Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,984
Mwaka 2021 umeanza kwa kutangazwa kodi au tozo ambazo awali hazikuwepo. Tumesikia ukaguzi wa magari, garama za kuagiza magari zimepanda mara mia, tozo katika bidhaa nyingi za nje nk.
Hii inaashiria vyanzo vya mapato vilivyomo nchini vikilinganishwa na miradi tunayoanzisha nakusimamia vinakinzana. Gharama za miradi zipo juu kuliko uwezo wetu wa kukusanya. Misaada nayo imeshuka kutokana na covid na diplomasia yetu ya kimataifa kukosa mwelekeo na mtu sahihi wakuisimamia.
Tunachokwenda kuvuna huko tuendako ni ongezeko la watu wasio na ajira kwa sababu sekta binafsi inakwenda kudidimia....Bora Kodi ndogo inayolipwa na watu wengi kuliko kutegemea Kodi kubwa inayolipwa na watu wachache, Wizara ya fedha irudi kwenye maltiplier effects zitokanazo na kila transaction yakibiashara nchini.