Kitendo cha kutaka kuhamisha familia 400 zinazozunguka eneo la kimondo cha Ndolezi Mbozi bila fidia ni cha kishenzi

Nakumbuka nilivokua chuo tulienda kwenye iko kimondo.

Kipo overrated sana.
 
Nimezaliwa pembeni ya hicho kimondo mita kama 30 hivi, enzi hizo ulikuwa hauwezi kukatisha pale mida ya usiku ikiwa peke yako, kilikuwa kinatoa mwanga mkali sana,
Last time niliona kimefubaha. Watu wanajaribu kupiga msumeno. Kichafu.
 
Nakumbuka nilivokua chuo tulienda kwenye iko kimondo.

Kipo overrated sana.
Kiko overrated kivipi? Kwamba siyo kimondo?

Kimondo ni jiwe lililodondoka kutoka angani hivyo ni kivutio hasa kwa wanasayansi kukifanyia uchunguzi na utafiti ili kuifahamu vizuri anga!
 
Last time niliona kimefubaha. Watu wanajaribu kupiga msumeno. Kichafu.
Lipo vile vile miaka yote sema zamani kilikuwa na miujiza yake sio poa, wazee wetu ndipo walipokuwa wanatambikia, vitu kama kimbunga hidaya sijui corona mitaa ile visingeweza kusogea,
 
Chanzo Cha Matatizo(CCM) kipo kazini. Walianza na Ngorongoro tukachukulia poa. Sasa wamehamia Mbeya, wachaga mkae mkao wa kuondoka kandokando ya mlima Kilimanjaro maana huyu CEO wa kampuni hatanii. Atatania na kurembua kwenye kuwachukulia hatua wapigaji wa fedha za umma lakini sio kuhamisha watu ili kuwapa eneo waarabu
 
Na nchi ilivyo na machawa wengi sasa!
huku kulikuwa na MTU 100 tu ilikomboa hekta 1700 ni kijiji wakaja mpaka jwt jamaa wakasema mtuue hapahapa ila eneo hatutoi na hatuhami serikar ikabidi itii amri
 
Less creative

Kijiji kingeachwa na kuboreshwa ili watalii wakija wapige story na Mashuhuda jinsi kimondo kilivyo piga hiyo siku....mijitu inawaza kupiga tu
Kimondo kinaibwa,nilipokua msingi 1990s picha za kimondo kulikua kubwa,juzi nimeona kimepungua,halafu waondoke tu kwa maslahi ya taifa,sisi akina ngosha tulitimuliwa bhulyanhulu kupisha mgodi,na kuuawa juu
 
Less creative

Kijiji kingeachwa na kuboreshwa ili watalii wakija wapige story na Mashuhuda jinsi kimondo kilivyo piga hiyo siku....mijitu inawaza kupiga tu
Umesahau ndani ya miaka 30, kijiji kitakuwa mji, mazingira yote ya asili yanapotea, wale watu walioona kimondo hawapo tena ,

Btw siungi mkono kuwaondoa bila kulipa fidia, ni upuuzi grade A
 
Kimondo kinaibwa,nilipokua msingi 1990s picha za kimondo kulikua kubwa,juzi nimeona kimepungua,halafu waondoke tu kwa maslahi ya taifa,sisi akina ngosha tulitimuliwa bhulyanhulu kupisha mgodi,na kuuawa juu
Utakuwa uliangalia kwa jicho la kengeza vinginevyo kimondo kiko vilevile ukiondoa sehemu chache zilizokatwa kwa msumeno.
 
Serikali ya CCM inajali wanyama kuliko binadamu Watanganyika.

Ukitaka kuthibitisha hili angalia adhabu ya kugonga fisi na binadamu ndipo utajua hali ni mbaya sana
juzi kati tembo alikatiza barabarani bahati mbaya akagongwa paja na basi moja akajeruhika, viongozi wa kijiji wakataoa taarifa kwa wanaohusika na wanyama pori wakaja mbio haraka bila kuchelewa. Lakini wanyama wakiharibu mazao ya wananchi au kujeruhi watu wakipigiwa simu waje wanakuja kwa kuchelewa hawajali maisha ya watu. Wana majibu mabaya kuwa wanyama wana thamani kubwa kuliko watu na wanaingiza fedha nyingi. Mwananchi haingizi fedha kama wanyamapori
 
Hiyo ndiyo akili ya Serikali ya CCM kwao wanyama wana thamani kuliko binadamu
 
Safi sana .

Walianza na wamasai sasa wamekuja kwa wanyaki.

Ngoja wachaga nao wahamishwe maana wanasumbua mlima kilimanjaro.

Kila kabila litafikiwa kwa wakati wake.
 
Nimezaliwa pembeni ya hicho kimondo mita kama 30 hivi, enzi hizo ulikuwa hauwezi kukatisha pale mida ya usiku ikiwa peke yako, kilikuwa kinatoa mwanga mkali sana,
Tafadhali nifahamishe zaidi hili!

Kinatoa mwanga? Kwa maana kina meremeta? Na huo mwanga kwenye kimondo ni baada ya kumulikwa na mbaramwezi?
 
Tafadhali nifahamishe zaidi hili!

Kinatoa mwanga? Kwa maana kina meremeta? Na huo mwanga kwenye kimondo ni baada ya kumulikwa na mbaramwezi?
Nadhani ni hadithi tu za kunogesha Baraza kwa sababu hicho kimondo ni jiwe chuma. Yaani kina madini mengi ya iron (Fe) ambayo hayang'ai na kwa kuwa kiko wazi na kinapigwa mvua na jua kina rangi ya kutu nyeusi au dark brown.
 
Nashukuru kwa ufafanuzi.

Kwa hakika ulichokielezea ndicho nami ninachokijua hicho. Maelezo yake yamenishitua! Hivyo nikataka kujua zaidi.

Nashukuru kwa kuniweka sawa mkuu.
 
Tatizo ni thamani ya hicho kimondo, material yake ni muhimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…