Uchaguzi 2020 Kitanzi cha CCM Kawe: Watia nia 176 wa ubunge dhidi ya Halima Mdee CHADEMA

Majimbo yote ya Dar yanarudi CCM.ndo maana kwa Dar watiania wa CCM ni wengi.kwa kila jimbo.maana yake CCM ikikupitisha tyr wewe ni mbunge.
 
Hili linaweza kuwa ajabu lingine la dunia ama linaweza kuingia kwenye kitabu cha rekodi za dunia World Guinness Book of Records, ama linaweza kuvunja rekodi ya nchi na dunia kwa jimbo moja la ubunge kuwa na watia nia wengi kuwahi kutokea na karibia asilimia mia moja wa chama kimoja.

Pamoja na kwamba kibubu cha tume ya uchaguzi ya CCM kitatuna kwa mapato na pengine kuwa jimbo lililoingiza mapato mengi zaidi kwa kuuza form nyingi zaidi lakini madhara yake ni makubwa kuliko hayo mapato.

1. Katika watia nia wote hao 80 nina hakika hawapungui walau 20 wenye nguvu ya pesa, ushawishi ndani ya chama na wale wa mbeleko na vimemo. Kwa kuzingatia hili pekee tayari yatatokea makundi yasiyopungua 10 hivi. Makundi yenye nguvu na misuli ya kila aina. Hapa badala ya kupambana na adui yataanza kupambana yenyewe kwa yenyewe.

Jimbo la Kawe lililomegwa kutoka Kinondoni limekuwa na umaarufu mkubwa kuliko hata Kinondoni yenyewe na hii pengine ni kutokana na jiografia yake na aina ya mtu anayelishikilia.

3. CCM wanalitaka hilo Jimbo kwa hali na mali. Na wamewekeza muda mrefu sana tena kwa gharama kubwa mno. Hivyo kitendo cha kulikosa kitakuwa aibu kubwa, fedheha na hasara kubwa kisiasa.

4. Kitendo cha wanaume na uwekezaji wao wote kuja kushindwa na mwanamke mmoja ni ndoto ya kutisha sana na jinamizi wasilolipenda CCM

5. Kuonesha umwamba na ubabe kuwa wakitaka kitu hawashindwi kwakuwa wana kila kitu kila nyenzo ya kupata ushindi

Ni kwa muktadha huo wa kukamia kulikopitiliza hilo jimbo.. Wamejikuta wanatoa boko. Kwakuwa watatumia muda mwingi sana kwenye:
Mchujo
Kupata tano bora
Kwenye kupata mgombea mmoja
Kwenye kuunganisha makundi
Kwenye kuponya majeraha kabla ya uchaguzi

Kumbuka kila hatua kati ya hizo zote itaacha maumivu kwa kundi fulani
Ni wakati wakihangaika na yote haya Halima Mdee atakuwa busy kuimarisha himaya yake.

Matokeo yake ni nini? Muda utasema

Kwanza nikusahihishe, Fomu zinazonunuliwa ni za CCM siyo za Tume. Hivyo wanaofaidika na huo utitiri wa wagombea ni CCM siyo Tume ya Uchaguzi.

Pili, kujitokeza kwa watia nia wengi ni ishara ya kuimarika kwa demokrasia ndani ya chama lakini pia ni imani kubwa waliyonayo watanzania kwa CCM kuliko vyama vingine. Na jambo kubwa ni kupungua kwa vitendo vya rushwa. Sasa hivi kila mmoja ana nafasi ya kuweza kuwa mgombea haijalishi una pesa ama la. Ili mradi tu ukubalike.

Tatu, Jimbo la Kawe lilikua lirudi CCM toka 2015. Lakini upepo wa Lowassa ulilinusuru Jimbo hilo pamoja na majimbo mengine ya Dar kubaki upinzani. Ndo maana Halima Mdee, kipindi kile alipewa Uenyekiti wa BAWACHA ili akilikosa jimbo hilo basi aingie Bungeni kwa mgongo wa BAWACHA kama Viti Maalum.

Mwisho, Halima Mdee hawezi kupanga himaya yake kwa wakati huu, halafu akashinda Uchaguzi. Kama hakuweza kuipanga kwa miaka 5 akiwa mbunge hawezi kuipanga kwa hii miezi miwili iliyobakia kuelekea uchaguzi Mkuu.
 
Bashite ana machale sana kakimbia zake Kigamboni...Kwa Halima hata Magu akigombea Kawe hawezi kushinda
 
Dah...kibongobongo...kazi ya ubunge ndiyo kazi rahisi kukiko zote ....inahitaji sifa mbili tu ..kujua kusoma na kuandika...wakati Konda wa daladala lazima ajue na kuhesabu [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwanza nikusahihishe, Fomu zinazonunuliwa ni za CCM siyo za Tume. Hivyo wanaofaidika na huo utitiri wa wagombea ni CCM siyo Tume ya Uchaguzi.

