Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Last time niliona kimefubaha. Watu wanajaribu kupiga msumeno. Kichafu.Nimezaliwa pembeni ya hicho kimondo mita kama 30 hivi, enzi hizo ulikuwa hauwezi kukatisha pale mida ya usiku ikiwa peke yako, kilikuwa kinatoa mwanga mkali sana,
Kiko overrated kivipi? Kwamba siyo kimondo?Nakumbuka nilivokua chuo tulienda kwenye iko kimondo.
Kipo overrated sana.
Lipo vile vile miaka yote sema zamani kilikuwa na miujiza yake sio poa, wazee wetu ndipo walipokuwa wanatambikia, vitu kama kimbunga hidaya sijui corona mitaa ile visingeweza kusogea,Last time niliona kimefubaha. Watu wanajaribu kupiga msumeno. Kichafu.
Vyeti fakeKama wanahamishwa bila fidia wakatae ila kama walivamia eneo la kimondo basi watakachopewa na Serikali ndio stahiki Yao.
Mwendazake asingewapa hata mia kama alivyofanya Kwa vyeti fake na waliopisha ujenzi wa Barabara
huku kulikuwa na MTU 100 tu ilikomboa hekta 1700 ni kijiji wakaja mpaka jwt jamaa wakasema mtuue hapahapa ila eneo hatutoi na hatuhami serikar ikabidi itii amriNa nchi ilivyo na machawa wengi sasa!
Kimondo kinaibwa,nilipokua msingi 1990s picha za kimondo kulikua kubwa,juzi nimeona kimepungua,halafu waondoke tu kwa maslahi ya taifa,sisi akina ngosha tulitimuliwa bhulyanhulu kupisha mgodi,na kuuawa juuLess creative
Kijiji kingeachwa na kuboreshwa ili watalii wakija wapige story na Mashuhuda jinsi kimondo kilivyo piga hiyo siku....mijitu inawaza kupiga tu
Umesahau ndani ya miaka 30, kijiji kitakuwa mji, mazingira yote ya asili yanapotea, wale watu walioona kimondo hawapo tena ,Less creative
Kijiji kingeachwa na kuboreshwa ili watalii wakija wapige story na Mashuhuda jinsi kimondo kilivyo piga hiyo siku....mijitu inawaza kupiga tu
Ili polisi wakawapige risasi?gomeni msitoke
ndio mana mnahamiswa hovyohovyIli polisi wakawapige risasi?
Utakuwa uliangalia kwa jicho la kengeza vinginevyo kimondo kiko vilevile ukiondoa sehemu chache zilizokatwa kwa msumeno.Kimondo kinaibwa,nilipokua msingi 1990s picha za kimondo kulikua kubwa,juzi nimeona kimepungua,halafu waondoke tu kwa maslahi ya taifa,sisi akina ngosha tulitimuliwa bhulyanhulu kupisha mgodi,na kuuawa juu
Miaka mingapi hiyo iliyopita mkuuNimezaliwa pembeni ya hicho kimondo mita kama 30 hivi, enzi hizo ulikuwa hauwezi kukatisha pale mida ya usiku ikiwa peke yako, kilikuwa kinatoa mwanga mkali sana,
juzi kati tembo alikatiza barabarani bahati mbaya akagongwa paja na basi moja akajeruhika, viongozi wa kijiji wakataoa taarifa kwa wanaohusika na wanyama pori wakaja mbio haraka bila kuchelewa. Lakini wanyama wakiharibu mazao ya wananchi au kujeruhi watu wakipigiwa simu waje wanakuja kwa kuchelewa hawajali maisha ya watu. Wana majibu mabaya kuwa wanyama wana thamani kubwa kuliko watu na wanaingiza fedha nyingi. Mwananchi haingizi fedha kama wanyamaporiSerikali ya CCM inajali wanyama kuliko binadamu Watanganyika.
