Kitchen na dining rooms za watanzania wengi hazitumiki inavyotakiwa. Hivi ni kwa nini?

Kitchen na dining rooms za watanzania wengi hazitumiki inavyotakiwa. Hivi ni kwa nini?

Hiyo yakulia dinning kila MTU na sahani yake ni tumeiga tuu,

Ndio maana kuishi kinamna hiyo inakuwa ngumu,

Sisi kule kijjn watoto wote tulikuwa tunakula pamoja kwenye chombo kimoja yaani Sinia. Hii ilitusaidia kujenga umoja Kama ndugu...

Siku hizi Kula pamoja ni adventure... Kisinia shishi food

Siku hizi kila MTU na sahani yake anakula Kwa muda wake, usipokuwa makini unakuta watoto hawana hata table manners,
Babu sie tulikuwa tunakula kwenye Ungo😀😀😀😀
Kuna mwamba mmoja tulikamatama mikono kwenye kipande cha Kuku,alizima kibatari mhuni yule..ile anepapasa tukagongana,,,aisee nilikula konzi hatari sana siji kusahau...😀😀😀

Nitawajaribu hivyo watoto wangu😀😀😀
 
Kula pamoja katika kisinia ni uchafu wa kulishana mate tu, sawa na wale watu wanaokunywa pombe kutoka chungu kimoja kwa mirija.
😂😂😂😂

Hamna uchafu hapo
Babu sie tulikuwa tunakula kwenye Ungo😀😀😀😀
Kuna mwamba mmoja tulikamatama mikono kwenye kipande cha Kuku,alizima kibatari mhuni yule..ile anepapasa tukagongana,,,aisee nilikula konzi hatari sana siji kusahau...😀😀😀

Nitawajaribu hivyo watoto wangu😀😀😀


Yes mkuu, wataishi kindugu watakuwa wamoja
 
Ule ni utamaduni so kama wewe me au ke ujakulia katika utamaduni huo huwezi hata kulia kijiko ni shida

Nyumba nzuri ya kisasa unakuta sufuria kwenye fosa sitting room mama anakula ukoko wa wali
 
1742837653112.png
 
Hiyo yakulia dinning kila MTU na sahani yake ni tumeiga tuu,

Ndio maana kuishi kinamna hiyo inakuwa ngumu,

Sisi kule kijjn watoto wote tulikuwa tunakula pamoja kwenye chombo kimoja yaani Sinia. Hii ilitusaidia kujenga umoja Kama ndugu...

Siku hizi Kula pamoja ni adventure... Kisinia shishi food

Siku hizi kila MTU na sahani yake anakula Kwa muda wake, usipokuwa makini unakuta watoto hawana hata table manners,
Hatari sana.
Hata ikitokea mmekula pamoja. Mkono moja kijiko mwingine simu.
 
Hii ni sahihi miaka hii wazazi wengi wamekuwa wavivu wa kuwafundisha watoto wao madili ya mezani

Na sisi kama wazazi tumekuwa wavunjaji wa maadili ya mezani mfano kula huku tunatazama televisheni au tumeshika simu mkononi tukiperuzi mitandaoni.

Kwa hiyo wazazi wenyewe nao wanatakiwa wafundishwe maadili ya mezani
​
Samahani mkuu, maadili ya mezani yana faida gani?
 
Inapendeza kuona nyumba nyingi za Watanzania zikiwa na jiko na chumba cha kulia, ila cha kushangaza kitchen (jiko) na chumba cha kulia (dining room) ni kama mapambo tu.

Kwa familia kadhaa au wengi utakuta wanatumia chumba cha nje kupikia maarufu kama jiko la nje wengine wanapikia nje tu tena kibarazani na huku jiko lipo ndani.

Wakati wa mlo Watanzania wanapenda kulia sebuleni. Utakuta chakula kimewekwa kwenye dining table wanajipakulia na kuketi sebuleni au mahali pengine hata nje kabisa au vyumbani.

Hata hawawafundishi watoto wao kula wakiwa wameketi kwenye dining table ni purukushani tu nyumba nzima mtoto anakula au analishwa akimwaga mwaga chakula

Na hii sio tu kwa familia za kipato cha chini na cha kati ni kama kadesturi ka Watanzania wa hali zote

Shida ni nini hasa? Ni ushamba au huu utamaduni wa Kimagharibi umetushinda?

Usije na hoja ya jiko la mkaa.
​
Sasa ugali na mboga Moja unaanzaje kulia dining?
 
Back
Top Bottom