Pili, kujitokeza kwa watia nia wengi ni ishara ya kuimarika kwa demokrasia ndani ya chama lakini pia ni imani kubwa waliyonayo watanzania kwa CCM kuliko vyama vingine. Na jambo kubwa ni kupungua kwa vitendo vya rushwa. Sasa hivi kila mmoja ana nafasi ya kuweza kuwa mgombea haijalishi una pesa ama la. Ili mradi tu ukubalike.

Tatu, Jimbo la Kawe lilikua lirudi CCM toka 2015. Lakini upepo wa Lowassa ulilinusuru Jimbo hilo pamoja na majimbo mengine ya Dar kubaki upinzani. Ndo maana Halima Mdee, kipindi kile alipewa Uenyekiti wa BAWACHA ili akilikosa jimbo hilo basi aingie Bungeni kwa mgongo wa BAWACHA kama Viti Maalum.

Mwisho, Halima Mdee hawezi kupanga himaya yake kwa wakati huu, halafu akashinda Uchaguzi. Kama hakuweza kuipanga kwa miaka 5 akiwa mbunge hawezi kuipanga kwa hii miezi miwili iliyobakia kuelekea uchaguzi Mkuu.
Asante kwa masahihisho
 
Labda sijaelewa mada, yaani watu 80 wanashindanishwa na mtu mmoja.
 
Mshana Jr kwa Maandalizi na Mikakati niliyoiona na ninayoiona kwa 2020 hii, Afe Mmaasai au Mmang'ati CCM analichukua Jimbo la Kawe rasmi.
 
Inawezekana umeshindwa kuelewa,walochukua fomu hao 80,hawaendi kupambana na Halima Mdee,atakae pambana na Halima Mdee hapo ni mtu mmoja tu,yani ni kama leo Usemi wingi wa wachukua fomu za uraisi chadema wanataka kupambana na Magufuli wakati atakaepanda jukwaani na Mgaufuli ni mmoja tu.
Ila wasowajanja wataelewa kweli watu 80 wanataka kupambana na Mdee,hili nalo ni ajabu la wasiofikiria.
 
Hili linaweza kuwa ajabu lingine la dunia ama linaweza kuingia kwenye kitabu cha rekodi za dunia World Guinness Book of Records, ama linaweza kuvunja rekodi ya nchi na dunia kwa jimbo moja la ubunge kuwa na watia nia wengi kuwahi kutokea na karibia asilimia mia moja wa chama kimoja.

Pamoja na kwamba kibubu cha tume ya uchaguzi ya CCM kitatuna kwa mapato na pengine kuwa jimbo lililoingiza mapato mengi zaidi kwa kuuza form nyingi zaidi lakini madhara yake ni makubwa kuliko hayo mapato.

1. Katika watia nia wote hao 80 nina hakika hawapungui walau 20 wenye nguvu ya pesa, ushawishi ndani ya chama na wale wa mbeleko na vimemo. Kwa kuzingatia hili pekee tayari yatatokea makundi yasiyopungua 10 hivi. Makundi yenye nguvu na misuli ya kila aina. Hapa badala ya kupambana na adui yataanza kupambana yenyewe kwa yenyewe.

Jimbo la Kawe lililomegwa kutoka Kinondoni limekuwa na umaarufu mkubwa kuliko hata Kinondoni yenyewe na hii pengine ni kutokana na jiografia yake na aina ya mtu anayelishikilia.

3. CCM wanalitaka hilo Jimbo kwa hali na mali. Na wamewekeza muda mrefu sana tena kwa gharama kubwa mno. Hivyo kitendo cha kulikosa kitakuwa aibu kubwa, fedheha na hasara kubwa kisiasa.

4. Kitendo cha wanaume na uwekezaji wao wote kuja kushindwa na mwanamke mmoja ni ndoto ya kutisha sana na jinamizi wasilolipenda CCM

5. Kuonesha umwamba na ubabe kuwa wakitaka kitu hawashindwi kwakuwa wana kila kitu kila nyenzo ya kupata ushindi

Ni kwa muktadha huo wa kukamia kulikopitiliza hilo jimbo.. Wamejikuta wanatoa boko. Kwakuwa watatumia muda mwingi sana kwenye:
Mchujo
Kupata tano bora
Kwenye kupata mgombea mmoja
Kwenye kuunganisha makundi
Kwenye kuponya majeraha kabla ya uchaguzi

Kumbuka kila hatua kati ya hizo zote itaacha maumivu kwa kundi fulani
Ni wakati wakihangaika na yote haya Halima Mdee atakuwa busy kuimarisha himaya yake.

Matokeo yake ni nini? Muda utasema

Mshana update taarifa mpaka jana usiku kulikuwa na wagombea 137 wa CCM jimbo la kawe.
 
Back
Top Bottom