Ukitaka kuthibitisha hili angalia adhabu ya kugonga fisi na binadamu ndipo utajua hali ni mbaya sana
Hiyo ndiyo akili ya Serikali ya CCM kwao wanyama wana thamani kuliko binadamujuzi kati tembo alikatiza barabarani bahati mbaya akagongwa paja na basi moja akajeruhika, viongozi wa kijiji wakataoa taarifa kwa wanaohusika na wanyama pori wakaja mbio haraka bila kuchelewa. Lakini wanyama wakiharibu mazao ya wananchi au kujeruhi watu wakipigiwa simu waje wanakuja kwa kuchelewa hawajali maisha ya watu. Wana majibu mabaya kuwa wanyama wana thamani kubwa kuliko watu na wanaingiza fedha nyingi. Mwananchi haingizi fedha kama wanyamapori
Tafadhali nifahamishe zaidi hili!Nimezaliwa pembeni ya hicho kimondo mita kama 30 hivi, enzi hizo ulikuwa hauwezi kukatisha pale mida ya usiku ikiwa peke yako, kilikuwa kinatoa mwanga mkali sana,
Nadhani ni hadithi tu za kunogesha Baraza kwa sababu hicho kimondo ni jiwe chuma. Yaani kina madini mengi ya iron (Fe) ambayo hayang'ai na kwa kuwa kiko wazi na kinapigwa mvua na jua kina rangi ya kutu nyeusi au dark brown.Tafadhali nifahamishe zaidi hili!
Kinatoa mwanga? Kwa maana kina meremeta? Na huo mwanga kwenye kimondo ni baada ya kumulikwa na mbaramwezi?
Nashukuru kwa ufafanuzi.Nadhani ni hadithi tu za kunogesha Baraza kwa sababu hicho kimondo ni jiwe chuma. Yaani kina madini mengi ya iron (Fe) ambayo hayang'ai na kwa kuwa kiko wazi na kinapigwa mvua na jua kina rangi ya kutu nyeusi au dark brown.
Tatizo ni thamani ya hicho kimondo, material yake ni muhimuWananchi wa kijiji cha Ndolezi kilipo kimondo maarufu cha Mbozi wamekuwa wakiishi hapo kabla ya wanasayansi kuthibitisha kuwa jiwe lile ni kimondo, hivyo kulipa jiwe hilo hadhi ya pekee kulinganisha na mawe mengine yaliyopo kijijini hapo.
Baada ya uthibitisho huo wanasayansi, watalii, na watu wengine wadadisi kwa mamia wamekuwa wakitembelea eneo hilo. Hapo awali ilikuwa kutembelea eneo hilo ilikuwa bure kabisa lakini baadaye serikali ikaweka ada ya kuliangalia jiwe hilo. Jambo hilo halikuwa baya kwani kijiji na serikali vilipata fedha kwa ajili ya shughuli za maendeleo.
Tofauti na awali ambapo wanakijiji walifurahia kupokea wageni na kunufaika kiuchumi sasa jiwe lile (kimondo) limezua balaa. Wananchi wanatakiwa kuondoka eneo hilo ili serikali ijenge wigo kwa ajili ya wanyama wa porini (Zoo) ili kuongeza vivutio kwa watu wengi zaidi kutembelea eneo hilo.
Kitendo hicho hakikubalika kabisa na hasa kuwaondoa wananchi bila stahiki na fidia za mali zao. Kwa nini serikali hii inayojinasibu kuheshimu haki za binadamu inataka kuwafanyia dhuluma wananchi wake kwa sababu ya wanyama wa porini? Kwani hakuna vivutio vingine nchi hii zaidi ya wanyama? Kwa nini serikali hii inapenda kuanzisha migogoro isiyo ya msingi na wananchi wake?
Hii inaonyesha wazi kabisa kuwa serikali hii haina watu wabunifu, wamekaririshwa kuwa wanyama pekee ndiyo kivutio cha utalii. Hivi haiwezekani serikali kujenga nyumba ya makumbusho (Museum) ambayo kwanza itachukua eneo dogo lakini pia itahifadhi vitu vya kale na vya utamaduni wa jamii ya watu wa mkoa wa Songwe. Pili itawawezesha wananchi wanaoishi eneo hilo kuendelea kukaa kwa amani na kuendeleza shughuli zao za kiuchumi.
Wakati umefika kwa serikali kujisafisha kwa kuondoa watumishi wanaokosa ubunifu katika kutekeleza majukumu yao na kuajiri wanaoweza kubuni miradi ambayo itawanufaisha wananchi na serikali kupata kipato bila kuathiri maisha ya watu na mazingira yaliyopo!