Kitendo cha kutaka kuhamisha familia 400 zinazozunguka eneo la kimondo cha Ndolezi Mbozi bila fidia ni cha kishenzi

Haya ndo mambo ambayo CHAWA km Mwashambwa wangekuwa wanapigia kelele tena MBOZI ndo kwao kabisa, Yani ni the NYIA BOY lakini yeye utamkuta anabwabwaja mambo yasio ya msingi. Kusifia tu mambo ya hovyo hovyo wakati mambo nyeti km haya huwezi kumuona.
Lucas Mwashambwa anawaza tumbo lake tu!
 
Mpaka sasa hilo eneo hajatokea mjanja ajikatie hati miliki ili wakihamishwa apate madola kadhaa?
 
Mpaka sasa hilo eneo hajatokea mjanja ajikatie hati miliki ili wakihamishwa apate madola kadhaa?
Wananchi walisimama kidete kuhakikisha linabaki kuwa hifadhi ya kijiji hadi hapo serikali kuu ilipolitwaa!
 
Kwani Serikali imesema haitawapa fidia?
 
Watawafukuza halafu wajengee maeneo kwa Ajili ya Utalii wa Kimondo.😂😂😂😂

Mtaja uzwa mazima!
 
Kama wanahamishwa bila fidia wakatae ila kama walivamia eneo la kimondo basi watakachopewa na Serikali ndio stahiki Yao.

Mwendazake asingewapa hata mia kama alivyofanya Kwa vyeti fake na waliopisha ujenzi wa Barabara
 
Kimodo unanifahamu?

Kimondo kilivamia dunia kijiji cha Ndolezi hivyo kama serikali inakitaka haina budi kuwalipa wanakijiji!
 
Wanaotunga sera wanakaa masaki na osterbay hawapo field so madhila hayawahusu.
Wanaotunga sera sio wahanga. Mfano tu WA reli ya SGR unawawekea uzio kuwatenganisha wananchi pande mbili bila kuacha sehemu za kupita wananchi utadhani wote wanamiliki magari
 
Wanataka fidia stahiki na ya haki kulingana na hali ya maendeleo ilivyo! Kifupi hawataki dhuluma!
Watalipwa kama wanavyolipwa fidia stahili Watanzania wengine mahala pengine. Huku Jijini Mwanza watu wamefurahia sana fidia ya SGR. Hope na hao watafurahia!
 
Kama fidia ipo na watu wamekubal nini tatizo? Hio museum unaposema kwan haipo pale? Si kuna bonge la jengo pale ambalo nadhan ndio linahifadhi historia .labda wanataka kuliongezea thamani, tena wakiweka na michezo ya watoto na eneo la byakula na finywaji patakua pazur sana,mana ukiwa mombo sijiu momba hamnaga sehem ya kwenda kutembea zaid ya labda tunduma mabaa
 
Wananchi ndiyo wanakataa kuhamishwa wakidai ni eneo lao la asili na kuna makaburi ya vizazi kadhaa vya wapendwa wao!
 
Ukiwa Tanzania epuka kukaa / kujenga karibu na hifadhi ya mimea, mbuga za wanyama, sehemu zenye madini, watu Kama Lucas Mwashambwa, kimondo, bandari, barabara, matajiri na wanasiasa.
Utanishukuru uzeeni.
 
Hivi inawezekana eeeeenh?
inawezekana na Nina mifano hai ilitokeaga ruvuma ilitokea Lindi pia serikali ilitaka eneo wanchi wakagoma kwasauti moja ila muwe na ushilikiano asiwe chawa kat yenu au mtoa nyeti zenu taarifa no iwe no haswa
 
Na nchi ilivyo na machawa wengi sasa!
 
Nimezaliwa pembeni ya hicho kimondo mita kama 30 hivi, enzi hizo ulikuwa hauwezi kukatisha pale mida ya usiku ikiwa peke yako, kilikuwa kinatoa mwanga mkali sana,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…