Kitendo cha Lema na Familia yake kupewa Asylum Canada kinaashiria Taifa limeanza kutengeneza wakimbizi wa kisiasa, jambo ambalo halina afya

Kwa wanasiasa nguli dhidi ya utawala uliopo hawako salama...muulize mdude
 
Eti atapata kazi nzuri

Kitaaluma Lema ana fani gani? Tuanzie hapo kwanza.

Kwa taarifa yako Ugaibuni kama huna taaluma ya kueleweka utaishia kubeba mabox

Ukibeba box ughaibuni utakuwa na kipato kizuri tu. Kuliko kuishi kikondoo hapa bora ukabebe box ughaibuni. Kama huamini siku serikali ya Canada itangaze watanzania wanaotaka kubeba box Canada waende, utashangaa mpaka watu watu wanaofanya kazi TRA, TANAPA nk wanaacha kazi wanaenda kubeba box Canada.
 
Kwahiyo nawwe unaamini kabisa kwamba Lema alikua anatishiwa uhai wake na watawala.

Sio kwamba ninaamini, ndio ilivyo. Mambo yanayofanyika sasa hivi dhidi ya wapinzani wa kweli, tunayaona kwa macho yetu wala sio ya kuhadithiwa.
 
Nahitimisha kwa kusema wewe ni kilema wa fikra, hufai kuwepo Tanzania leo na kesho.
 

Balozi Slaa alihamiaje kule baada ya vijimambo vilee?
 
Ukimbizi wanajitengenezea wenyewe, mbona huo Ubalozi wa Canada haukumuuliza Lema kipindi akiwa jambazi wa kuiba magari aliua watu wangapi kama kweli kafanyiwa veting ya kutosha kabla ya kupewa hifadhi ya ukimbizi?

Vijana wengi wanakaa mitandaoni kuongea pumba ukiuliza umewahi kufanyia nini nchi yako hawana jibu? Unapanga kufanyia nini nchi yako hawajui. wamebakiza madongo yasiyo na msingi na ushabiki tu. Hii ndiyo sababu nchi yetu inaingia kwenye udikteta! Tuna vijana wengi sana ambao bado hawana upeo kama huyu. Inawezekana upeo mdogo ni umri au kuhujumiwa na propaganda
 
Canada iko wazi kwa mtu yeyote kuhamia huko. Yaani ukijihisi tu unahitaji kwenda huko unaenda.

Bosi wangu alikuwa muarabu mkataba wake ulipoisha mwaka jana akatimukia Canada.
 
Nahitimisha kwa kusema wewe ni kilema wa fikra, hufai kuwepo Tanzania leo na kesho.

Ni kweli ni kilema wa fikra kwa mtu mwenye mitazamo ya kikomunisti kama ww. Kwanza ungesema nina fikra sahihi ningeshangaa sana, ingebidi niangalie nimekosea wapi. Ni hivi, enzi za kutawala watu kwa shuruti zimeisha, watu watakaa kimya sio kwa kuridhika, bali ni kwakuwa wakionyesha hisia zao tofauti na watawala, watauwawa, kuhujumiwa njia zao za kuwaingizia kipato, kutekwa na madhila mengine kama hayo. Lakini ukweli tumechoka kutawaliwa kwa shuruti. Kama ni bwawa la umeme, reli, barabara nk, hata makaburu wa Afrika kusini walijenga maana walikuwa wanakusanya kodi. Iweje leo tutawaliwe kwa shuruti na wezi wa kura, kisa tu kuna reli ya mkopo inajengwa?
 



Tusubiri kuna waziri amewekwa kabisa kushughulikia mitandao hii ili Watanzania wafugwe midomo kabisa. Wameanza kupiga marufuku whatup group za wafanyakazi wa serikali na watajaribu kufunga mitandao baada ya hapo ni nchi ya kunyamaza na kusubiri kuambiwa kila kitu. Upigaji kura umeshakuwa bure! ni ndani ya nyama tu!. Waliwaambia mkafikiri uzushi sasa mtaona tunakoenda. Ushabiki mbaya hamkuwasikiliza sasa Watanzania wote tutakuwa watumwa
 
Lema kakimbia madeni
 
Ukimbizi wanajitengenezea wenyewe, mbona huo Ubalozi wa Canada haukumuuliza Lema kipindi akiwa jambazi wa kuiba magari aliua watu wangapi kama kweli kafanyiwa veting ya kutosha kabla ya kupewa hifadhi ya ukimbizi?
Jeshi letu la polisi na mahakama zetu walimwuliza hilo swali? Au wao.hawajui? Ingekuwa vizuri ungelisaidia jeshi la polisi maana una taarifa za kutosha
 

Uza ubongo huo maana unakaa nao kwa hasara. Kizazi hiki sio cha hizi propaganda zako za kizee.
 
We unajua aliwekeza bei gan ktk harakati za kutaka kurejea Bungeni?
Atawekeza ngapi kwa ubunge wa Arusha mjini? Kama ni uungwaji mkono alikuwa nao, hakuna mbunge wa upinzani anayeweza kuhonga wapiga kura maana wapiga kura wengi wa upinzani wanamkubali mtu sio kwa rushwa. Kama alitumia nyingi haikufika 100m. Fahamu kuwa hakuweka bango hata moja, hakugawa tshirt ama vyakula, na mikutano hakuwa anafanya kila siku.
 
Amekimbia madeni yake yaliyosomwa bungeni ya milioni zaidi ya 400?

Lema unazidi kuwachafua zaidi wachaga, dawa ya deni ni kulipa siyo kukimbia na kujifanya mkimbizi feki, sasa umekimbilia kwa wazungu watakupa kazi ya kuosha vibibi na vibabu.
Jamani uzi unajieleza vizuri, mbona mnaleta masihara ktk issue nyeti kwa taifa letu? Tujitafakari tumekosea wapi mpaka tunaanza kutengeneza wakimbizi. Sifa ya taifa letu inaharibika. TUTAFAKARI kwa kina!
 
Nimesoma huu ujinga umeandika hapa nikacheka kwa nguvu. Eti wazungu wanataka tugombane ili waje wachukue raslimali zetu miaka hata mia ijayo. Mpaka sasa tuko na hizo raslimali bila hao wazungu kuwepo, mbona sio matajiri? Huu ujinga mmeupata ukubwani au ni wa kuzaliwa nao?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…