Kitendo cha Lema na Familia yake kupewa Asylum Canada kinaashiria Taifa limeanza kutengeneza wakimbizi wa kisiasa, jambo ambalo halina afya

Kitendo cha Lema na Familia yake kupewa Asylum Canada kinaashiria Taifa limeanza kutengeneza wakimbizi wa kisiasa, jambo ambalo halina afya

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Hivi mnafikiri hao wazungu ni wajinga sana?

Wazungu wanajua kila kitu, isitoshe wana mabalozi wao hapa, kwahiyo kama kuna hali mbaya hawahitaji kinca Lema wakimbie ndio wajue kuna hali mbaya.

Wanajua kabisa kwamba hao kina Lema wanaenda tu kula bata baada ya kushindwa ubunge ila kwamba kuna hali mbaya au la, wanajionea wenyewe.

Kwa taarifa yako hao wazungu mpaka wakupe ukimbizi lazima wajiridhishe na vielelezo vyako. Huyo Lema kapata ukimbizi maana ana ushahidi wa kutosha na ambao hata sisi tunaujua. Siasa zetu ndani ya hii miaka mitano wote tumeziona, uonevu na unyanyasaji kwa wapinzani uko wazi.

Na kwa kukusaidia tu ni kuwa Lema kaula, watoto wake watapata elimu nzuri, yeye na mkewe watapata kazi zinazowalipa kuliko wangekaa hapa. Yaani kakutana na bonge la neema ya kimaisha.
 
Canada mji gani ?Nipo Montréal huku Québec Baridi kali sana. Semeni mji alipo tukamtembelee. Karibu Canada nchi yenye asali na maziwa. Sasa tatizo hajasoma. Ila itambidi asome hata nursing assistant mwaka mmoja hasa mkewe ili afanye kazi na baadae anaweza endelea kusoma zaidi. Hapa kama haujasoma utaishia kufanya kazi supermarket ingawa nazo zinalipa. Watoto watasoma vizuri Elimu Bora kabisa. Bienvenue dans le Canada. Mimi nipo huku francophone.
 
Ni ujinga huo, wala hakuna la maana hapo! Mtu mzima unaamua kujipeleka utumwani wewe pamoja na familia yako! Watoto wake watapoteza mengi hapa duniani, Kizazi cha tatu cha Lema ndicho kitakuja kuinjoi maisha huko kwani ujinga wa Babu yao mzaa Baba au Mama ( ambaye ni Lema wa sasa) wa kukimbia Nchi yake kwa sababu za kutunga zitakuwa zime-fade away!
 
Huwezi kuwekeza kiasi chote hicho ukahama nchi. Alizitumbua hana kitu
Kama maisha yake yalikuwa hatarini kama yeye mwenyewe alivyosema,,basi alikuwa sahihi maana uhai hauna mbadala.
 
Ndiyo mikataba waliyokuwa wameingia kwamba wahamasishe vurugu, zikifaulu au kushindikana watapewa makazi. So makubaliano yanatekelezwa.

RIP Acacia Mining, Pole Barick, Heko JPM. Vita ya kiuchumi tutashinda.
 
Kwa taarifa yako hao wazungu mpaka wakupe ukimbizi lazima wajiridhishe na vielelezo vyako. Huyo Lema kapata ukimbizi maana ana ushahidi wa kutosha na ambao hata sisi tunaujua. Siasa zetu ndani ya hii miaka mitano wote tumeziona, uonevu na unyanyasaji kwa wapinzani uko wazi.

Na kwa kukusaidia tu ni kuwa Lema kaula, watoto wake watapata elimu nzuri, yeye na mkewe watapata kazi zinazowalipa kuliko wangekaa hapa. Yaani kakutana na bonge la neema ya kimaisha.
Kaula kisa kaenda Canada?

Wazungu siyo wajinga, wanajua Lema kaenda kula tu maisha.
Ni ujinga tu kujiita makamanda alafu unakimbia kitisho cha kwenye simu.
 
Ninapata shida sana kuelewa ulichoandika unachomaanisha, najiuliza lini Lema aliwahi kushiriki kuuza madini ya Tanzania kwa Canada?

0Mkuu,

Your thread is emotionally polarized.

Wewe mpaka unaandika huu uzi uko Tanzania au nje ya Tanzania ?

Kama uko ndani ya Tanzania, je kuna mazingira hayo unayodai yamefanikisha huyo mtu wako kupata hadhi ya ukimbizi?

Hao wasomi unaodai waishauri serikali kutumia rejea ipi iliyothibitishwa na mamlaka halali za kitaifa na kimataifa?

