Halafu mtu ukimwambia kuwa wewe humkosoi Magufuli bali unamchukia,anakataa. Yani mtu hataki huyo Magufuli afanye lolote anataka aendelee kufanya mabaya ili azidi kumchukia na kumsema na watu wengine zaidi nao wamchukie,sasa huku sio kukosoa bali ni chuki.
Yani watu walikuwa wanyongwe wafe, ila kwa kuwa aliyetengua uamuzi huo wa kunyongwa ni Magufuli basi mtu hajapendezwa na huo uamuzi sababu tu umefanywa na Magufuli,ni kwamba bora wangenyogwa wale watu ili Magufuli azidi kuonekana mbaya na hicho ndio anachokipenda.