole sana for Halima, chadema and democracy!!

Very plausible. Naona hata hiyo idadi kubwa ya wagombea wa CCM ni kutokana na kuaminishwa kuwa mgombea wa CCM ndiye, automatically, atakuwa mbunge wa Kawe. Mbona imeshasemwa. Uchaguzi wa Mwaka huu utaamuliwa kwa mkono wa chuma (eti demokrasia inatuchelewesha!)

Huo wingi na miparurano ya wagombea wa CCM kwenye majimbo ni kiashiria tosha kuwa sasa mafisi yameona fursa kubwa na rahisi ya ulaji bungeni. Huhitaji ridhaa ya wananchi bali kete ni kumridhisha mtu mmoja na wapambe wake basi. Kwingine unapiga blabla za kawaida kwa malofa (wananchi!). Na kawaida yetu tutakuja kuamka tena wakati nchi iko kwenye deep s.h.
 
Mshana update taarifa mpaka jana usiku kulikuwa na wagombea 137 wa CCM jimbo la kawe.
[emoji44][emoji44][emoji44][emoji848][emoji848][emoji848][emoji144][emoji144][emoji144]hii sasa ni rekodi ya mpaka mwezini na Pluto
 
CCM ni jalala..Kila mtu anataka uongozi kwa sababu asilimia kubwa wanafanya biashara kharamu..wanataka walinde maslahi yao, wanakharamu hawa!!
 
Form ikitoka moja shida, zikitoka nyingi shida, binadamu Hatuna jema
 
Unaweza kuwa sahihi maana halima 2010 aliupata baada ya Katibu wa Mkoa wa CCM kuingiza jina la Kizigha kinyemela wanaCCM wakanuna na kumpa mdee.
Mdee anakubalika sana Kawe. Ni mtu wetu ni dada yetu na amefanya mambo mengi mazuri sana Kawe pamoja na figisu za ccm.
Tano tena kwa Mdee
 
[emoji44][emoji44][emoji44][emoji848][emoji848][emoji848][emoji144][emoji144][emoji144]hii sasa ni rekodi ya mpaka mwezini na Pluto
CCM watapiga pesa sana kwenye fomu , ukipiga laki laki nchi nzima kwa watiania inaweza kugonga 1.3B+ kwa Evarage ya kila Jimbo wagombea 50 na jumla ya majimbo 260+
 
Hiyo namba nne yako ndio inakwenda kutokea, watashindwa na mwanamke halafu hawataweza hata kuangaliana usoni. Huo wingi wa waliochukua fomu hautawaacha salama, lazima wapasuke makundi.

Japo wao wanaona sifa wengi kujitokeza kwenda kuchukua fomu, utadhani hizo fomu wanazichukulia mwezini.
Nilitamani Daudi Albert Bashite achukue fomu Kawe apambane na Mdee.
 
Hili linaweza kuwa ajabu lingine la dunia ama linaweza kuingia kwenye kitabu cha rekodi za dunia World Guinness Book of Records, ama linaweza kuvunja rekodi ya nchi na dunia kwa jimbo moja la ubunge kuwa na watia nia wengi kuwahi kutokea na karibia asilimia mia moja wa chama kimoja.

Pamoja na kwamba kibubu cha tume ya uchaguzi ya CCM kitatuna kwa mapato na pengine kuwa jimbo lililoingiza mapato mengi zaidi kwa kuuza form nyingi zaidi lakini madhara yake ni makubwa kuliko hayo mapato.

1. Katika watia nia wote hao 80 nina hakika hawapungui walau 20 wenye nguvu ya pesa, ushawishi ndani ya chama na wale wa mbeleko na vimemo. Kwa kuzingatia hili pekee tayari yatatokea makundi yasiyopungua 10 hivi. Makundi yenye nguvu na misuli ya kila aina. Hapa badala ya kupambana na adui yataanza kupambana yenyewe kwa yenyewe.

Jimbo la Kawe lililomegwa kutoka Kinondoni limekuwa na umaarufu mkubwa kuliko hata Kinondoni yenyewe na hii pengine ni kutokana na jiografia yake na aina ya mtu anayelishikilia.

3. CCM wanalitaka hilo Jimbo kwa hali na mali. Na wamewekeza muda mrefu sana tena kwa gharama kubwa mno. Hivyo kitendo cha kulikosa kitakuwa aibu kubwa, fedheha na hasara kubwa kisiasa.

4. Kitendo cha wanaume na uwekezaji wao wote kuja kushindwa na mwanamke mmoja ni ndoto ya kutisha sana na jinamizi wasilolipenda CCM

5. Kuonesha umwamba na ubabe kuwa wakitaka kitu hawashindwi kwakuwa wana kila kitu kila nyenzo ya kupata ushindi

Ni kwa muktadha huo wa kukamia kulikopitiliza hilo jimbo.. Wamejikuta wanatoa boko. Kwakuwa watatumia muda mwingi sana kwenye:
Mchujo
Kupata tano bora
Kwenye kupata mgombea mmoja
Kwenye kuunganisha makundi
Kwenye kuponya majeraha kabla ya uchaguzi

Kumbuka kila hatua kati ya hizo zote itaacha maumivu kwa kundi fulani
Ni wakati wakihangaika na yote haya Halima Mdee atakuwa busy kuimarisha himaya yake.

Matokeo yake ni nini? Muda utasema



huu ni mwaka wa kuizika rasmi ccm
 
Back
Top Bottom