Kupata hifadhi kwenye nchi kama Kanada (Quebec/Ottawa) ni mkakati wa kiuchumi kwa kuwa wawekezaji wengi wa madini ambao mikataba yao iligundulika kuwa ilikuwa ya kitapeli wanatokea huko (Reference Barrick Gold Mines & Associates).

Lema anauzandiki mkubwa sana yuko tayari kuuza utu, hadhi ya nchi ili mradi apate mali kwa yeyote.

Siasa huwa ni vichaka vya watu wenye historia mbaya, tabia mbovu na ukosefu wa maadili kwa baadhi yao kukimbilia huko kama kinga ya maovu yao.

Tambua uhalifu wote chanzo chake ni wanasiasa hasa wanaharakati ( Study on criminality, criminology and & crimes Source)

Mleta mada huyo aliyekimbia ni mwenzio kwa kumbukumbu tulizonazo hivyo amekutuma kupima joto la kisiasa litaashiria kitu gani kwa wananchi . The methodology you have agreed on to surface through a vagued political barometer survey shall not sustain teh status quo.

Huyo yumo kwenye mnyororo wa mamluki, usaliti na pandiki uasi dhidi ya nchi yake kwa kisingizio hawakubaliani na kiongozi wa nchi aliyeko madarakani kutokana na kudhibitiwa utukutu wao. Any elect regime that comes to power through the citizens endorsement and performs in accordance with teh citizen will he shall stay until such time.....so do not stir up panic among the good people of the lovely Tanzania and strangers enjoying its gracious haven peace.

WAPINZANI WASAINI MIKATABA NA KUWAUZIA MADINI CANADA, alisikikika msomi mmoja wa Tanzania akiandika hapa JF
 
Akae huko huko, nchi haijapoteza chochote maisha yanaendelea. CCM oyee

Yaani ni kwakuwa hakuna uwezekano wa kila mmoja wetu kuondoka hapa nchini, ingewezekana Canada waturuhusu tunaotaka kwenda huko, hapa nchini mngebaki nyinyi wazalendo uchwara muendelee na maisha ya dhiki. Maisha atakayoishi Lema na familia yake ni ya hali ya juu, huku watoto wake wakipata elimu bora, watoto wake watakaporejea hapa nchini watapata ajira nzuri, kuliko watoto waliosoma kwenye shule za kata.
 
Kama maisha yake yalikuwa hatarini kama yeye mwenyewe alivyosema,,basi alikuwa sahihi maana uhai hauna mbadala.
Usanii tu, nani amuue? Kwa threat gani aliyonayo kwa taifa? Mbona wapinzani wengine hawajauliwa hadi sasa hivi? Yeye ana nini cha ziada kuliko Mbowe, sugu , mnyika na wengine wengi ambao hawajakimbia nchi?

Ule msemo wake "hakuna kitu kibaya kama uoga " Leo imekuaje? Hana lolote huyo alikuwa anatafuta maisha mteremko ameshayapata atulie huko huko.
 
Hivi ule unyama mliokuwa mnatenda kwa miaka yote mitano na mauaji , utekaji na utesaji wa raia kwenye uchaguzi , huku ikiagizwa Lema auliwe ama apewe kesi isiyo na dhamana mnadhani dunia ilikuwa haioni ?
Wacha aende ila mwambie asije kudokoa huko, atfungwa au kubanwa shingo na goti.
Huko watu huacha magari yana funguo saa zingine, sasa akilishobokea imekula kwake.
 
Kaula kisa kaenda Canada?

Wazungu siyo wajinga, wanajua Lema kaenda kula tu maisha.
Ni ujinga tu kujiita makamanda alafu unakimbia kitisho cha kwenye simu.

Ukitaka kujua kwenda Canada ni kuula kimaisha, leo hii Wacanada waseme wanaotaka kwenda Canada waende, uone kama hamjabaki wazalendo uchwara tu hapa nchini. Yaani kwa kwenda Canada atakuwa na maisha bora kuliko aliyokuwa nayo hapa akiwa mbunge.
 
Yaani ni kwakuwa hakuna uwezekano wa kila mmoja wetu kuondoka hapa nchini, ingewezekana Canada waturuhusu tunaotaka kwenda huko, hapa nchini mngebaki nyinyi wazalendo uchwara muendelee na maisha ya dhiki. Maisha atakayoishi Lema na familia yake ni ya hali ya juu, huku watoto wake wakipata elimu bora, watoto wake watakaporejea hapa nchini watapata ajira nzuri, kuliko watoto waliosoma kwenye shule za kata.
Unamuonea wivu pole sana. Utaendelea kuwepo hapa hapa bongo land tuisome namba kwa pamoja.
 
