Kitendo cha IGP Sirro kutoa hukumu ya Ugaidi wa Mbowe huku kesi ikiwa Mahakamani ni Uhalifu. Napendekeza kesi hiyo ifutwe haraka

SIO POLISI Wote ni wabaya au wanaonea watu lakini mara kadhaa jeshi Hili limelaumiwa sana kwa uongo tena wanaosema huo Uongo ni viongozi wao wakuu...Uzushi...Kuumiza na kujeruhi watu na mengine mengi maovu.

JESHI Hili lina mfungamano Mkubwa sana Na Wanasiasa wa chama chetu kiasi hawawezi kutenganisha kabisa kazi yao na Sisi wana CCM.

Ni wenzetu kabisa lakini Kingine wanadhani Vitisho na kuonea watu itatusaidia sisi Milele.

Ni kweli wengine hatujui matendo ya Mbowe lakini polisi kuanzia miaka ya nyuma wana lawama na madoa mengi..Mahita aliwahi kubumba mavisu akaleta hadharani akisema ameshika makontena..Hatukuona hayo makontena..Yuko anazeeka kwa aibu hana haya.

Sirro unajua kabisa mmeambiwa wazi na Rais mlibambikia watu kesi...kama mm ni wewe nilitakiwa kuacha hiyo kazi mana kwenye kubambika mnaumiza na kudhalilisha watu...Nani atawaamini??? Hamuaminiki...na mnatumia sheria mbaya hizo za ugaidi..Utakatishaji na mengine mengi kuumiza watu.

Hao viongozi wa Serikali waliokua wauwawe na hao akina mbowe ni akina nani??? Mbona Lissu yeye alisemaga anafuatwa na anatishwa hao hawakufuatwa??? Walilalamika wapi???
MSITUHARIBIE HII NCHI...
 
Umeandika kizalendo sana !
 
Boss nawe una kazi! KIla siku ni kutetea Mbowe! Au una nini na yeye?
Polisi ni haki yao kutuhumu uharifu. Ndo maana wanakututusa hadi mahakamani. Na ni kazi yao kushawishi mahakama kwamba ushahidi ni huu! sasa wewe unahangaikaaaaa!
Sema pia Ni kazi ya kubambikia watu kesi
 
Ulisema utoshabikia siasa na ulituaga au umebadilisha gia mkuu
 
Igp kilaza baada ya mahita
 
Mama naskia unakazwa hapo mitaa ya lumumba,bladifakeni
 
Hiyo hukumu iko wapi?
 
Kwani mama yenu mpendwa alisemaje?ukimpinga mama unapigwa laana kama hiyo.DJ awe na adabu asifikiri yupo Casino na libenzi lake na Konyagi.
Pole Ndugu,
Yaonekana dhahiri kuwa umepungukiwa uwezo wa kuelewa hoja iliyopo, matokeo yake washindwa kabisa kujibu wala kujenga hoja imara.
Sijui wanao watakuja kuwa wa sampuli gani.
Ee Mungu twakuomba uwaepushe na kurithi balaa hiyo.
 
Kwani mama yenu mpendwa alisemaje?ukimpinga mama unapigwa laana kama hiyo.DJ awe na adabu asifikiri yupo Casino na libenzi lake na Konyagi.
Pole Ndugu,
Yaonekana dhahiri kuwa umepungukiwa uwezo wa kuelewa hoja iliyopo, matokeo yake washindwa kabisa kujibu wala kujenga hoja imara.
Sijui wanao watakuja kuwa wa sampuli gani.
Ee Mungu twakuomba uwaepushe na kurithi balaa hiyo.
 
Vipi Chadema wanapotoka hadharani na kuongea kwenye press kwamba Mbowe si gaidi wakati kesi iko Mahakamani, hiyo ni sahihi kisheria? Je wao hawajatoa hukumu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…