Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu hapo kwenye maandishi yaliyokolezwa wino (bold fonts) umemaliza kila kitu. Hilo jambo la kupoteza muda kwenye masuala madogo madogo ambayo hayana muendelezo wa kudumu nimeliongelea sana.
Watu wanataka jambo la kujipatia umaarufu wa haraka ambayo mengi ni mambo madogo ya jawaida sana siyo ya kukusaidia kushinda vita ya kumng'oa mpinzani wako kwenye madaraka.
Yaani ni mambo ya hovyo kabisa. Mkurugenzi wa NEC anaweka pingamizi dhidi ya mgombea halafu anakuwa ndiye mamlaka ya mwisho ya kusikiliza rufaa ya mgombea dhidi ya pingamizi (sick) aliloliweka yeye mwenyewe.
Mwezi mei vyama vya siasa vilipelekewa rasmu ya kanuni hizi ila inasikitisha kuona vyama havikujali wala kuona hatari ya njama zilizofichika ndani ya kanuni hizo.
Ninadhani, hata kama havisemi, vyama vya siasa viko under capacitated au pengine wanaona aibu kutafuta misaada ya policy experts kuwasaidia kuchambua kisha wao watumie refined expert output ku-engage NEC/ZEC.
Na hawajipangi si kwa sababu hawajui vipengele hivyo bali inaonesha ni kwa aidha makusudi au wana ushirikiano wa siri na watawala.
Ikiwa si hivyo KWANINI HAWAKUPIGIA "KELELE" VIPENGELE OVU HIVYO? KUDAI TUME HURU INGALI KUNA VIPENGELE KAMA HIVYO NI "KIPENGELE!!"
UKWELI USEMWE
Mkuu, huwezi kuanza kuomba kitu kikubwa ilhali vidogo hujapewa!! Hebu tazama hizo kanuni hata kama tutakuwa na tume huru itatusaidiaje? Kanuni zingekuwa rafiki hata tume ingekuwa mbaya na mbovu bado wangebanwa ana "wangeliona haya!" Twapaswa kwenda na yote vinginevyo kilio kikuu chajaWapige kele vipi mbona tume huru na katiba mpya wanapiga kelele haipatikani sasa wapige kelele kanuni zilizotokana na sheria mbovu ya tume isiyokuwa huru hayo si ndiyo matokeo ya tume isiyokuwa huru. Kelele zinatosha labda machafuko ndiyo bado.
=Siasa ni kupaza sauti. Sauti za vyama vya siasa (primary stakeholders' voice matters) ina nguvu kwenye maamuzi yahusuya uchaguzi. Their voice matters.We ulikuwa wapi mbona walisema ulitaka wafanyeje kama wao siyo wenye uamuzi wa mwisho. Kuna kanuni zimetolewa kuhusu online contents mdau gani alizijadili na mbona zimekuwa gazetted zinatumika hapo unamlaumu nani. Hii awamu kila hila imeonekana waziwazi hakuna namna ni kwenda nayo sambamba.
Nahisi uelewa wako wa hiyo lugha upo chini ya wastani au umetumia kamusi ya english--swahili ambayo imekupeperushiaNi bahati mbaya sana kuona wapinzani hawajipangi wala kujishughulisha na masuala ya hatari kama haya isipokuwa muda wao mwingi wako 'busy' na trivial issues wakati vichwa vyao vinaelekezwa kibra!
Wewe uko kwenye ushabiki tu au kuendesha distortions za kulinda status quo; wala hujui hata kuwepo kwa conventional principle of impartiality of EMB. Maofisa wa serikali wala Tume hawapaswi kumuwekea pingamizi mgombea isipokuwa mgombea mwenzake. Kanuni hiyo imekuwa ikifuatwa miaka yote isipokuwa uchaguzi wa 2019 na sasa kwenye uchaguzi huu.Nahisi uelewa wako wa hiyo lugha upo chini ya wastani au umetumia kamusi ya english--swahili ambayo imekupeperushia
mbali
Kisome vizuri kufungu Cha nne,ukikielewa kitaondoa kabisa mchecheto wako
Si kila pingamizi lazima likubaliwe,pia mgombea anaruhusiwa kisheria kukata rufaa tume ya taifa ya uchaguzi,hili pia lilifanyika 2015,wakati ulikua shule