Huyu mzee muone tu vile alivyo. Akiwa mzoefu wa siasa, mtu asiyeyumba na mwenye historia ya kukumbana na vikwazo vingi vya chama dola (CCM) amekuwa mtu wa kutokata tamaa.
Yaliyopita yamepita tokea uchaguzi wa 1995 hadi uchaguzi wa 2015 , CCM ilipodhihirisha kuwa haiko tayari kukabidhi madaraka licha ya miafaka mingi iliyofanywa ili Zanzibar iweze kusonga mbele. Wakati tunaelekea 2020 Zanzibar inaendeshwa bila uwepo wa gnu ambayo ni matakwa ya Katiba. SMT ipo inailinda serikali ya Dr Shein. Maalim hachoki kuwatuliza watu wake na kutaka wasikate tamaa. Taarifa zilizopo si kuwa Wana CCM wameridhika kuendesha serikali Yao bila bubudha lakini Wana hofu hawajui huyu mzee kakusudia nini hasa.
Tayari hofu kuelekea 2020 imewaingia kutokana na kujuwa ukweli kwamba Zanzibar Kuna mgogoro ambao haujapatiwa ufumbuzi. Kinachowapa hofu CCM ni usiri wa maalim Seif juu ya Nini hasa anatarajia kifanyike. CCM Wana hofu kwamba watakwenda kwenye uchaguzi kwa mazingira ya sasa na kusiwe na mageuzi yoyote na wadau wote wa uchaguzi wa ndani na nje watakubali? Ukweli wanajuwa kuwa kuna dhambi ya kidemokrasia ilifanywa na kamwe hairuhusu kufanywa tena uchaguzi kwa mazingira Yale yale.
Zipo taarifa za kuongezeka hofu kutokana na maalim kufanya ziara ya karibuni kule ughaibuni na kuwa kimya Hadi sasa zaidi ya kuwaahidi wafuasi wake kuwa haki Yao itapatikana. Nini kinaendelea hasa ni siri. Jee cuf na maalim Seif ndio wameridhika au kuna nini kuelekea 2020? Jee watashiriki uchaguzi huo kwa mazingira haya. Jee dunia ndio imebariki uchaguzi ule wa 2015 na kwamba wako radhi uchaguzi wa 2020 uendelee bila kufanywa chochote? Hapo ndipo unapomuona maalim Seif na harakati zake akiwa na Siri nzito.
Vyanzo vya uhakika vimethibitisha kwamba harakati za azimio la Zanzibar la vyama na kule kutangulizwa mbele maalim Seif kuongoza harakati hizo kumezidi kuwapa hofu CCM.
Maalim Seif ana siri nzito.
Kishada