Nchi kama Canada na Amerika (USA) bado zinahitaji sana watumwa. Baada ya biashara ya utumwa kufutwa, nchi hizi zimeendelea kupata watumwa kutoka hasa mabara ya Afrika na Asia kwa mbinu tofauti mbali mbali hususani kutoa free vissa na green cards kwa ye yote anayependa kwenda kuishi nchini kwao na kufanya kazi hizo za utumwa. Mbinu nyingine ya kupata watumwa hawa ni kutoa political assylums kwa wakimbizi (refugees) mbali mbali. Lengo ni kupata vibarua kwenye shughuli mbali mbali za kiuchumi nchini kwao hususani shughuli za usafi mahotelini, kwenye viwanda, majumbani, majeshini, super markets na kadhalika kwa malipo duni; kama ilivyokuwa wakati huo wa biashara za watumwa!
Canada ndiyo nchi inayoongoza duniani kwa biashara hii. Sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kuwa Canada ni nchi kubwa sana kwa eneo lakini ina wakazi wachache sana. Kwa ukubwa wa eneo, Canada ni nchi ya pili duniani. Ina kilomita za mraba 9.985 million yaani ni zaidi ya China (9.597m), USA (9.834m), India (3.287m). Nchi ya Russia ndiyo ya kwanza duniani kwa ukubwa wa eneo (17.1m km za mraba).
Pamoja na kuwa na eneo kubwa kiasi hicho Canada ina idadi ya watu (population) milioni 37.8 tu. Yaani inapitwa kwa mbali na nchi ndogo sana ya UK ambayo eneo lake la mraba ni 0.242m lakini idadi ya watu wake ni millioni 68. USA angalao wana watu 331 million. China na India kila moja ina watu zaidi ya 1.3 billion! India ina watu 1.380 bilioni na China ina watu 1.439 bilioni kwa takwimu za 2020.
Hivyo Canada kuna ombwe (vacuum) kubwa sana la watu. Inawalazimu kufanya hicho wanachokifanya cha kuokoteza watumwa kutoka maeneo mbali mbali duniani. Hawana option nyingine kwani watu wao hawapendi kuzaa na sasa hivi ndiyo mbaya zaidi kwani wanaoana wa jinsia moja - yaani mwanaume anaoa mwanaume mwenzake na mwanamke anaoa mwanamke mwenzake.
Tunakutakia kila la kheri ndugu yetu Lema kwenda kujaza hilo ombwe la watu lililoko Canada. Tunaomba tu utuchungie wanao wasije wakaiga hizo tabia zingine zisizofaa za wakazi wa huko.