Kitendo cha Jaji Mugasha kukosoa mamlaka hadharani ni utovu wa nidhamu, sio ushujaa

kwani Yeye Jaji Mugasha yupo chini ya Rais au Jaji Mkuu?
je huoni Jaji Mugasha alitakiwa kwanza ashauriani na Kiongozi wake ambaye ni Jaji Mkuu kisha Jaji Mkuu ndipo aishauri mamlaka ya juu?
Taratibu za Kimahakama hauzijui...tulia endelea kuwa nduza
 
jaji kala kiapo kulinda na kusimamia sheria za nchi sio za Rais.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani katiba imeanza kuvunjwa leo? wakati wa JPM kukataza mikutano ya kisiasa alikuwa wapi? wakati wabunge 19 bila chama wanaingizwa bungeni alikuwa wapi? wakati AG anatolewa alikuwa wapi? katiba ikikugusa wewe tu ndio anakumbuka kuna katiba. hawa wote ni walewale tu
 
Ana miaka mingapi ungesema hapa halafu tujadili. Huyo anataka hata akae mwaka tu kuna maslahi makubwa kuliko kukosa hata mwaka
 
Uungwana ni kitendo. Kitendo kama Cha jaji. Soma maelezo yake. Then, kaa kwa kutulia.
 
Uungwana ni kitendo. Kitendo kama Cha jaji. Soma maelezo yake. Then, kaa kwa kutulia.
soma kwa makini andiko langu, sina tatizo na maoni ya Jaji, anauhuru wa kutoa maoni yake lkn hoja yangu ni utaratibu alio utumia kama kiongozi wa umma.

ama anatumiwa na kundi la watu? kajificha kwenye kivuli.
 
Huyo Jaji kasimamia katiba yupo sahihi sana...wanaachwa Wazee madarakani kwa muda mrefu kwa manufaa ya wachache wanajua wanachokifanya bora kaongea mimi nipo upande wake...
 
Dogo huna akili ya kudadavua
 
Siamini kama huu upupu umeandika wewe...umesahau kuwa kipindi cha jiwe nyie wote mlikuwa chawa pro max!!!
 
Inabidi mtu awe na ujasiri wa uwendawazimu kuitetea katiba.
Wajinga wajinga kama mtoa mada ndio hawajui kuwa kstiba inabidi kutetewa kizalendo.
 
Ana miaka mitatu tuu kustaafu.
Sasa midogo hiyo? yeye akipata hiyo mitatu akija kustaafu ana staafu katika level nyingine kuwa mstaafu judge wa rufaa na judge kiongozi ni big different. Miaka mitatu mingi kwenye position hata miwili inatosha. mama wazi kakereka na hili personal sio kwa faida ya nchi
 
Siamini kama huu upupu umeandika wewe...umesahau kuwa kipindi cha jiwe nyie wote mlikuwa chawa pro max!!!
Hapana uko wrong nenda kwenye post zangu za wakati wa JPM labda 80% nilikuwa namshtumu sana na akifanya vizuri nilikuwa nampa sifa zake lakini sijawahi kukubali kuzuia mikutano wala sera zake za kiuchumi.
 
Jaji ametimiza wajibu wake wa kikatiba wa checks and balances.

Kama hoja zake zina makosa, kosoa hoja zake, usikosoe yeye kutumia uhuru na wajibu wake wa kikatiba.

Wananchi pia wana haki ya kikatiba ya kujua mambo muhimu ya kuhusu nchi yao inavyoendeshwa. Jaji amewatendea haki wananchi kwa kuwatimizia haki yao ya kikatiba kwa kuweka uwazi katika jambo hili.

Tatizo letu mihimili haisimamiani. Haiwajibishani. Tunaweka hizi dhana kwenye maandishi kama urembo tu.

Spika Ndugai kasema nchi inauzwa, halafu badala ya kuisimamia kauli yake na kuibana serikali kuu, kajiuzulu. Huu ni udhaifu.

Tunataka kuona mihimili inawajibishana zaidi, ndiyo point ya kuwa na mihimili katika demokrasia.

Kama hutaki hilo, badilisha nchi iwe absolute monarchy.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…