Uchaguzi 2020 Kitanzi cha CCM Kawe: Watia nia 176 wa ubunge dhidi ya Halima Mdee CHADEMA

Uchaguzi 2020 Kitanzi cha CCM Kawe: Watia nia 176 wa ubunge dhidi ya Halima Mdee CHADEMA

mie hatra waweke jiwe na mdee jamani yule dada mshenzi sana bora ccm tu tujue moja hakuna alichofanya kwa 5 years
 
Dah...kibongobongo...kazi ya ubunge ndiyo kazi rahisi kukiko zote ....inahitaji sifa mbili tu ..kujua kusoma na kuandika...wakati Konda wa daladala lazima ajue na kuhesabu [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
umemsahau beki tatu anatakiwa ajue na kuosha vyombo pia
 
Hili linaweza kuwa ajabu lingine la dunia ama linaweza kuingia kwenye kitabu cha rekodi za dunia World Guinness Book of Records, ama linaweza kuvunja rekodi ya nchi na dunia kwa jimbo moja la ubunge kuwa na watia nia wengi kuwahi kutokea na karibia asilimia mia moja wa chama kimoja.

Pamoja na kwamba kibubu cha tume ya uchaguzi ya CCM kitatuna kwa mapato na pengine kuwa jimbo lililoingiza mapato mengi zaidi kwa kuuza form nyingi zaidi lakini madhara yake ni makubwa kuliko hayo mapato.

1. Katika watia nia wote hao 80 nina hakika hawapungui walau 20 wenye nguvu ya pesa, ushawishi ndani ya chama na wale wa mbeleko na vimemo. Kwa kuzingatia hili pekee tayari yatatokea makundi yasiyopungua 10 hivi. Makundi yenye nguvu na misuli ya kila aina. Hapa badala ya kupambana na adui yataanza kupambana yenyewe kwa yenyewe.

Jimbo la Kawe lililomegwa kutoka Kinondoni limekuwa na umaarufu mkubwa kuliko hata Kinondoni yenyewe na hii pengine ni kutokana na jiografia yake na aina ya mtu anayelishikilia.

3. CCM wanalitaka hilo Jimbo kwa hali na mali. Na wamewekeza muda mrefu sana tena kwa gharama kubwa mno. Hivyo kitendo cha kulikosa kitakuwa aibu kubwa, fedheha na hasara kubwa kisiasa.

4. Kitendo cha wanaume na uwekezaji wao wote kuja kushindwa na mwanamke mmoja ni ndoto ya kutisha sana na jinamizi wasilolipenda CCM

5. Kuonesha umwamba na ubabe kuwa wakitaka kitu hawashindwi kwakuwa wana kila kitu kila nyenzo ya kupata ushindi

Ni kwa muktadha huo wa kukamia kulikopitiliza hilo jimbo.. Wamejikuta wanatoa boko. Kwakuwa watatumia muda mwingi sana kwenye:
Mchujo
Kupata tano bora
Kwenye kupata mgombea mmoja
Kwenye kuunganisha makundi
Kwenye kuponya majeraha kabla ya uchaguzi

Kumbuka kila hatua kati ya hizo zote itaacha maumivu kwa kundi fulani
Ni wakati wakihangaika na yote haya Halima Mdee atakuwa busy kuimarisha himaya yake.

Matokeo yake ni nini? Muda utasema



Hii inaonyesha jinsi mpasuko ulivyo ndani ya CCM. Pamoja na mkwara wa M/Kiti kuwaonya wale aliyewateua katika nafasi mbali mbali kuchukua fomu, lakini ndio utitiri wa waliochaguliwa naye M/k. Hii inamaanisha wanaotaka kuleta siasa tofauti na zile zinazoendeshwa sasa hivi ni wengi.

Kumbuka kwamba wakati huu ndio wakati pekee na nyeti kwa kipindi cha miaka 4 na nusu mbwa kufunguliwa kamba yake. Na hakuna hakika kama kesho nafasi hiyo itatolewa tena, kwa hiyo kila mmoja anataka kuonyesha kaliona jua. Du, kumbe CCM ni wahanga wakubwa wa umwinywaji wa demokrasia.
 
Fomu ya juu kuliko zote imetoka, ikawa nongwa kwa majority. Form za watia nia ubunge zimekuwa utitiri, imekuwa nongwa pia. BTW, hiki ni chanzo kizuri cha mapato kwa hao CCM, mbona ya upande wa pili yanaumiza wengi? This is why huwa nasema kuitoa CCM madarakani inaweza kuwa ngumu kuliko, coz hata tunaosema tuko nje bado tunaiabudu na kuisujudia kwa maandiko na mabandiko yetu.
 
Mdee angefanya kama Mnyika na Kubenea tu. Kawe na majimbo mengine ya Dar yapo kimkakati, hata kwa faulu tatanishi lazima mengi yaende kwa mataga.
Jitahidi kujipa moyo kwani hautakuja amini.
 
Chadema Safari wawape kipaumbele wanawake wengi kuliko wanaume,ni rahisi kumnunua Malaya wa kiume kuliko wa kike.Pia wanawake ni strong kwenye mapambano ya kupinga unyanyasaji na udhalimu kuliko wanaume.
Wanaume watanunulika
 
yani ningekuwa raisi hawa ningezuia hata fomu wasipewe kabisa. kwa utaratibu wa sasa na uchukuaji fomu kupigana, ni kuthibitisha wahusika oxygen yao katika siasa ni vurugu,ugomvi na fitina. sasa ni kma samaki kahamishiwa nchi kavu wanalazimishana vurugu
Morogoro tayari wameshaanza kuparurana
View attachment 1508064
 
Ungwana ni kukubali kukosea, sikuwahi fikiri unafikra za kitoto namna hii. Good day.
Hapana hii ni mara ya nne unakosoa heading za mada zangu.. Na wewe peke yako.. Sasa unataka kunikosoa ila nikijaribu kukuweka sawa unamaind duu...
 
Back
Top Bottom