Hivi kipindi cha mkwere kweli hatukupata wakimbizi wa kisiasa kama sasa hivi
Kumbuka Lema anaongezeka kwenye list ya Lissu,Gurumo na hatujui nani atafuata labda Henche & Mbowe
 
Wacha aende ila mwambie asije kudokoa huko, atfungwa au kubanwa shingo na goti.
Huko watu huacha magari yana funguo saa zingine, sasa akilishobokea imekula kwake.

Kwa jinsi maisha yalivyo duni hapa nchini, ni bora ukabanwe shingo na mzungu huko Canada, kuliko kukaa hapa kwenye dhiki.
 
Ukitaka kujua kwenda Canada ni kuula kimaisha, leo hii Wacanada waseme wanaotaka kwenda Canada waende, uone kama hamjabaki wazalendo uchwara tu hapa nchini. Yaani kwa kwenda Canada atakuwa na maisha bora kuliko aliyokuwa nayo hapa akiwa mbunge.
Hivi atakuwa anapewa kila kitu bure au kuna namna atawezeshwa aweze kupiga Moshe zake halafu Lema anapenda sana Moshe za forex & cryptocurreny naona huko ndio ameenda sehemu sahihi
 
Unamuonea wivu pole sana. Utaendelea kuwepo hapa hapa bongo land tuisome namba kwa pamoja.

Nitaacha kumuonea wivu wakati amekuwa mbunge kwa miaka kumi, na sasa ameenda kupata maisha bora zaidi ya alivyokuwa mbunge, tena kwa hila za hawa hawa viongozi wetu?
 
Wazee wa kutekana na kupotezana watanunaje!! "Missing in Action"
 
Upo umuhimu wa wasomi na wataalam wetu kuliangalia ili suala kwa macho mapana na kuishauri serikali. Tusione Canada wanatoa hifadhi kwa Watanzania tukakaa kimya, tujiulize tumefikaje hapa?

Ikumbuke kwa mujibu wa sheria za kimataifa ukimbizi ni hadhi unayopata baada ya wataalam kukaa na kujiridhisha kwamba unastahili.

Kama lema na familia yake wamekubaliwa hifadhi ni udhibitisho kwamba wamepita kwenye mchujo nakufauli, wameweka ushahidi nakuishawishi Canada kuwapokea. Familia yake itaishi kwa raha na watoto watasoma vizuri zaidi ya hapa ila kila siku kwa maika dahari ya Taifa letu watabaki kusomwa kwenye hiztoria ya Taifa letu Kama tunavyowasoma akina Kambona.

Tujitafakari mara nyingine Tena, Tanzania si sehemu salama? Kama Ni sehemu salama kwanini marafiki zetu wa muda mrefu Canada wanautangazia Ulimwengu kwamba tuna wakimbizi wakisiasa? Tujadiliane nao tulifute doa ili na lema na familia yake warejee nchini kuendelea na siasa.

Tulizoea haya kutokea kwa majirani zetu na tuliyakemea ikiwemo viongozi wetu waandamizi kushiriki kuwarejesha nchini kwao wakimbizi wakisiasa...tunalo jukumu lakufuta sifa hii mbaya iliyomea na inayostawi.
Tanzania ni sehemu salama sana, mbona mimi na familia yangu tunaishi kwa amani tu? Msipende kuchochea ujinga, huyu dogo Lema ni mjanja tu, alishasoma alama za nyakati na akaona kukaa miaka 5 bila kazi na ana watoto ataishije, so akaamua kudanganya mabwana zake ili akapakatwe majuu.
 
T
Kwa jinsi maisha yalivyo duni hapa nchini, ni bora ukabanwe shingo na mzungu huko Canada, kuliko kukaa hapa kwenye dhiki.
Teremkia south africa nawe ukimbie maana naona ndiko watu wa kutoka sudani wanapitia, na wewe nenda hujabanwa.
 
Nitaacha kumuonea wivu wakati amekuwa mbunge kwa miaka kumi, na sasa ameenda kupata maisha bora zaidi ya alivyokuwa mbunge, tena kwa hila za hawa hawa viongozi wetu?
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] wapenda kitonga bana, fanya kazi dogo...au pambana na wewe ukawe mbunge wa upinzani..mkishindwa uchaguzi ukaombe hifadhi nchi za nje. Simple tu
 
Back
Top Bottom