Kitendo cha kutengua maamuzi wafugwa wa kunyogwa ni cha kisiasa

Mh hizi records zako hapana.Mwinyi na Nyerere wamenyonga watu wengi tu.Ila Mkapa na Kikwete ndo hawakunyonga
 
Mkapan alinyonga wangapi? Kikwete alinyonga wangapi?

Wakati dunia inaendelea kukemea capital punishment wengine hapa wanatetea.
 

Mkapa alinyonga wangapi? Kikwete alinyonga wangapi? Tuanzie hapo.
 
Akili yako haina akili
 
Maamuzi ya Rais sio ya kisiasa.
Amefanya jambo linalokubalika kisheria na katiba ya Nchi imempa Mamlaka hayo.
Kasome Ibara ya 45 alafu urudi hapa
 

Kanywe maji, utulie halafu hasira ikipungua soma ulichoandika kisha kifanyie marekebisho muhimu.
Nashauri hivyo kwa sababu, mtu akisoma hapa, anaona hisia zaidi kuliko maudhui.
 

Njia rahisi tu bunge ni la chama kimoja ni rahisi kupeleka sheria ya kifo ikafutwa! Sio kuweka siasa. Kama Maraisi hawawezi kufuata sheria basi wabadilishe.
 
Shida kubwa MUNGU anasema neno moja tu USIUE. Kwa njia yoyote hutakiwi uue. MTU anayekujia ili AKUUE huyo inabidi KUJILINDA kwa njia yoyote ikiwa pamoja ikishindikana kumwua. Hapa hakuna neno. Hao waliohukumiwa wengine wamesingiziwa. Yule mfungwa aliyetolewa baada ya miaka 18 marais wangekuwa wametoa ruhusa wanyongwe si angekuwa amekufa kwa uonevu? Ametoka na kusema wako wenzake wengi waliohukumiwa kifo na hawamjui hata waliemwua. HALI hii ukiwa rais huna haja ya kuidhinisha hukumu kwa vile kuna huo uonevu. Sijui ni nini lakini nasikia ukishikwa wanakubandikia murder unaunganishwa kwenye kesi ambayo huijui. FIKIRIA HUYU ALIYETOKA ALIUNGANISHWA VIPI KTK KESI ILE NDIO UJUE HAKUNA HAJA YA KUTOA VIBALI VYA KUNYONGWA. Mfungwa aliyenyongwa anajutaje alilofanya?
 
Well said. Wako wapi Azory, Ben Saanane na chupuchupu Lissu? Nani kaua? Tuache kiki za kipuuzi.
 
Tatizo nyie mnawasikiliza sana wanasiasa..ulizeni askari walioko pale Gereza la Isanga Dodoma kama unapita mwezi bila watu kula kitanzi.sio Jiwe,kikwete wala watangulizi wao ambao hawajanyonga watu...huku kwenye makamera wanawaongopea tu..
 
Lakini inakuwa fundisho. Kungekuwa kuna kunyongwa kwa wauwaji hata mauaji yangepungua.
Kumnyonga binadamu hadi afe sio kitu kidogo kiboboso
Pamoja na kwamba ni sheria lakini watekelezaji ni binadamu wenye imani zao na mioyo☺
 
Kama huwezi kuuwa basi huwezi kuwa Amiri Jeshi mkuu maana unapoliamiri Jeshi kwenda vitani, unawapeleka wanajeshi kwenda kuuwa watu. Simple as that.
 
Tatizo nyie mnawasikiliza sana wanasiasa..ulizeni askari walioko pale Gereza la Isanga Dodoma kama unapita mwezi bila watu kula kitanzi.sio Jiwe,kikwete wala watangulizi wao ambao hawajanyonga watu...huku kwenye makamera wanawaongopea tu..
Amini kwambaa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Yani huwaga nakuwa mgumu sana kuamini kuwaa watu hawanyongwiii...!!
 
Mimi nampongeza hata kama maamuzi yake yalikuwa ya kinafiki. Nikuambie tu. Hukumu ya kunyoga haimfanyi aliyeua kupata funzo
Si kila adhabu hutolewa ili kumfunza mkosaji...adhabu nyingine hutolewa ili iwe funzo kwa wengine...mkosaji unakua tu case study,unatolewa sadaka ili ipatikane jamii safi...na ndo mana makosa mengi yana minimum and maximum sentences... unajua kwanini?
 
Mimi nampongeza hata kama maamuzi yake yalikuwa ya kinafiki. Nikuambie tu. Hukumu ya kunyoga haimfanyi aliyeua kupata funzo
hivi hujiulizi kwanini SIRIKALE imeweka sheria ya hukumu ya kunyongwa ujinyee mpaka ufeee au ndio utopolo wa lumumba unakusumbua kwenye makalio maana nsikia akili zenu zimikimbilia HUKO
 
Ukiongelea haki za binadamu unageneralize sana...ongelea death penalty na uonyeshe ni wapi na lini Tanzania imeiondoa hiyo adhabu ya kifo? hivi vitu so vya siri...tusiweke conspiracy kwenye kila kitu...Art 14 ya CURT inaonyesha kila kitu kuhusu hilo.

Hao Marekani wenyewe bado wanatekeleza adhabu ya kifo.
 
Njia rahisi tu bunge ni la chama kimoja ni rahisi kupeleka sheria ya kifo ikafutwa! Sio kuweka siasa. Kama Maraisi hawawezi kufuata sheria basi wabadilishe.
Hata wewe hapa unaleta siasa,mambo ya bunge kuwa chama kimoja yamekujaje?ndio maana nasema tatizo hapa ni magufuli na si suala la kutofuata sheria wala nini kwa sababu hata angewanyonga bado angeonekana ameweza kutekeleza sheria hiyo bila tabu kwa sababu anajulikana ni muuwaji kama kawaida.

Kumchukia mtu ambaye huwezi kumfanya kitu ni kujitia stress tu.
 
Wewe jamaa mimi siandiki conspiracy. Hizo ishu zinafundishwa madarasani.

Wapi hujaelewa?

Mbona sijakataa kwamba watu hawahukumiwi? Nilichosema ambacho ndicho hali halisi ni kwamba utekelezaji hua haufanywi badala yake aliyehukumiwa hukaa for life.

Kitu rahisi kama hicho unataka kukianzishia ubishi?

Marekani hawatekelezi hiyo adhabu. Kuna majimbo yanatekeleza na mengine hayatekelezi.

Sadam Hussein kesi yake iliendeshwa Marekani ila adhabu ikatolewa ikatekelezwe Iraq. Kwanini? Kwasababu Marekani akiwa kama advocate wa Human Rights ingemuwekea picha mbaya kuitekeleza ile adhabu kwenye ardhi yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…